Kizungumkuti Dowans

Jana kwenye pita pita yangu nilikutana na Mjumbe mmoja wa Bodi ya Tanesco. Katika maongezi nae nilimuulizia kuhusu suala la Dowans. Kwenye maelezo yake ni kuwa malipo ya Dowans ni halali kabisa, kwani wanacho kidai ni gharama za umeme ambao wao walizalisha na hawakuwahi kulipwa na Tanesco mpaka mkataba pale ulipo vunjwa.
Kwa maana hiyo basi, wanadai hela yao halali kabisa ambayo umeme ulizalishwa na mie na wewe tuliutumia. Sasa hapo malipo ambayo sio halali ni yepi ? au tuna nia ya kudhulumu haki za watu ?.

Na kuhusu hukumu ya mahakama ya ICC wao vitu walivyo uliza ni vichache tu, kama mitambo ipo wapi ? ilizalisha umeme au haikuzalisha ? huko nyuma walikuwa wanawalipa au hawakuwalipa? Mkataba ulivunjwa kabla ya muda ?. Majibu ya maswali yote hayo ni ndio, ndipo mahakama ikatoa huku ya Dowans kulipwa haki yao kwa kile walichotuzalishia na kukitumia.

Ulihalalisha wewe na nani? Acha kutudanganya huyo uliyeongea naye naye akili yake haina akili.
 
Wezi wetu ni waelewa na wanajua kusoma alama za nyakati na ndio maana wametupunguzia pesa ambazo walikuwa wamepanga kutuibia kutoka Billion 185 hadi Billioni 94 baada ya watanzania kuamka kutoka kwenye usingizi wa amani, utulivu na mshikamano na kuanza kupiga mayowe ya mwizi, mwiziiii.... Tukichachamaa zaidi na kuendelea kuwazomea, kuna uwezekano mkubwa bwana Ngeleja akatutangazia kwamba wezi wetu wametusamehe. Jamani zidi kupiga mayowe

It is true, suala liliopo sio ku-bargain kiasi cha kuwalipa hawa majambazi wakubwa ( JK + Company) bali ni kupinga kwa nguvu zote kuwalipa. Walianza na Tsh. 185 billion, baada ya kelele nyingi Ngeleja akasema ni Tsh. 94 billion na akisisitiza kwamba ni lazima Dowans walipwe. Baada ya wananchi kusimama kidete sasa fisadi mmoja (Nimrodi Mkono) akichangia hoja kwenye semina ya wabunge wa CCM alisema ataisaidia serikali kupunguza hilo deni au lifutwe kabisa! Jamani huku sio ndio kutuchezea kweli? Inakuwaje watu wachache JK, RA, Nimrodi Mkono and others watuchezee watanzania millioni 44? Hivi hatuwezi kuwashughulikia?
 
KWA UTHIBITISHO HUU WA WIZI MGONGONI MWA DOWANS, SERIKALI IJIUZULU MARA MOJA

Kwa mtaji wa taarifa hii KUTHIBITISHA VIONGOZI WETU SERIKALINI kutulazimisha visivyohalali kulipa Dowans na hatimaye hii siri nzito kutufikia walipakodi masikioni basi kwa pamoja Watanzania hatuna lingine tena

Kwa pamoja tunasema Kikwete, Rostam Azizi, Nimrod Mkono, Nazir Karamagi, Balozi Maajar, Ngeleja, Chenge, Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madalali wenu wengine wengi zaidi, tunasema MJIUZULU MARAMOJA!!!!

Na nyinyi vyama vya upinzani, asai za kiraia na wanaharakati mbali mbali mkiendelea kunyamazia zaidi HICHI KITHIBITISHO CHA WIZI WA KODI ZETU iliokua iliokua ikilazimishwa na Kikwete na CCM na hatimaye Mungu kutuletea uthibitisho huu, basi watu tutawageukeni na nyinyi na kuonana wabaya hapa!

Kwa taarifa hii Serikali ya CCM ijiuzulu sasa hivi na wala si kusubiri zaidi. Hii na hatarii!!!
 
MBINU MPYA CCM KUJILIPA MARA 3 SHEA WANAYOISUBIRIA DOWANS KWA KUWAUZIA WANANCHI JOTO JINGI NA GIZA NENE KWA MAVUNO MANONO ZAIDI KARIAKOO:

Enyi wana CCM, Dowans hatuwalipi hata senti moja kutoka kwenye kodi zetu mbona hatuelewani??

