Kiyabo: CCK itatoa Rais 2015

Kiyabo: CCK itatoa Rais 2015

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Posts
15,860
Reaction score
5,803
[h=2][/h]Alhamisi, Aprili 18, 2013 07:33 Na Joe Beda

*Kupanga safu imara ya uongozi kesho jijini Dar es Salaam

RICHARD Kiyabo (pichani), ni kada wa Chama Cha Kijamii (CCK) ambaye pia ni mmoja wa waasisi wa chama kilichoundwa na kuitikisa Tanzania kwa muda mfupi kabla ya kufutwa, Chama Cha Jamii (CCJ). Mwanasiasa huyo amefanya mahojiano na RAI, ambapo ameeleza kuwa CCK ina nafasi kubwa ya kukamata dola mwaka 2015.

Kiyabo, ambaye baada ya CCJ kufutwa alihamia Chama Cha Mapinduzi (CCM) kabla ya kuamua kuachana na siasa kwa muda, amesema anaamini kwamba Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania litakuwa na wabunge wa kutosha kutoka CCK.

“Hii si ndoto, ni kitu kilicho wazi na kinachowezekana kabisa kwani kwa sasa CCK ndicho chama pekee kinachoongozwa na mwenyekiti kijana, msomi, mwanadiplomasia mwenye sifa sawa kabisa na Baba wa Taifa (Mwalimu Julius Nyerere),” anasema Kiyabo.

Mwenyekiti wa muda wa CCK ni Constantine Akatanda, akiwa amechukua mikoba kutoka kwa Kiyabo aliyeibuka na CCJ mwanzoni mwa mwaka 2010 na kuitikisa medani ya siasa nchini huku akiaminika kuwa amewekwa pale na watu waliokuwa wakiutaka urais mwaka huo.

“Ukweli ni kwamba hatukuwekwa na mtu wala kundi lolote la watu. Tulijipanga vyema na bahati nzuri wananchi wakatuelewa na viongozi wa vyama vyote nchini wakaanza kutuogopa,” anasema, akiizungumzia CCJ, chama kilichozinduliwa kwa mbwembwe nyingi lakini kikakwama kupata usajili wa kudumu kabla ya kufutwa kwa tamko rasmi la Serikali.

Katika harakati hizo mwaka 2010, Kiyabo anaeleza kwamba alikumbwa na mkasa mkubwa baada ya kuvamiwa na watu watano wasiojulikana maeneo ya Kariakoo, kisha kupigwa na kupoteza fahamu.

Katika tukio hilo watu hao waliondoka na mkoba uliokuwa na nyaraka muhimu za chama.

Anaeleza kuwa matibabu yake yaligharamiwa kwa kiasi kikubwa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe.

Mwanasiasa huyo hakuishia hapo bali ameeleza kwamba baada ya afya yake kuimarika aliikuta CCJ ikiwa imefutwa; kisha akahamia CCM na baadaye akaamua kuachana na siasa; “lakini sasa ninarejea tena kwenye siasa. Si CCM, hapana, bali nitakwenda CCK.

“Hii ni kwa sababu chama hiki kina malengo na matazamio sawa na CCJ. Chama hiki kina uongozi thabiti chini ya Akatanda ambaye wakati tukianzisha CCJ alikuwa nami bega kwa bega; akajifunza; akapata uzoefu na kutokana na elimu yake ya diplomasia, nilipokuwa nje ya siasa alifanikiwa kukiongoza chama hadi kupata usajili wa kudumu.

“Aprili 19 (kesho),wajumbe kutoka mikoa yote Tanzania watakuwapo Dar es Salaam kwa ajili ya mkutano mkuu na ningependa kuwaomba sana wampe nafasi Akatanda awe kiongozi wa chama ili akiimarishe tayari kwa mapambano ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2014 na kisha Uchaguzi Mkuu 2015.”

Akimzungumzia Akatanda, Kiyabo alisema kwamba kijana huyo anajua maana halisi ya uongozi kwani si mbinafsi na iwapo chama kitaridhia agombee urais 2015, hakika ana ubavu wa kupambana na mgombea kutoka chama chochote nchini.

“Maana ya uongozi ni kuelekeza watu au kundi la watu kwenda kwenye matokeo bora zaidi. CCK ndiyo pekee chenye nafasi ya kuwapa Watanzania matumaini na faraja, vitu ambavyo kwa sasa vimepotea kabisa.

“Hebu tuwape nafasi vijana kama Akatanda waiongoze na kuikomboa nchi hii kwa fikra zao mpya. Ndani ya CCK tayari kijana huyu ameshafanya uongozi uliotukuka. Ukizungumza naye unaona kabisa maono yake kuhusu uchumi wa taifa letu. Huyu ni Mandela wetu na ana uwezo wa kuwa Amiri Jeshi Mkuu,” anasema.

