Kocha Mkuu Sven Ven Der Broeck aachana na Simba SC

Shark

JF-Expert Member
Jan 25, 2010
29,459
29,154
SIMBA SC YAACHANA NA KOCHA SVEN

DAR ES SALAAM: JANUARI 07, 2021

#HABARI: KLABU ya SIMBA SC imetangaza kuachana na kocha wake Mkuu Sven Vanderbroeck kwa makubaliano ya pande zote mbili.

Taarifa kutoka katika Klabu hiyo imeeleza kuwa, nafasi ya Kocha huyo itakaimiwa na kocha msaidizi, Selemani Matola.

Vanderbroeck akiwa na Simba amefanikiwa kuchukua Ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, FA, Ngao ya Jamii na kuifikisha timu hiyo hatua ya makundi katika ligi ya Mabingwa Afrika.

uhurudigital_20210107_8.jpg
 
Tetesi zinazosambaa kwa kasi ni kuhusu Sven (Kocha wa Klabu ya Simba) kuachana na Simba SC.

Sababu zinazotajwa kumuondoa Simba SC ni matatizo ya kifamilia huku Sababu zingine zikielezwa kua ni kushindwa na Uongozi wa Simba SC.

Je ikiwa ni kweli Sven kaachana na Simba SC hii haiwezi kua hatari kwa Simba?
 
Kama mkataba wake umeisha sawa, lakini kama bado ana mkataba hawezi kuondoka kienyeji. Ni lazima kwanza akae mezani na mwajiri wake wazungumze namna ya kuvunja huo mkataba.
 
Back
Top Bottom