Hodi wana jukwaa,
Kama mjuavyo ulimwengu wa kisasa unawapelekesha sana vijana wetu wa kidot com. Juma hili lililopita niliamua kwenda sehemu ambayo nilidhani itakuwa tulivu kwa ajili ya kurefresh. Nikaenda sehemu, kwa kweli kwa mtazamo wangu niliona walau inaridhisha, nikakaa sehemu nikaaagiza vinywaji vyangu na kutoa oda ya nyama choma kama kawaida yangu. Sehemu ile ina kivuli cha asili cha miti, lakini imefanyiwa maboresho ili kuvutia wateja.
Sehemu niliyokaa, kwa nyuma yangu upande wa pili walikaa akina dada watatu wakipata vinywaji na walionekana wamechangamka. Kilichonifaya nije kupost hapa ni maongezi yao ambayo yalinishtua kidogo. Topic ilikuwa ni wanaume, na mmoja wao akasikika akisema, '... kwani ndoa kitu gani....... mimi sijaolewa lakini napata huduma zote ambazo hao walio kwenye ndoa wanapata." Akaendelea mbele zaidi na kusema kuwa anatoka na mume wa mtu. Ikaonekana kuwa huyu dada alishaishi kinyumba na mwanaume wakazaa mtoto mmoja then wakaachana lakini hawakuwa na ndoa. Huyu mdada jinsi alivyokuwa anamchambua huyu bwana wake waliyeachana naye, nikavuta picha kama ndo wewe unasemwa vile alafu ukajua unasemwa vile, kama huna roho ngumu utachukua bastola aisee. Kamtukana matusi yote na kusema kuwa hajui mambo.
Upande wa pili, huyu mume wa mtu aliye naye akamwagiwa sifa kem kem, anajua kutunza, na kunako Mombasa raha anajua kupeleka mashambulizi haswa. Mwanadada anakiri kwa wenzake kuwa liwalo na liwe hawezi kuachana na yule mume wa mtu. In short she feels like in a paradise. Mbaya zaidi wenzake nao wanasupport hoja zake. jamani dunia imefika mwisho, akina dada walio kwenye ndoa abiria chunga mzigo wako, shauri zenu.