Kiyabo aliyekuwa Katibu wa Uchumi na Fedha wa Tawi la CCM Mbagala anasema awali hawakuwa na lengo la kuanzisha chama cha kisiasa, bali asasi isiyo ya kiserikali (NGO), lakini baada ya kuwashirikisha wasomi kadhaa kuandaa rasimu ya katiba ya NGO hiyo, wanasheria walioipitia wakawaambia kuwa katiba hiyo ni zaidi ya NGO na kuwashauri waanzishe chama cha kisiasa.

“Hapo tukaanza kuzungumza na watu tunaofahamiana nao ndani na nje ya nchi, tukashauriana, tukachangishana na kuipeleka katiba yetu kwa Msajili wa Vyama vya Siasa, John Tendwa, na alipoisoma mwenyewe akakiri kuwa ile ndiyo katiba mbadala na bora kuliko nyingine karibu zote.

“Bahati mbaya au nzuri, kuna mwandishi wa habari aliipata katiba hiyo, akaitangaza siku mbili kabla ya uzinduzi wa chama chetu. Siku ya uzinduzi ikawa balaa! Chama kikajulikana kweli kweli. Tukatangaza kuwa katika kukitangaza chama mikoani, tungeanzia mkoa wa Mara nyumbani kwa Mwalimu Nyerere.

“Wafadhili wakajitokeza, tukapewa tiketi za ndege, tukaenda Butiama na kuzindua kazi zetu pale pale. Hakika ilikuwa tishio na kama tungeshiriki uchaguzi wa 2010, tungepata wabunge wengi sana na hata 2015 ninakwambia tutapata viti vingi.

“Sababu kubwa ni moja, CCK ndicho chama cha kukimbilia watu wasiopenda mizengwe, minyukano na walio tayari kuikomboa nchi yetu,” anasema.

Anamalizia kwa kuzungumzia ukombozi wa pili wa Tanzania, amesema rasilimali tulizo nazo ni lazima zitumike viwandani kwani bila viwanda hakuna maendeleo ya kiuchumi, muda umefika wa kujikomboa kutoka kwenye laana tuliyonayo.

Israel ndiyo nchi yenye teknolojia au watu waliobobea kwenye teknolojia duniani na ili tuendelee, tunapaswa kuwatumia watu hao (Waisrael) kwa kushirikiana nao tofauti na sasa ambapo hatuna uhusiano wa kibalozi
 
bora hata cck kuliko cdm wazee wa viingilia utadhani bend ya muziki
 
Tatizo BONGO sio Kama KENYA - JINA la MTU sio NJIA ya KUJIPATIA KURA kwenye CHAMA CHENU... labda utapata kura kwenye hilo JIMBO unalogombea...

Na Wabunge wengi wa CCM ni WACHAFU wakijiunga na CCK ambacho hakina connection na Wananchi watatupwa nje haraka; Na kama ni Wabunge wanaobadilisha badilisha VYAMA hii itakuwa MWISHO wao...
 
Hahahaa dah!

Hii CCK mi nilidhani ilishakufa kama ilivyokufa CCJ lakini kumbe bado ipo na bado ina ndoto za kutoa rais mwaka 2015.

Anaishi Tanzania ipi huyo Bw. Kiyabo?

Kwa vyovyote vile 2015 urais ni wa CCM tu. Na CCM hata wamuweke mgombea bomu namna gani watashinda tu hiyo nafasi.

Hata mgombea wao awe Mwigulu Nchemba, watashinda tu urais. Na huu si utabiri kwa sababu huwezi kutabiri jambo lililo dhahiri kama hili.

Ni ukweli tu ambao kwa wengine unaweza ukawa ni mchungu kuukubali.
 
Nyie msiwe kama chama tumaini letu, wanenda bungeninkuzungumzia stori za JF za UDINI!
 
taratibu basi jamani; uwanja mpana huu kila mtu anaweza kucheza.. vyama vingine vya upinzani havina sababu ya kuihofia CCK, chama kidogo na hakina watu wenye majina, hakina diwani wala Mbunge... waachwe wajijenge..

Mzee Mwanakijiji ushauri wako umelenga katika kukuza demokrasia, tatizo la vyama vyetu havitaki kabisa kuona vyama vyingine vinakua japo vinapigania demokrasia.
 
