Kizungumkuti cha akina dada wa siku hizi na maisha ya ndoa

OIL CHAFU

JF-Expert Member
Jun 8, 2012
982
1,000
Hodi wana jukwaa,

Kama mjuavyo ulimwengu wa kisasa unawapelekesha sana vijana wetu wa kidot com. Juma hili lililopita niliamua kwenda sehemu ambayo nilidhani itakuwa tulivu kwa ajili ya kurefresh. Nikaenda sehemu, kwa kweli kwa mtazamo wangu niliona walau inaridhisha, nikakaa sehemu nikaaagiza vinywaji vyangu na kutoa oda ya nyama choma kama kawaida yangu. Sehemu ile ina kivuli cha asili cha miti, lakini imefanyiwa maboresho ili kuvutia wateja.

Sehemu niliyokaa, kwa nyuma yangu upande wa pili walikaa akina dada watatu wakipata vinywaji na walionekana wamechangamka. Kilichonifaya nije kupost hapa ni maongezi yao ambayo yalinishtua kidogo. Topic ilikuwa ni wanaume, na mmoja wao akasikika akisema, '... kwani ndoa kitu gani....... mimi sijaolewa lakini napata huduma zote ambazo hao walio kwenye ndoa wanapata." Akaendelea mbele zaidi na kusema kuwa anatoka na mume wa mtu. Ikaonekana kuwa huyu dada alishaishi kinyumba na mwanaume wakazaa mtoto mmoja then wakaachana lakini hawakuwa na ndoa. Huyu mdada jinsi alivyokuwa anamchambua huyu bwana wake waliyeachana naye, nikavuta picha kama ndo wewe unasemwa vile alafu ukajua unasemwa vile, kama huna roho ngumu utachukua bastola aisee. Kamtukana matusi yote na kusema kuwa hajui mambo.

Upande wa pili, huyu mume wa mtu aliye naye akamwagiwa sifa kem kem, anajua kutunza, na kunako Mombasa raha anajua kupeleka mashambulizi haswa. Mwanadada anakiri kwa wenzake kuwa liwalo na liwe hawezi kuachana na yule mume wa mtu. In short she feels like in a paradise. Mbaya zaidi wenzake nao wanasupport hoja zake. jamani dunia imefika mwisho, akina dada walio kwenye ndoa abiria chunga mzigo wako, shauri zenu.
 
Cyan6

JF-Expert Member
Aug 8, 2013
4,534
0
Kelele za mlango hazimnyimi mwenye nyumba usingizi! Maji ya moto hayachomi nyumba moto!
 
mfudu

Member
Dec 13, 2012
36
95

sawa bosi weka video
 
4 Digits

Member
Oct 4, 2011
47
95
Si story ya kushtua sana hapa mjini kwa sasa, asichojua huyo mdada hata huyo mume wa mtu pia ana nafasi kubwa ya maamuzi ya kumuacha kama akipata ufahamu na ku-analyze prons & cons za mahusiano yao, hasa kwa kuzingatia tamaa za wadada kama hao na starehe na company za kijinga, ambazo mara hata wao hugeukana. Asante kwa mafunzo yaliyomo kwenye hadithi hii, kwa wanandoa la muhimu msifikie mahali na kujiangalia ninyi tu! Kumbukeni pia athari kwa uzao wenu zitakazipatikana kw starehe zenu za muda mfupi na zisizo na tija!
 
Mkempia

JF-Expert Member
Mar 5, 2013
1,142
1,500
Nyie wanaume mnaotembea nje ya ndoa zenu mnahitaji pia kuwa waangalifu sana, nasema hivyo kwasababu kuna kijana ninamfahamu anatarajia kuoa mwezi huu. Huyu kijana amewapa mimba wasichana wawili kwa mpigo na wamepishana miezi tu kujifungua. Hapo kuna baamedi alihaidiwa kuolewa, kuna binti mwingine alihaidiwa nae kuolewa huo mkoa mmoja alipokwenda mapunzikoni. LAKINI MWISHO WA YOTE HAYA ILIKUJA KUGUNDULIKA KUWA HATA BABA YAKE MZAZI NA KIJANA HUYO ALIKUWA HIVYO HIVYO.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom