Klopp alitabiri mshindani wa Liverpool FC itakuwa Liverpool FC yenyewe. kifupi haitakuwa na mshindani!

Titicomb

JF-Expert Member
Jan 27, 2012
11,329
17,832
Ni jambo la kushangaza kidogo, unaweza kujiuliza alitoa wapi ujasiri na maono hayo?
Kabla ya kuanza msimu wa Ligi Kuu Uingereza wa 2019/2020 meneja au kocha mkuu wa Liverpool FC akiwa katika ziara ya maandalizi msimu mpya (pre-season preparation tour) nchini Marekani katika jiji la New York mnamo mwezi July 2019 alisema

"Mshindani wa Liverpool siku zote itakuwa Liverpool FC yenyewe, kuongeza kwa tamaa au njaa [ya mafanikio] na ukuaji wa pamoja haitakuwa mahitaji bali ni sheria."

'During the introductory meeting on Lexington Avenue, Klopp insisted Liverpool's greatest competitor will always be itself. An increase in greed and collective growth is therefore "not a demand, but the law." ' source: http:s//www.espn.com

Maelezo hayo yanasimuliwa na shabiki na mwandishi maarufu wa habari za michezo hasa za Liverpool FC mwanadada Melissa Reddy akiandika habari zake chini ya ESPN.

Kwa matokeo ya Liverpool kungoza ligi tofauti ya pointi 22 baada ya kucheza mechi 25 bila kupoteza mechi, sare 1 na kushinda mechi 24 hadi leo tarehe 13 February 2020, kuzifunga timu zote za ligi kwa msimu huu angalau mechi moja, inaonesha sio bahati bali ni mikakati ya Klopp na jumuiya yote ya Liverpool FC.

Hakika LFC haina mpinzani na kwa hakika mpinzani wa Liverpool ni Liverpool yenyewe, maneno yake yametimia kama unabii.
 
Jurgen Klopp ni genius wa soka. Ni kocha mwenye falsafa nzuri sana za mpira na ana tactical nounce inayomweka kwenye level ya peke yake.

Ni kocha ambae anauwezo wa kumbadili mchezaji garasa kuwa world class player. Ameirudisha Liverpool kwenye level yake inayostahili.

Kule kwenye uzi wetu huwa ninaandika kwamba Klopp anaweza akanichukua hata mimi akaniweka kwenye kikosi na tukashinda mechi.
 
Kule kwenye uzi wetu huwa ninaandika kwamba Klopp anaweza akanichukua hata mimi akaniweka kwenye kikosi na tukashinda mechi.
Kweli kabisa, juzi nimekutana na dingi mmoja ni shabiki mwenzetu akaniambia mbona hajaona makali ya Minamino nikamwambia anawezaje ku judge performance au adaptation ya mchezaji kwenye team kwa mechi tatu?

Nikamuuliza anakumbuka Fabinho alipotua Liver ilimchukua mda gani kuanza first eleven? Akanijibu ndio nikamwambia atulie Klopp huwa anajua namna ya kum-intergrate mchezaji kikosini taratibu alafu ana tick.

Angalia kwa sasa LFC kila player akipewa nafasi anafanya kweli mpaka unashindwa aanze nani abaki nani.
 
Mashabiki wa Liverpool bwana; yaani timu kuonesha kushinda ligi kuu ya Uingereza kwa msimu mmoja ndo maneno yamekua mengi sana. Hizi tambo uwezi kuzisikia kule Juve wala PSG wala Barca wala Man City kwa misimu miwili mfululizo.

Kwahiyo Clopp amekua Gen kwa Liverpool lakini hakuwa wakati almanusura aishushe Dot daraja kule Bundesliga.
 
Mashabiki wa Liverpool bwana; yaani timu kuonesha kushinda ligi kuu ya Uingereza kwa msimu mmoja ndo maneno yamekua mengi sana. Hizi tambo uwezi kuzisikia kule Juve wala PSG wala Barca wala Man City kwa misimu miwili mfululizo.

Kwahiyo Clopp amekua Gen kwa Liverpool lakini hakuwa wakati almanusura aishushe Dot daraja kule Bundesliga.
Mzee huu moto wa liver haujaanza msimu huu, kama unakumbuka msimu uliopita liver alipoteza kombe kwa point, pia alikosa ucl fainali, kwahiyo kinachofanyika msimu huu ni muendelezo wa misimu iliyopita
 
Back
Top Bottom