Kizunguzungu, NRA kushiriki uchaguzi Zanzibar, yampinga mgombea wake wa urais

Daniel Mbega

JF-Expert Member
Mar 20, 2013
338
180
NRA.jpg

CHAMA cha National Alliance and Reconstruction (NRA) kimesema kitashiriki uchaguzi wa marudio visiwani Zanzibar uliopangwa kufanyika Machi 20, 2016 na kukanusha tamko lililotolewa na mgombea wao wa urais Zanzibar kwamba chama hicho kimejitoa.

Katibu Mkuu wa NRA, Hassan Almasi Kisabya, amewaambia wanahabari jijini Dar es Salaam leo kwamba, tamko lililotolewa na mgombea huyo Seif Ali Iddi Februari 14, 2016 ni la kupuuzwa kwa sababu siyo tamkoa la chama.
ZAIDI...
 
Mgombea mwenyewe kajitoa basi wachague mtu mwengine kama sharia inawaruhusu wasimlazimishe mtu ambaye hataki.
 
CCM ni watu wa ajabu sana hawajawahi kutokea dunia hii! Wanaposema makamishna wa tume ZEC kwamba kauli ya Jecha ni yake pekee hajaishirikisha tume wanakataa. Lakini kinaposema chama uchwara chenye njaa kama kauli ya mgombea wao ni yake pekee hajakishirikisha chama, wanakubali.

Mwaka 2000 CUF waliposema uchaguzi urejewe nchi nzima kwa vile haukuwa huru, wao (Mkapa on record) akasema haiwezekani kufutwa uchaguzibwa nchi nzima, utafanywa pale uchaguzi ulipoharibika tu. Lakini mwaka 2015 wao ndio wanasema uchaguzi ufutwe na urejewe nchi nzima! Ama kweli, "Sikio la kufa halisikii dawa"
 
Mgombea hataki,wewe unamlazimisha kama nani?
Jecha alisema wagombea watakuwa ni walewale na hakuna kufanya kampeni! Ndio maana ZEC wamegoma kuondoa jina la maalim kwenye karatasi za kura.
 
Mgombea mwenzao kapewa fungu na wale machotala akaambiwa ajitoe ndiyo tabu ya wagombea njaa.
 
Back
Top Bottom