Tatizo kubwa hapa kwetu sio kocha gani anafaa kufundisha taifa stars, bali ni mfumo mzima wa timu zetu kuanzia ngazi za vilabu. Hata kama tukampa Sir Ferguson hii timu hawezi kuleta miujiza, kwa sababu atawatumia hawa hawa akina J Jabu, Nadir, Ngasa, Ndinti, Dihile, Samatta, Mgosi, kwa sababu ndio tilionao.
kazi ya kocha wa timu ya taifa huwa sio kufundisha mpira kwa mchezaji mmoja mmoja, kazi ya kocha wa timu ya taifa huwa ni kuunganisha uwezo alionao kutoka ktk club yake za mchezaji mmoja mmoja na nakutengeneza mfumo mmoja wa uchezaji ili kuleta mafanikio kwa timu kwa ujumla.
Kwa hio mimi nionavyo ni kuwa tatizo letu ni uzalishaji wa wachezaji wanastahili kuchezea ktk ngazi ya vilabu na baadae kuitwa timu ya taifa kwetu ndio tatizo.
Mfano haiwezekai timu itengeneze nafasi na kuingia kwenye box zaidi ya mara 20 lakini wanashindwa kufunga magoli.
Sasa hio sio kazi ya kocha wa timu ya taifa, ni jukumu la mchezaji mwenyewe na trainning ya kutosha kule aliko lelewa ki-mpira.
Suluhisho
1. Sports academy karibu kila wilaya
2. kufufua michezo mashuleni
3. Iwepo kwenye kipaubele cha nchi kwa zababu ni ajira
4. Kila club inayo shiriki ligi kuu iwe na progaramme za watoto kam u-12, u-17, u-21 na timu senior timu
Hapo ndipo tutakapo thubutu kushindana na timu za Nigeria, Cameroon, Senegal, Misri, na nyingine nyingi.