KKKT (ELCT) Recycles Malasusa

KKKT (ELCT) Recycles Malasusa

nimeshangaa sana kujua kwamba Malasusa aligombea tena alafu wakampa. 2019 hivyo hivyo aligombea tena wakati alishakuwa mkuu wa kanisa. Huyu mtu theolojia anaijua lakini kazi ya uchungaji kama vile kwake sio ya wito.

Baba askofu Bagonza au pengine huyo wa Makete ingawa simjui ingekuwa safi sana kwa kanisa na kwa nchi kwa ujumla.
 
Unampa vipi hongera huyo muhuni?
Kwan huyu askofu kapigiwa kura na Akina nani, maana anashutumiwa Sana, pengine walio mpigia kura ndio wahuni wabobezi,
AU nao kkkT wanaiba kura kama NEC,

Malasusa Sio muhuni pekee, kkkT Kuna wahuni wengi sana yan
 
Tatizo ni kwamba watu wanawaza kila jambo kisiasasiasa kwa hiyo hata kama kitu sio watajaribu kuunganisha doti mpaka anaweza fikiri ni kweli. Kwa mpaka mtu anachagulia Mara ya pili katika mazingira kama haya ya vipindi viwili tofauti wajumbe walichambua in out ya wote na kuonelea Mwalasusa ashike kijiti tena hizi ni taasisi nyeti hazi hitaji mihemuko katika kufanya maamuzi
 
Nionavyo mimi hamkufurahishwa na Dr.Malasusa kabisa. Jaribuni kuvumilia tu kule hawakati rufaa kama NEC. Natambua inavyoumiza lakini mtafanya nini.
 
Kwan huyu askofu kapigiwa kura na Akina nani, maana anashutumiwa Sana, pengine walio mpigia kura ndio wahuni wabobezi,
AU nao kkkT wanaiba kura kama NEC,

Malasusa Sio muhuni pekee, kkkT Kuna wahuni wengi sana yan
Hakika
 
Hongera Baba Askofu Dr. Alex Gehaz Malasusa kwa kuchaguliwa mara ya pili (lkn kwa awamu ya 3 ya utumishi) kuwa Kiongozi kwy huduma ya Mkuu wa KKKT Tz.

Nadhani kuimarisha kazi ya huduma shambani mwa BWANA kwa tija na kuleta utangamano kwy kazi ya Uinjilishaji, DMP igawanywe kutengeneza Dayosisi mpya.

Napendekeza majina ya Dayosisi kama ifuatavyo:-

1. Dayosisi ya Dar es Salaam (au Dayosisi ya Metropolitan Dar es Salaam). Eneo lake liwe:-
  • Temeke
  • Ilala
  • Kigamboni
  • Kinondoni
  • Ubungo
2. Dayosisi ya Mashariki. Eneo lake liwe:-
  • Kisarawe
  • Rufiji
  • Kibiti
  • Mkuranga
  • Mafia
  • Kibaha
  • Chalinze
  • Bagamoyo
  • Zanzibar

NB
- Kiti cha Askofu wa Dayosisi ya Mashariki (Hqs) kiwe Kibaha.

- Dar es Salaam ni Metropolitan hivyo ibaki kama ilivyo na wilaya zake 5 ambazo ndizo ziwe Majimbo yake.

- Dayosisi mpya ya Mashariki ambayo kimsingi sehemu yake kubwa ni Misioni sasa ipandishwe hadhi kuwa Dayosisi kama Misioni za Kigoma, Tabora, Konde, Kusini Kati na Ziwa Tanganyika zilivyopandishwa hadhi kuwa Dayosisi.

- Kukiwapo haja ya chanzo imara cha uchumi kwa Dayosisi mpya ya Mashariki basi ipewe Temeke alafu Dayosisi ya Metropolitan Dar ichukuwe Zanzibar.

- Kama Dayosisi ya Metropolitan Dar ikibaki na wilaya zake zote 5 basi katika hatua ya uchanga wa Dayosisi mpya ya Mashariki napendekeza ilelewe na Dayosisi ya Metropolitan Dar kama ambavyo Dayosisi ya Kaskazini ililea Dayosisi ya Konde na sasa Dayosisi ya Ziwa Tanganyika lakini ikiendelea kulea pia baadhi ya Misioni za Malawi, Zambia, DR Congo, Msumbiji na Kenya.

Binafsi sikutegemea kama Baba Askofu Dr. Malasusa angegombea tena. Kuondolewa kwenye orodha ya wagombea jina la Askofu Bagonza halijanistua kwa sababu kwa misimamo yake na historia yake nilitegemea lolote lingemfika kama lilivyomfika.

