Kizazi kijacho kitarithi LAWAMA...! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kizazi kijacho kitarithi LAWAMA...!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by ZeMarcopolo, Feb 7, 2011.

 1. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #1
  Feb 7, 2011
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,589
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Kizazi cha leo kimerithi Uhuru toka kwa kizazi kilichotangulia ambacho kilirithi ukoloni toka kwa kizazi kilichowatangulia.
  Najiuliza, kizazi chetu kitaacha urithi gani kwa ajili ya kizazi kijacho?
  Tukumbushane tu, kuwa swala la kuacha urithi kwa ajili ya vizazi vijavyo si jukumu la serikali. Ni jukumu la kila anajitabua kama mtanzania.
  Kizazi chetu kimekuwa ni kizazi cha lawama kila kukicha. Majadiliano yetu ya kutoa lawama hayaambatani na majadiliano ya nini kifanyike ili kuweka mambo sawa. Tukiendelea hivi, kizazi kijacho kitarithi lawama tupu.

  Natoa wito kwa vijana wote wa kizazi hiki kuangalia zaidi ufumbuzi wa matatizo yetu badala ya kujikita zaidi kwenye kutafuta wa kuwalaumu.

  Tujenge utamaduni wa kufanya kazi kwa bidii, huu uwe urithi wa kizazi kijacho.
  Tujenge utamaduni wa kuchukia kila aina ya rushwa na ubadhilifu (siyo wa mabilioni tu), huu uwe urithi wa kizazi kijacho.
   
Loading...