KLM imeshindwa kutua Kilimanjaro kisa hakuna umeme

TheForgotten Genious

JF-Expert Member
Jan 18, 2014
995
1,508
Hii nchi bwana ina umbumbu Sana, yaani kiwanja cha ndege cha kimataifa kinakosa emergency Power system?

Ndege ya KLM imeshindwa kutua usiku huu Kilimanjaro na kulazimika kwenda kutua Dar baada ya kukosekana kwa umeme.

=====

Mdau anasimulia:

“Ni kitu cha kusikitisha sana aisee.

Nilikuwepo ndani ya hiyo ndege. Kwenye screen ilikuwa inatuonyesha 20 minutes to land in Kilimanjaro lakini tunaona ndege haina muelekeo.

Baada ya muda screen ikachange ikasema 1hr 20 minutes to land tukashangaa tukajua kuna shida hapa.

Baada ya muda pilot akatutangazia kwamba runway ina shida taa haziwaki zimeharibika na haijulikani zitatengemaa saa ngapi na ndege mafuta yanaisha kwa hiyo tunenda Dar. Tukashtuka sana.

Kwa hiyo wakatuleta Dar ndege imeshehena watalii wana plans zao kibao tight za kwenda mbuga za wanyama. Aisee ni shida!

Tumefika Dar wametuchukua na vi-coaster kutusambaza hoteli mbali mbali watutafutie ndege kesho za kutupeleka KIA.

Njiani kicoaster chetu kikazima hakina mafuta🤦🏽‍♂️, dereva akaweza kukiwasha tena akaingia petrol station. Kuingia petrol station nako hakuna mafuta wako empty🤦🏽‍♂️.

Tumekaa pale watalii hawana habari what is going on hakuna mtu wa kuwaambia kinachoendelea. Ikabidi nitake charge kuwatuliza na kuwaelezea situation. Basi dereva akaweza kumtuma bodaboda baada ya muda akaja na kidumu kina mafuta wakatafuta chupa ya maji kavu pale wakaikata kuifanya iwe funnel wakamwagia mafuta tukasepa tukaletwa hotelini.

Sasa ndio wanatafutia watu ndege za kwenda KIA kesho.

Kwa kweli kitendo cha runway kuharibika taa kimetusononesha sana kwa kutuharibia plans zetu nyingi.

Halafu wale wasafiri waliokuwepo KIA wakiisubiri KLM ambao wanaenda zao sehemu mbali mbali duniani ina maana na wao wameachwa solemba pale KIA, waliiona ndege juu wakajua tunachukuliwa mara ikasepa🤦🏽‍♂️.”
 
Hii nchi bwana ina umbumbu Sana, yaani kiwanja cha ndege cha kimataifa kinakosa emergency Power system ?

Ndege ya KLM imeshindwa kutua usiku huu Kilimanjaro na kulazimika kwenda kutua Dar baada ya kukosekana kwa umeme
Aisee
 
Mbona ni aibu Sana jamani, Sasa zile juhudi za mama na Royal tour Si zitakuwa tunaziaribu na kupoteza trust kwa wageni....tatizo ni Nini....?
 
Hii nchi bwana ina umbumbu Sana, yaani kiwanja cha ndege cha kimataifa kinakosa emergency Power system ?

Ndege ya KLM imeshindwa kutua usiku huu Kilimanjaro na kulazimika kwenda kutua Dar baada ya kukosekana kwa umeme
Kwahiyo ilishindwa kwenda kutua hata arusha kuliko kurudi hadi dar? Na hizo hasara nani analipia ...au mmi ndo nipo dunia yangu sielewi
 
Hii nchi bwana ina umbumbu Sana, yaani kiwanja cha ndege cha kimataifa kinakosa emergency Power system ?
Jirani yangu kuna apartment building la Mtanzania-Mhindi mmoja, ana wapangaji wazungu kibao, hataki ujinga, getini hapo kafunga generator kubwa, inawaka automatically. Sasa raia anamiliki generator ambayo serikali haina. Wauze land cruiser moja tu ya Katibu Tawala wa Wilaya ($100,000 jumlisha kodi, jumla $200,000), watapata generator za kutosha airport zote 10 za nchi hii
 
Chakushangaza nini wakati viongozi wakiumwa wanatibiwa nje.

Ndani hakuna huduma bora hizo wanazotudanganya nazo kwenye Media

Back
Top Bottom