Nimepata shida na Baba Askofu Dr. George Mark Fihavango wa Dayosisi ya Kusini-Makete kwa kuanguka kwenye uchaguzi huo.

Kiongozi huyu Baba Askofu Dr. Fihavango ninaweza kum-mithilisha na Kardinali Mteule Protase Rugambwa wa Kanisa Katoliki Tz kwa hekima, busara, falsafa, uwezo wa kusimamia haki bila kuyumbishwa, kujikana na maslahi binafsi ya ki-utu na kitaasisi, usafi wa nia na dhamiri, umahiri katika Injili, mwanamajumui mwenye kipawa cha kutangua mazonge kwenye huduma ya wito wake.

Baba Askofu Dr. Fihavango yuko vizuri Kiroho na kiuongozi wa kitaasisi. Ameumbiwa uwezo wa kufasiri jumbe za Ki-mamajusi zilizozonga Kanisa.

Nimesoma kitabu chake pale duka la Soma Biblia Mikocheni na pia safu yake kwy gazeti la Upendo la DMP.

Kwenye kitabu chake chenye kichwa "Uongozi Wetu na Dai la Uadilifu Katika Karne ya 21" ameandika akiakisi uongozi wa Kikanisa akitaja sifa kuu 4 za Kiongozi mzuri kuwa ni:-

1. Aliye tayari kuishi bila kuwa Kiongozi.

2. Aliye tayari kukabidhi uongozi inapompasa kufanya hivyo.

3. Anayejuwa na kuzingatia kuwa dhamana ya uongozi ni mkopo aliopewa na anaowaongoza ili aje awarejeshee na faida/riba (akimaanisha matokeo ya kazi).

4. Anayejuwa kusema anapotakiwa kusema na kunyamaza anapotakiwa kunyamaza.

Kile Kitabu chake chafaa kusomwa na viongozi wote wa Kiroho na Kisekula, tena wakikabidhiwe pamoja na Katiba na hati ya kiapo; wanapokula viapo.

Nisichokijuwa:
Dayosisi ya Mashariki na Pwani ilimpigia kura ya imani Askofu Malasusa inayompa kuwa Askofu hadi astaafu badala ya muda wa Kikatiba wa awamu 2 tu.

Askofu Malasusa alizaliwa Aprili 18, 1961, hivi sasa ana miaka 62, atastaafu Uaskofu wa DMP 2026 atapokuwa amefikisha umri wa Kikatiba wa Utumishi (kwake pekee kufuatia kupigiwa kura ya imani naye) wa miaka 65.

Kwa kuwa Mkuu wa Kanisa KKKT lazima awe Askofu aliyeko kazini kwenye Dayosisi yake na anayo haki ya kuwa Mkuu wa Kanisa kwa awamu 2 kwa kura, na kwa kuwa muda wake wa Uaskofu wa DMP unakoma 2026 lakini ngwe yake hii ya kwanza ya miaka 4 ya Ukuu wa Kanisa Tz unakoma 2027 maana yake ni kuwa DMP italazimika kumuongezea muda kwenye kiti cha Uaskofu ili asipoteze sifa ya kuwa Mkuu wa Kanisa Tz ambao kwa awamu 2 ya miaka 8 inatakiwa akabidhi kiti cha Ukuu wa Kanisa Tz mwaka 2031 na hivyo basi ataendelea kuwa Askofu wa DMP hadi 2031 atapokuwa na umri wa miaka 70.

Mhe. Baba Askofu Dr. Malasusa ni Banker kitaaluma anajuwa hesabu.
Tunaomba uzi wa mabadiriko mapya ya katiba mama ya KKKT.
 
Nionavyo mimi hamkufurahishwa na Dr.Malasusa kabisa. Jaribuni kuvumilia tu kule hawakati rufaa kama NEC. Natambua inavyoumiza lakini mtafanya nini.
Aliyeumia ni Benson Bagonza wa Karagwe, Stephen Munga wa Kaskazini Mashariki na Ambele Mwaipopo wa Ziwa Tanganyika.

Bagonza anaishi kuipinga serikali na chama tawala, anapinga Kanisa lake KKKT Tz na huenda anajipinga mwenyewe kwenye Dayosisi yake aliyojipa kuwa Askofu wa kudumu; maana Roho wa kupingapinga anamtumikisha ndani yake. Kuna rekodi yoyote ya Bagonza kuisifia serikali?