Ni kero kubwa ilioje kwamba wananchi tuwashike viongozi wabadhirifu serikalini na tuhuma nzito za kutupora kwa miaka mingi kodi zetu kwa kutumiamakampuni ya kitapeli yasiojulikana wamiliki wake halafu hata bila ya jibu hilo sasa muanze kugeuza Kiswahili cha kujadilkiana na WEZI ETI KUPUNGUZIANA KIWANGO CHA FEDHA ZA WIZI WA KUWALIPA; hizi ndizo busara za wapi??

Kama hilo halitoshi, CCM hii hii bado inatuona mataahira wale wale wa miaka ya jana kwa kutuaminisha ya kwamba MTUHUMIWA WETU, NIMROD MKONO, MBUNGE MWAKILISHI WA JIMBO LA UFISADI, MFILISI WA BoT BILA UZALENDO NA MTAALAM WA KUTUFUNGISHA MIKATABA ya kuletea taifa shimanzi kila mwaka eti ndio sasa aende mahakamani kutuwakilisha katika mpango wa wizi aliouunda mwenyewe ili kwa janja za nyani tukapunguziwe kitu.

Nasema hatudanganyiki, kama AG Werema na sisi Nguvu ya Umma Jalada la Dowans tumelifunga badala yake tukutane bungeni Dodoma kwa hili ili chombo chenye mamlaka kisheria kusimamia uthibiti wa mapato na matumizi ya serikali itupe mwelekeo zaidi kwa kuzingatia kumbukumbu zilizomo ndani ya Hansard ya bunge baada ya Tume ya Mwakyembe kuwashilisha ripoti yake.

Acheni kujibaraguja hapa, kilichobakia ni sisi wananchi kutoa adhabu ya kihistoria ili ije iwe fundisho tosha kwa vyama vya kisiasa vinavyoongozwa na WALAGHAI NA MAFISADI WAKUU kama ilivyo kwa CCM. Wabunge wa CCM, kuna jambo bado wengi wenu hamjalielewa hapa; sisi wananchi hatuko kwenye mzaha na nyinyi.

Tunajua fika ni kazi gani tuliwatuma bungeni na kwamba mkienda vipi na basi iwe vipi. Katika hii kashfa na pia suala la KATIBA MPYA mchakato kuanzia bungeni sisi hesabu zetu hapo ni kwamba AMA UKO NA SISI AU UKO PAMOJA NA KAMBI YA MAFISADI ITAKAYOKUPIGIA KURA TENA HUKO MBELE YA SAFARI. Tuelewane vizuri kabisa hapo.

Naona kwenye mtego huu hata huyu ndugu tuliewahi kumuamini, Mizengo Pinda (ambaye hadi sasa kajigeuza Mtoto wa Mkulima wa Mjini) naye kajiingiza kichwa kichwa mle lakini bahati yake alishatangaza kwenda kupumzika siasa baada ya hapa, je nyinyi??

Na kwa bahati mbaya sana sana, Nguvu ya Umma uchunguzi wetu jijini umebaini kwamba kwanza mpaka sasa hivi CCM imeshajilipa zaidi ya mara 3 ya udanganyifu kwa Dowans kwa kule
 
Wewe ndiyo unazidi kututia hasira tu. Bora ungekaa kimya. Huyo bodi member uliyekutana naye mshauri aache kusinzia kwenye vikao

Duh ! Haha. Ah ha kweli. Haswa. Huyo mjumbe. Alikua kalala. Ama anandoto. Za mchana. Hata huyu. Alie post. Siajabu. Ni wale wale. Ambao wako kwenye. Mgao damn it
 
Tanesco ni shirika la nani kwani ? wewe hata muundo huujui kumbe tukusaidiaje sijui

I guess you have a cripple mind badala ya kujibu swali unauliza swali btw this is what we call erinaceous you are just partaining to the hedgehog
 
Jana kwenye pita pita yangu nilikutana na Mjumbe mmoja wa Bodi ya Tanesco. Katika maongezi nae nilimuulizia kuhusu suala la Dowans. Kwenye maelezo yake ni kuwa malipo ya Dowans ni halali kabisa, kwani wanacho kidai ni gharama za umeme ambao wao walizalisha na hawakuwahi kulipwa na Tanesco mpaka mkataba pale ulipo vunjwa.
Kwa maana hiyo basi, wanadai hela yao halali kabisa ambayo umeme ulizalishwa na mie na wewe tuliutumia. Sasa hapo malipo ambayo sio halali ni yepi ? au tuna nia ya kudhulumu haki za watu ?.

Na kuhusu hukumu ya mahakama ya ICC wao vitu walivyo uliza ni vichache tu, kama mitambo ipo wapi ? ilizalisha umeme au haikuzalisha ? huko nyuma walikuwa wanawalipa au hawakuwalipa? Mkataba ulivunjwa kabla ya muda ?. Majibu ya maswali yote hayo ni ndio, ndipo mahakama ikatoa huku ya Dowans kulipwa haki yao kwa kile walichotuzalishia na kukitumia.

