Kocha mpya wa Simba SC Patrick Aussems atambulishwa rasmi leo

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
Mabingwa wa soka Tanzania Bara, Klabu ya Simba 'Wekundu wa Msimbazi' ya jijini Dar es salaam, leo imemtambulisha rasmi kocha mpya Mbelgiji Patrick Aussems, ambaye anatarajia kuifundisha klabu hiyo kuelekea kwenye maandalizi ya msimu mpya wa ligi kuu Tanzania bara sambamba na michuano ya Kimataifa.

Kocha Aussems amesaini mkataba wa mwaka mmoja mbele ya Kaimu Rais wa Simba, Salim Abdallah (Try Again) pamoja na Kaimu Makamu Rais Idd Kajuna, kukinoa klabu hiyo akichukua nafasi ya Pierre Lechantre raia wa Ufaransa aliyemaliza muda wake mwezi uliopita.
FB_IMG_15320009600432250.jpg
 
Huu ugonjwa wa wazungu sijui utaisha lini tanzania. Kocha wa maana hawezi akafunga safari kutoka ulaya akaja tanzania.
 
Huu ugonjwa wa wazungu sijui utaisha lini tanzania. Kocha wa maana hawezi akafunga safari kutoka ulaya akaja tanzania.
Mwafrika akienda kufanya kazi ulaya anakuwa wa maana. Ila mzungu akifunga safari kuja Afrika kufanya kazi si maana..Ugonjwa huu utaisha lini?
 
Klabu ya soka ya Simba 'Wekundu wa Msimbazi' ya jijini Dar es salaam, leo imemtambulisha rasmi kocha mpya Mbelgiji Patrick Aussems, kuifundisha Klabu hiyo kuelekea kwenye maandalizi ya msimu mpya wa ligi kuu sambamba na michuano ya Kimataifa.

Kocha Aussems amesaini mkataba wa mwaka mmoja kukinoa klabu hiyo akichukua nafasi ya Pierre Lechantre raia wa Ufaransa aliyemaliza muda wake.View attachment 813259
Kocha hajui kiswahili hafu wachezaji karibia wote wanajua kiswahili na hawajui Kiinglish wala kifrenchi. Watapata tabu sana
 
Mwafrika akienda kufanya kazi ulaya anakuwa wa maana. Ila mzungu akifunga safari kuja Afrika kufanya kazi si maana..Ugonjwa huu utaisha lini?

Mishahara ya maana iko kwao. Kocha mwenye sifa za maana hawezi kutoka huko akaja huku. Umewahi kusikia mchezaji ametoka ulaya akaja africa kucheza mpira?
 
Kwa mtazamo wako huo. Lakini hujui lengo la klabu ya Simba SC
Ni saidie wewe ni lipi.


Najua presha yetu kubwa ni kwenye mechi za kimataifa msimu ujao?

Pia nahisi wameona kama kocha kashindwa kagame atawezaje caf.
 
Ni saidie wewe ni lipi.


Najua presha yetu kubwa ni kwenye mechi za kimataifa msimu ujao?

Yah..lengo nikufanya vizuri kutetea ubingwa wa VPL na kufuzu makundi michuano ya kimataifa. Kwa hivyo Djuma siyo mbaya lakini kwa klabu ya Simba anatakiwa kocha zaidi ya Djuma, ndio maana kwenye mkutano wa leo wanasema Kocha huyu Aussems mpaka kupewa kazi imetokana kukidhi vigezo kuelekea kwenye lengo la Klabu na falsafa ya klabu ambayo safari hii benchi la ufundi lilishirikisha wataalamu wa tano wa mpira ambao walimpa interview na kuridhika na kocha huyu.
 
Back
Top Bottom