Kodi hizi ni halali au mnataka tufe?

Kodi hizi ni halali au mnataka tufe?

Nimefungua kiduka changu nikiwa na mtaji wa million moja,

nimeenda TRA wakanipigia hesabu ya kulipa 150,000 Kwa mwaka huu 2017.

Sijakaa kidogo wamepita watu wa leseni kwenye hii manispaa ya Ubungo
Wakadai natakiwa kulipa 151,000 Kwa mwaka la sivyo kiduka kinatiwa kufuri.

Maswali yangu Kwa wahusika wa kodi hizi zote
mnataka sifa ?
Au mnalengo lingine wa wavuja jasho?

Hawezekani mtaji wa million moja mchukue TRA ichukue 150,000 na Manispaa 151,000 Kwa mwaka.

Wahusika mnajua Pesa ilivyo ngumu mtaani.
b5601f80c9cf66aa3fa979997178fef5.jpg
8e72b691743697e8b3341b9f971017ed.jpg
 
Kiongozi ninachosema kimenikuta,wametuma kikampuni chao cha kufuatilia lesen mitaani yaani nikilio wilaya mpya ya ubungo.

Si unajua kibongo bongo mtu akilipa TRA anajua kamaliza sasa wakaibuka watu wa leseni wakidai wametumwa na Manispaa na hayo ndio yaliotukuta
TRA walifanya makadirio ya mauzo yako kwa Mwaka?
 
Nimefungua kiduka changu nikiwa na mtaji wa million moja,

nimeenda TRA wakanipigia hesabu ya kulipa 150,000 Kwa mwaka huu 2017.

Sijakaa kidogo wamepita watu wa leseni kwenye hii manispaa ya Ubungo
Wakadai natakiwa kulipa 151,000 Kwa mwaka la sivyo kiduka kinatiwa kufuri.

Maswali yangu Kwa wahusika wa kodi hizi zote
mnataka sifa ?
Au mnalengo lingine wa wavuja jasho?

Hawezekani mtaji wa million moja mchukue TRA ichukue 150,000 na Manispaa 151,000 Kwa mwaka.

Wahusika mnajua Pesa ilivyo ngumu mtaani.
Mmeyataka wenyewe tulieni sindano ziingie...
 
Mbona TRA huwa wanasema kuwa sheria inataka mwenye mauzo kuanzia milioni nne kwa mwaka ndiyo anastahili kuanza lipia kodi na oia kama kakadiriwa 150,000 anatakiwa alipe kila baada ya miezi mitatu robo ya 150,000.Isitoshe kodi hawatozi kwenye mtaji huwa wanatoza kutokana na mwenendo wa utakachopata kama kikizidi milioni nne kwa mwaka.itakuwa ajabu kama watakuwa wanafanya tofauti na sheria au wacheki kwa namba 0800780078 nilishawahi ulizia hapo maswali na kuoata majibu.
 
  • Thanks
Reactions: ADK
hapa nadhani yaipasa Serikali ipitie mifumo ya ukusanyaji wa Kodi ili kuondoa Utitiri wa kodi kwa wafanyabiashara.

Eidha iondoke manispaa ibakie TRA peke yake, au iondoke TRA na Kubaki Manspar ili kuondoa Usumbufu kwa wadau.
 
Mtumishi wa umma unakatwa kodi kila mwezi, eti ukichukua mkopo benki serikali inakata kodi pia katika huo mkopo.

The difficult thing to understand in the World is the Income tax- Albert Einstein
 
Nimefungua kiduka changu nikiwa na mtaji wa million moja,

nimeenda TRA wakanipigia hesabu ya kulipa 150,000 Kwa mwaka huu 2017.

Sijakaa kidogo wamepita watu wa leseni kwenye hii manispaa ya Ubungo
Wakadai natakiwa kulipa 151,000 Kwa mwaka la sivyo kiduka kinatiwa kufuri.

Maswali yangu Kwa wahusika wa kodi hizi zote
mnataka sifa ?
Au mnalengo lingine wa wavuja jasho?

Hawezekani mtaji wa million moja mchukue TRA ichukue 150,000 na Manispaa 151,000 Kwa mwaka.