Huyo aliyekwambia hajasoma hukumu ya ICC! nashauri na wewe uisome ndipo utajua kwamba issue ilikuwa ni uvunjaji wa mkataba
 
halipwi mtu!! gia zote za kutokea zitakwama itabidi mshuke nje na kusukuma! tatizo ni mlima haukweleki!

Kwa kweli hilo sasa liko wazi. Kelele za watu wengi wa ngazi mbalimbali zimewezesha hili. Lakini kuna kelele na jitihada za watu wachache sana ambazo zimesukuma wengine kushiriki kupiga kelele. Naomba Mkuu Mwanakijiji nikupe tuzo hiyo kwa jitihada zako za kufuatilia kwa makini na kuanzisha mijadala kuhusu Richmond na Dowans hapa JF.

Pengine hapa JF tuanzishe tuzo kwa watu wanaopambana na ufisadi, nitakuwa radhi kuchangia. Ni vigumu kupima kiwango cha uzalendo ambacho baadhi ya members wa JF wanaonesha kwa vitendo na impact yake kwe jamii yetu.

Lakini hii isiwe na maana kwamba kila mtu sasa akurupuke kuonesha kwamba yeye ni mpambanaji!!
 
Jana kwenye pita pita yangu nilikutana na Mjumbe mmoja wa Bodi ya Tanesco. Katika maongezi nae nilimuulizia kuhusu suala la Dowans. Kwenye maelezo yake ni kuwa malipo ya Dowans ni halali kabisa, kwani wanacho kidai ni gharama za umeme ambao wao walizalisha na hawakuwahi kulipwa na Tanesco mpaka mkataba pale ulipo vunjwa.
Kwa maana hiyo basi, wanadai hela yao halali kabisa ambayo umeme ulizalishwa na mie na wewe tuliutumia. Sasa hapo malipo ambayo sio halali ni yepi ? au tuna nia ya kudhulumu haki za watu ?.

Na kuhusu hukumu ya mahakama ya ICC wao vitu walivyo uliza ni vichache tu, kama mitambo ipo wapi ? ilizalisha umeme au haikuzalisha ? huko nyuma walikuwa wanawalipa au hawakuwalipa? Mkataba ulivunjwa kabla ya muda ?. Majibu ya maswali yote hayo ni ndio, ndipo mahakama ikatoa huku ya Dowans kulipwa haki yao kwa kile walichotuzalishia na kukitumia.

Pambafu....
 
Mwanakijiji wewe unasema .....halipwi mtu!! gia zote za kutokea zitakwama itabidi mshuke nje na kusukuma! tatizo ni mlima haukweleki!

Haki ya Kweli NAKWAMBIA lazima TUWALIPE Dowanz, piga ua Galagaza TUNAWALIPA . JK na wambunge wake Juzi wameshabariki Malipo ni nani ATAKAYEZUIA.

Tuache Kupiga kelele humu ndani na TUKUBALI kuwa TUNAWALIPA DOWANS. FULL STOP
 
MAOMBI ya madai ya usajili wa Tuzo ya Kampuni ya Dowans yamewasilishwa Mahakama Kuu kanda ya Dar es Salaam na kusajiliwa kwa kupewa namba ya usajili nane ya mwaka huu.

Dowans ilishinda kesi ya madai dhidi ya TANESCO katika Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Kibiashara (ICC) na kuamuliwa TANESCO kumlipa Dowans Sh Bilioni 94.

Naibu msajili mwandamizi wa mahakama hiyo, Salvatory Mwongole, alisema jana kuwa maombi hayo yameifikia mahakama hiyo januari 25 mwaka huu na yamewasilishwa na wakili wa kampuni hiyo hapa nchini kutoka kampuni ya uwakili ya Kennedy Fungamtama.

Mwongole alisema maombi hayo yamekwisha pangiwa jaji lakini kulingana na unyeti wa suala hilo jina la jaji linahifadhiwa kwasababu ndio kwanza ameteuliwa kushughulikia maombi ya usajili huo na jalada halijamfikia.

Alisema maombi hayo ya usajili yameombwa na kampuni ya Dowans Holdings S.A na Dowans Tanzania dhidi ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).

Source: Michuzi.

Huyu Fungamtama alishauri tusipolipa nchi haitapata misaada!!
 
Kennedy,kumbe pesa zako na vimbwembwe vyako vya kinyani zinapatikana kwa stahili za namna hii,SHAME ON YOU.The other day nakusoma unashauri hizo pesa lazima zilipwe kumbe ulikuwa unaweka mazingira sawa,uniuwe kabla sijakupata.
 
Back
Top Bottom