NAUNGA MKONO HOJA
,
MIMI NI MUUMINI WA KKKT NILISHAWAHI KULETA UZI KAMA HUU
sikubaliani na viongozi wa KKKT kutokukemea maovu,kutokusimama upande wa HAKI,siukubaliani na viongozi wa KKKT kutumia madhabahu takatifu za MUNGU kuwa dodoki la kuwasafisha wanasiasa...
imeandikwa nyumba ya Mungu kanisa itaitwa nyumba ya sala ,wala sio pango la kuwasafisha wanasiasa
Mwingine ni fisadi, au tapeli lakini atahudhuria kanisani kama ilivyo ada, na wala haendi kwa lengo la kubadilika, bali anakwenda pale kama sehemu yake ya kusitiri maouvu yake..
Ndugu yakumbuke maneno ya Bwana.. “Nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala; bali ninyi mmeifanya kuwa PANGO LA WANYANG’ANYİ”.
Usiigeuze nyumba ya Mungu kuwa ni sehemu yako ya maficho ya dhambi zako…bali pageuze kuwa mahali pa sala, mahali patakatifu pa kukujenga roho yako. Kadhalika nyumbani kwa Mungu sio mahali pa kwenda umevaa nusu uchi, umevaa vimini, au umepaka wanja na lipstick, au umenyoa kiduku, kwa ufupi sio mahali pa kutangaza mwili wako au biashara yako…pale ni mahali pa kumheshimu Mungu.
Kama Bwana alizipindua zile meza za wafanya biashara kwenye nyumba yake, hatashindwa kuipindua biashara ya kuuza mwili wako huo usio na staha uliokuja kuuza pale kwenye nyumba yake. Kama umeamua kutangaza biashara ya mwili wako, yapo mapango mengi huko mitaani, lakini usijaribu kuiguza nyumba ya Mungu kuwa kama mojawapo ya mapango hayo.
Mfano kamili wa leo, mtu atatoka kufanya uasherati, lakini mtu huyo huyo jumapili atakwenda kanisani…jumatatu atarudia kufanya kile kile kitu na kurudi tena kanisani, jumapili inayofuata…Mtu huyo ameigeuza nyumba ya Mungu kuwa pango la wazinzi, kanisa ni sehemu yake ya kujisitiri kwa muda, ili aonekane kwamba na yeye ni mkristo, au ili ajifariji moyoni kwamba bado anampenda na kumjali Mungu, na ili ajifariji kwamba jamii inamwona msafi..Lakini kiuhalisia hana mpango wa kuacha uasherati wake, wala hana mpango wa kumwacha yule mtu anayeishi naye ambaye wanayefanya naye uasherati.
11 Je! Nyumba hii, iitwayo kwa jina langu, imekuwa PANGO LA WANYANG’ANYI MACHONI PENU? Angalieni, mimi, naam, mimi, nimeliona jambo hili, asema Bwana”.
Mt 21:13
akawaambia, Imeandikwa, Nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala; bali ninyi mmeifanya kuwa pango la wanyang’anyi.
Umewahi kujiuliza kwanini, kwanini Bwana alitumia huo usemi…. “bali ninyi mmeifanya kuwa PANGO LA WANYANG’ANYİ”. Umewahi kutafakari pango la wanyang’anyi ni kitu gani?.
Siku zote wezi/vibaka wanakuwaga na maskani yao wanayojifichia, ambayo kwao ndio sehemu salama, na inakuwa ni sehemu ya maficho kwa muda, mara nyingi inaweza kuwa kwenye kipori fulani, au kwenye jengo fulani ambalo halijakamilika, au kwenye mapango ambayo ndani yana giza, Lengo ni kwamba wakishamwibia mtu, wanakimbilia huko, kujificha kwa muda, na baadaye kurudia tena kufanya uhalifu wao…hivyo inakuwa ni ngumu kuwakamata.. Na mara nyingi kwenye hayo maficho yao, ndio sehemu zao za kuchezea kamari, au kuvuta sigara, au kufanyia biashara zao haramu kama za kuuziana mihadarati.