Munga roho wa kupingapinga alimsahaulisha asijipe Uaskofu wa kudumu na sasa yuko kwenye majuto ya kustaafu wakati asali ndiyo iko tayari. Munga tangu akiwa Mkwawa Sec akilala double-deck-bed 1 na Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe. Capt. Makongoro Nyerere ambaye naye pia kama rafiki yake Munga ana Roho wa kupingapinga ambapo aliwahi kumpinga rais Nyerere (babake) na 2000 alibwaga manyanga CCM na kukimbilia NCCR-Mageuzi. Askofu Munga aliimarisha enzi yake na kutamani angeondoa herufi "a" kwenye jina lake Munga aweke herufi "u" lisomeke Mungu (Stephen Mungu). Halmashauri Kuu ya DKM ilimvua hadhi ya Uaskofu (baada ya mgomo) kwa hatia kadhaa zikiwemo:-

1. Kufuja milki/mali wakfu zilizo katika mfumo wa fedha ambazo zinatoka vyanzo vikuu vya sadaka na fadhila.

2. Siasa na uanaharakati.

3. Madeni ya SEKOMU (Sebastian Kolowa Memorial University) cha Dayosisi ya Kaskazini Mashariki yanakiweka chuo katika hali ya kuparara.

Mwaipopo bendera fuata upepo unaoitwa "BagonzaMunga Wind" lakini bila kutengeneza jina kwanza kwenye tasnia za siasa na uanaharakati, mtaji unamkatikia mwanzo wa msimu wa mavuno. Hawezi kupapura wanasiasa na system ambao wana ngozi ngumu.

KKKT Tz kum-recycle Malasusa kama mkuu wake ni wazi kuwa enzi za huo utatu-usio-mtakatifu umekoma kama ilivyokoma enzi ya Askofu (Mst) Dr. Peter L. Mwamasika wa Dodoma (the firebrand wide-mouthed Bishop).

Malasusa ni mtoto wa mjini kingi-yake-hailiwagi kwenye mchezo wa chess.

Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app
 
nimeshangaa sana kujua kwamba Malasusa aligombea tena alafu wakampa. 2019 hivyo hivyo aligombea tena wakati alishakuwa mkuu wa kanisa. Huyu mtu theolojia anaijua lakini kazi ya uchungaji kama vile kwake sio ya wito.

Baba askofu Bagonza au pengine huyo wa Makete ingawa simjui ingekuwa safi sana kwa kanisa na kwa nchi kwa ujumla.
Tatizo Kaisari Nero hayuko tayari kufanya kazi na Mitume Paulo na Petro. (Uwili-Mtakatifu lakini sumu kwa Nero)

Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app
 
Maaskofu wa KKKT hamuendi mbinguni kwa kuweka KKKT kwenye milki ya CCM
KKKT inakuwaga kwenye chama cha siasa kutegemea Mkuu aliyeko madarakani.

Mfano, wakati Shoo yuko madarakani KKKT ilikuwa kwenye milki ya CHADEMA.

Case study:
Shoo alimshambulia RC Makonda hadharani kwenye ibada bila kujali itifaki kwa kuwa tu RC alikuwa kinyume na Mbowe wa CHADEMA ilhali RC ni CCM na Msukuma kama mteuzi wake.

Shoo huyo huyo juzi hajamshambulia Mwigulu aliyesababisha Makanisa kusuasua kwenye sadaka kwa kuweka tozo nyingi zinazopunguza vipato vya waumini na kuwaambia wasiotaka wahamie Burundi ambayo hii maana yake ni kwamba wafuasi wa nyumba wakfu za ibada wapungue idadi Tz wakaongezeke idadi kwenye nyumba wakfu za ibada za Burundi.

Nilijuwa juzi hii angemtoa nyongo Mwigulu kama alivyomkamua kamasi RC Makonda. Labda kwa kuwa Mwigulu hakumgusa Mbowe Mchaga.

Malasusa yeye awapo madarakani KKKT inakuwaga kwenye milki ya CCM.

KKKT hainaga permanent position kama Katoliki ilivyo neutral (Katoliki inaangalia tu... serikali, haiangalii chama, kwa sababu hata huko upinzani pia kuna wafuasi wa Katoliki wengi tu.

Katoliki ingeangalia chama badala ya serikali Dr. Slaa wa CHADEMA angeshinda urais 2010 kwa sababu Kikwete alikuwa Muislamu siyo Mkatoliki).

Katoliki walikuwa tayari Muislam Kikwete awe rais badala ya Dr. Slaa Padre mwenzao.

Wakati Nyerere anamkampenia Mkapa Askofu Munga alimuuliza Nyerere eti kwanini zamu hiyo isingekuwa ya Walutheri kutoa rais? Jibu alilopewa na Nyerere nali-reserve (si unajuwa majibu ya Nyerere kwa swali lililopishana na matamanio yake).

KKKT wanahitaji kupata darasa la Katoliki.

Something is wrong somehow somewhere in ELCT!

Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom