Klabu bingwa Afrika: Simba ugenini kuchuana na Al Merrekh

Shadida Salum

Journalist at JamiiForums
Sep 11, 2020
69
150
IMG_20210306_104437_139.jpg
Al Merrekh watawakaribisha wababe wa Msimbazi katika Dimba la Al Hilal huko Khartoum saa kumi jioni, katika mchezo huo Wasudan watatafuta kupata ushindi wao wa kwanza katika hatua ya makundi ya mashindano hayo

Al Merrikh watawakaribisha Simba SC ambao wameshinda michezo yote miwili ya ufunguzi ya hatua ya makundi

Simba wanapewa nguvu na ushindi uliopita dhidi ya AS Vita Club ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Al Ahly ya Misri, huku timu hiyo ya Sudan ilishindwa kupata alama hata moja kutokana na mechi zao mbili dhidi ya timu hizo.

Miamba hiyo ya Msimbazi ilichukua ushindi wa bao 1-0 ugenini dhidi ya AS Vita kabla ya kuangusha mabingwa hao wa Afrika bao 1-0 jijini Dar es Salaam wakati Al-Merrikh, walipata kichapo cha mabao 3-0 ugenini kwa Al Ahly mjini Cairo kabla ya kukubali kichapo cha mabao 4-1 dhidi ya AS Vita wakiwa nyumbani kwenye mchezo wa pili

Licha ya kupata jeraha wakati wa mechi yao ya mwisho ya Ligi Kuu Bara dhidi ya JKT Tanzania, kipa Aishi Manula anatarajiwa kuanza katika mchezo huo, baada ya kuthibitishwa na madaktari wa timu.

Kocha Didier Gomes Da Rosa kwa kiasi kikubwa anaweza kuweka safu ya kuanzia ambayo iliwakabili na kuwashinda wapinzani wa kundi hilo hapo awali kwakuwa lengo lake ni kufuzu robo fainali .
I
Michezo mingine itakayopigwa hii leo ya michuano hiyo ni kati ya TP Mazembe dhidi ya Mamelodi Sandowns, Teungueth dhidi ya MC Alger, Keizer Chiefs dhidi ya Petro de Luanda, ES Tunis dhidi ya Zamalek, Al ahly dhidi ya Vita Club na Wydad AC dhidi ya Horoya
 
GEMBESON

JF-Expert Member
Apr 15, 2012
998
1,000
Kila la kheri Mnyama mkali.

Ushindi wenu ni furaha kwa Watanzania wote. Nilishangaa siku Mlipoifunga Al Ahly kuna shabiki mmoja wa Yanga nae alikuwa anarukaruka kushangilia ushindi. (Huyu jamaa huwa anaichukiaga sana simba).

Leo tena natamani kumuona akisuuzika na roho yake kwa soka safi la Simba.
 
Renzo Barbera

JF-Expert Member
Dec 8, 2015
668
1,000
Usiku wa deni haukawii kukucha.

El Merreikh Vs Simba
Leo ndio kipimo cha kwanza kigumu, simba leo atafungwa 2-0 na hatopata goli hata la offside.

Simba akipata goli ntakojoa kuanzia hapa Ununio mpaka Chamwino Dodoma.

Leo ndio ile siku ukuta wa simba utaabishwa kama alivyosema mchambuzi nguli wa michezo Jeff Lea

El Merreikh tunawategemea sana
 
Tate Mkuu

JF-Expert Member
Jan 24, 2019
7,538
2,000

Ngoja sasa waje wenye simba yao wakuporomoshee matusi. Maana umechokoza mzinga wa nyuki. 🏃🏃🏃
 
alumelunda

JF-Expert Member
Dec 30, 2016
796
1,000
Usiku wa deni haukawii kukucha.

El Merreikh Vs Simba
Leo ndio kipimo cha kwanza kigumu, simba leo atafungwa 2-0 na hatopata goli hata la offside.

Simba akipata goli ntakojoa kuanzia hapa Ununio mpaka Chamwino Dodoma.

Leo ndio ile siku ukuta wa simba utaabishwa kama alivyosema mchambuzi nguli wa michezo Jeff Lea

El Merreikh tunawategemea sana
Kwann washabiki wa Yanga ahadi zinakuwa ni hizo, ipo siku mtawatoa ahadi za madingi zenu
 
tamsana

JF-Expert Member
Jan 13, 2012
917
1,000
Usiku wa deni haukawii kukucha.

El Merreikh Vs Simba
Leo ndio kipimo cha kwanza kigumu, simba leo atafungwa 2-0 na hatopata goli hata la offside.

Simba akipata goli ntakojoa kuanzia hapa Ununio mpaka Chamwino Dodoma.

Leo ndio ile siku ukuta wa simba utaabishwa kama alivyosema mchambuzi nguli wa michezo Jeff Lea

El Merreikh tunawategemea sana
Kwani ni lazima kuapia mambo ambayo hayawezekani? Ukisema simba leo inafungwa ingetosha tu mkuu.
Anyway, 'wanasema ni wivu tu'
 
Malyenge

JF-Expert Member
Jan 16, 2012
6,291
2,000
Usiku wa deni haukawii kukucha.

El Merreikh Vs Simba
Leo ndio kipimo cha kwanza kigumu, simba leo atafungwa 2-0 na hatopata goli hata la offside.

Simba akipata goli ntakojoa kuanzia hapa Ununio mpaka Chamwino Dodoma.

Leo ndio ile siku ukuta wa simba utaabishwa kama alivyosema mchambuzi nguli wa michezo Jeff Lea

El Merreikh tunawategemea sana
Mkojo ukiisha kabla hujafika Chamwino utafanyaje?
 
Tate Mkuu

JF-Expert Member
Jan 24, 2019
7,538
2,000
Mimi nitafarijika mkifungwa ili kuwepo na utulivu hii wikiendi. Mkishinda mtachonga sana! Na pia hatuta kunywa maji.
 
Mwifwa

JF-Expert Member
Apr 3, 2017
37,081
2,000
Usiku wa deni haukawii kukucha.

El Merreikh Vs Simba
Leo ndio kipimo cha kwanza kigumu, simba leo atafungwa 2-0 na hatopata goli hata la offside.

Simba akipata goli ntakojoa kuanzia hapa Ununio mpaka Chamwino Dodoma.

Leo ndio ile siku ukuta wa simba utaabishwa kama alivyosema mchambuzi nguli wa michezo Jeff Lea

El Merreikh tunawategemea sana
Kil la kheri mkuu, andaa mkojo wa kutosha kwani umbali hadi Chamwino si wa kitoto
 
Feisal2020

JF-Expert Member
Nov 15, 2018
472
1,000
Usiku wa deni haukawii kukucha.

El Merreikh Vs Simba
Leo ndio kipimo cha kwanza kigumu, simba leo atafungwa 2-0 na hatopata goli hata la offside.

Simba akipata goli ntakojoa kuanzia hapa Ununio mpaka Chamwino Dodoma.

Leo ndio ile siku ukuta wa simba utaabishwa kama alivyosema mchambuzi nguli wa michezo Jeff Lea

El Merreikh tunawategemea sana
Sio kwa ubaya, ila mashabiki wengi wa uto ni wendawazimu
 
feyzal

JF-Expert Member
Apr 20, 2016
5,359
2,000
Mlianza kua AS Vita mlivyopigwa, mkahamia Al ahly tukawalamba na sasa mmekuja El Merrekh nasema MTAPIGWA TU MPAKA MCHAKAE UTOPOLO.
1614977066881.jpg
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom