Habari za jumapili ya leo wapendwa wanaJamiiForums.
Leo katika kanisa la Kiinjili la kiluteri Tanzania, Singida Usharika wa Emanueli (msalaba mrefu)
Nimetokea kupenda kauli ya msaidizi wa Askofu Singida, baada ya Mh. Lazaro Nyalandu Mbunge wa Maliasili na Utalii kuwa mmoja ya washiriki wa ibada kanisani akiwa na wasindikizaji wake katika safari ya kwenda Dodoma kuchukua form baada ya kutangaza nia yake ya Urais.
Kauli kutoka kwa msaidizi wa askofu, kasema, " Kanisa halina chama ila waumini wake ndio wenye chama" kafafanua zaidi kasema wapo CHADEMA, CCM, CUF na n.k
Hii ni kwamba wagombea wengi wanakimbilia sehemu za ibada kuwa sehemu zao za kupigia kampein au kutoa sera zao, musaidi wa askofu amempongeza mh. Lazaro Nyalandu kwa kutembelea sehemu za ibada na kuachana na imani za kukimbilia kwa sanga tit kujipatia mahirizi.
Hali ikoje huko mlipo katika sehemu zenu za ibada?
Nawasilisha
Mr. Asubuhi sana