Wahusika mnajua Pesa ilivyo ngumu mtaani.
Pole mkuu sisi wafanyabiashara wadogo tunaumia ila kuna mijitu inafurah sana kwa kuwa wanakula bure na kulala bure kwa mashemej zao! huu ni mtego wa panya hatujui kesho utamnasa nan?
 
hapa nadhani yaipasa Serikali ipitie mifumo ya ukusanyaji wa Kodi ili kuondoa Utitiri wa kodi kwa wafanyabiashara.

Eidha iondoke manispaa ibakie TRA peke yake, au iondoke TRA na Kubaki Manspar ili kuondoa Usumbufu kwa wadau.
Ukusanyaji kodi wa sasa hivi ni mkomoeni trust me.

Kodi zinaumiza sana asikwambie mtu.
Sasa awamu hii ni kukomoana tu.
 
Nilianzishaga biashara ya taxi kodi 840,000/= (miezi 3), mansions 61,000/=, bado service juu yao, naomba ubavuni.125,000/=. Abiria wenyewe wa kuunga unga .
 
Nimefungua kiduka changu nikiwa na mtaji wa million moja,

nimeenda TRA wakanipigia hesabu ya kulipa 150,000 Kwa mwaka huu 2017.

Sijakaa kidogo wamepita watu wa leseni kwenye hii manispaa ya Ubungo
Wakadai natakiwa kulipa 151,000 Kwa mwaka la sivyo kiduka kinatiwa kufuri.

Maswali yangu Kwa wahusika wa kodi hizi zote
mnataka sifa ?
Au mnalengo lingine wa wavuja jasho?

Hawezekani mtaji wa million moja mchukue TRA ichukue 150,000 na Manispaa 151,000 Kwa mwaka.

Wahusika mnajua Pesa ilivyo ngumu mtaani.
Hizo ndio kodi zenyewe, komaa kwenye kuwavutia wateja kwa kutoa huduma nzuri. uzuri wa TRA unaweza lipa kwa awamu nne kwa mwaka hivyo lipa ya nusu mwaka huku unaendelea na biashara japo kuwa mwaka wenyewe umeshaisha ikifika mwezi julai unalipa tena.
kila la kheri kiongozi
 
TRA walifanya makadirio ya mauzo yako kwa Mwaka?
TRA ndio walikadilia 150,000 baada ya kuwaambia nina mtaji wa million moja,
Ila hawa manispaa waliowapa kazi kampuni ya ukusanyaji kodi ndio hawaelewi na mchine yao.wanakuambia unatakiwa ulipe kiasi 150,000 na 1000 ya form sasa ukibisha wananunua kufuri ,wanafunga eneo la kazi.

Ila nahisi mkuu wa kaya hajui.

Ili kuhakikisha hii tunawaomba wahusika wa manispaa waje wilaya ya Ubungo waone watu wa leseni walicho tufanya.
 
Hizo ndio kodi zenyewe, komaa kwenye kuwavutia wateja kwa kutoa huduma nzuri. uzuri wa TRA unaweza lipa kwa awamu nne kwa mwaka hivyo lipa ya nusu mwaka huku unaendelea na biashara japo kuwa mwaka wenyewe umeshaisha ikifika mwezi julai unalipa tena.
kila la kheri kiongozi
Asante sana kiongozi, nilisha umia hapa kwa TRA,leseni, pango, umeme, usafi na Ulinzi ngoja nikomae baada ya mwaka nione, ijapo kila mwaka kodi inapanda sasa
 
TRA ndio walikadilia 150,000 baada ya kuwaambia nina mtaji wa million moja,
Ila hawa manispaa waliowapa kazi kampuni ya ukusanyaji kodi ndio hawaelewi na mchine yao.wanakuambia unatakiwa ulipe kiasi 150,000 na 1000 ya form sasa ukibisha wananunua kufuri ,wanafunga eneo la kazi.

Ila nahisi mkuu wa kaya hajui.

Ili kuhakikisha hii tunawaomba wahusika wa manispaa waje wilaya ya Ubungo waone watu wa leseni walicho tufanya.
Tafuta mwongozo mzee vinginevyo utafanya kazi faida wanachukua wao
 
Lipa tu ndugu
Mabombadia yataendwshwa vp bila kodi zenu.
 
Mkuu, Lipa Kodi tu. Wala usisite. Uliona wapi Serikal ina shamba au mashamba? Unadhan pesa wanazolipwa wabunge,mawaziri,wakuu wa mikoa,wa wilaya na watekaji zinatoka wapi?lipa kodi tafadhari.
 
Back
Top Bottom