Zemanda
JF-Expert Member
- Jan 10, 2021
- 10,999
- 23,542
Kasumba ya mabinti wengi wa kileo ni kutaka kuishi maisha ya kujiachia ila at the same time kuwa na ule ulinzi wa kijamii anaopewa mwanamke.
Mfano, leo mabinti wengi wanataka wasiolewe ila wazae na wanaume wenye ndoa zao halafu wapate matunzo sawa na mke halali wa ndoa.
Na hata ikatokea mume huyu amefariki usishangae kuona wanatafuta namna ya kupata sehemu ya urithi kwa kutumia mtoto huyu wa nje ya ndoa.
Mabinti/ wanawake wa kisasa hawataki kuwa na mwanaume wa kuwapangia ratiba ya kwenda wapi au kuwafuatilia yupo na nani ila still akiona mwenzake mume wake anampigia kujua yupo wapi,au amekula nini au kupelekwa hospital au anakuja mchukua na kwenda nae nyumbani, au wakitoka wameongozana na mume wake ndipo anaelewa kuwa uhuru unagharama kubwa kuliko kifungo cha ndoa.
Imagine kuwa nje usiku saa sita au zaidi halafu hana mwanaume, kinachotokea ni ile hofu ya kiusalama anabidi amwambie bodaboda amsindikize hadi nyumbani halafu asubirie hadi mpangaji mwenzie amfungulie geti ndipo boda boda aondoke.
Vipi pale akiwa anashida ya kifedha nani anakuwa karibu kutoa sapoti. Kuna ile hali ya kuwa mhitaji halafu anatokea mtu unayeishi nae anakupatia kiasi kile unachotaka au zaidi bila kutumia effort kutafuta na huyu mtu hakudai hiyo anakuwa kama amejipatia mwenyewe. Kwa mwanamke anayetaka uhuru hii pesa ataipata na zaidi ila atalipia kwa kupigwa mashine na kuweka rehani mwili wake.
Poleni sana Wanawake mnaoamini uhuru hauna gharama na ndio sehemu ya mwanamke kuwapo.
Uhuru una gharama kushinda kifungo cha mahusiano au ndoa. Kama unabisha subiri umri uzidi kusogea na hauna mwanaume wako wa ndoa.
Sent from my JKM-LX1 using JamiiForums mobile app