Alhamisi, Aprili 18, 2013 07:33 Na Joe Beda

*Kupanga safu imara ya uongozi kesho jijini Dar es Salaam

RICHARD Kiyabo (pichani), ni kada wa Chama Cha Kijamii (CCK) ambaye pia ni mmoja wa waasisi wa chama kilichoundwa na kuitikisa Tanzania kwa muda mfupi kabla ya kufutwa, Chama Cha Jamii (CCJ). Mwanasiasa huyo amefanya mahojiano na RAI, ambapo ameeleza kuwa CCK ina nafasi kubwa ya kukamata dola mwaka 2015.

Kiyabo, ambaye baada ya CCJ kufutwa alihamia Chama Cha Mapinduzi (CCM) kabla ya kuamua kuachana na siasa kwa muda, amesema anaamini kwamba Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania litakuwa na wabunge wa kutosha kutoka CCK.

“Hii si ndoto, ni kitu kilicho wazi na kinachowezekana kabisa kwani kwa sasa CCK ndicho chama pekee kinachoongozwa na mwenyekiti kijana, msomi, mwanadiplomasia mwenye sifa sawa kabisa na Baba wa Taifa (Mwalimu Julius Nyerere),” anasema Kiyabo.

Mwenyekiti wa muda wa CCK ni Constantine Akatanda, akiwa amechukua mikoba kutoka kwa Kiyabo aliyeibuka na CCJ mwanzoni mwa mwaka 2010 na kuitikisa medani ya siasa nchini huku akiaminika kuwa amewekwa pale na watu waliokuwa wakiutaka urais mwaka huo.

“Ukweli ni kwamba hatukuwekwa na mtu wala kundi lolote la watu. Tulijipanga vyema na bahati nzuri wananchi wakatuelewa na viongozi wa vyama vyote nchini wakaanza kutuogopa,” anasema, akiizungumzia CCJ, chama kilichozinduliwa kwa mbwembwe nyingi lakini kikakwama kupata usajili wa kudumu kabla ya kufutwa kwa tamko rasmi la Serikali.

Katika harakati hizo mwaka 2010, Kiyabo anaeleza kwamba alikumbwa na mkasa mkubwa baada ya kuvamiwa na watu watano wasiojulikana maeneo ya Kariakoo, kisha kupigwa na kupoteza fahamu.

Katika tukio hilo watu hao waliondoka na mkoba uliokuwa na nyaraka muhimu za chama.

Anaeleza kuwa matibabu yake yaligharamiwa kwa kiasi kikubwa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe.

Mwanasiasa huyo hakuishia hapo bali ameeleza kwamba baada ya afya yake kuimarika aliikuta CCJ ikiwa imefutwa; kisha akahamia CCM na baadaye akaamua kuachana na siasa; “lakini sasa ninarejea tena kwenye siasa. Si CCM, hapana, bali nitakwenda CCK.

“Hii ni kwa sababu chama hiki kina malengo na matazamio sawa na CCJ. Chama hiki kina uongozi thabiti chini ya Akatanda ambaye wakati tukianzisha CCJ alikuwa nami bega kwa bega; akajifunza; akapata uzoefu na kutokana na elimu yake ya diplomasia, nilipokuwa nje ya siasa alifanikiwa kukiongoza chama hadi kupata usajili wa kudumu.

“Aprili 19 (kesho),wajumbe kutoka mikoa yote Tanzania watakuwapo Dar es Salaam kwa ajili ya mkutano mkuu na ningependa kuwaomba sana wampe nafasi Akatanda awe kiongozi wa chama ili akiimarishe tayari kwa mapambano ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2014 na kisha Uchaguzi Mkuu 2015.”

Akimzungumzia Akatanda, Kiyabo alisema kwamba kijana huyo anajua maana halisi ya uongozi kwani si mbinafsi na iwapo chama kitaridhia agombee urais 2015, hakika ana ubavu wa kupambana na mgombea kutoka chama chochote nchini.

“Maana ya uongozi ni kuelekeza watu au kundi la watu kwenda kwenye matokeo bora zaidi. CCK ndiyo pekee chenye nafasi ya kuwapa Watanzania matumaini na faraja, vitu ambavyo kwa sasa vimepotea kabisa.

“Hebu tuwape nafasi vijana kama Akatanda waiongoze na kuikomboa nchi hii kwa fikra zao mpya. Ndani ya CCK tayari kijana huyu ameshafanya uongozi uliotukuka. Ukizungumza naye unaona kabisa maono yake kuhusu uchumi wa taifa letu. Huyu ni Mandela wetu na ana uwezo wa kuwa Amiri Jeshi Mkuu,” anasema.

Kiyabo aliyekuwa Katibu wa Uchumi na Fedha wa Tawi la CCM Mbagala anasema awali hawakuwa na lengo la kuanzisha chama cha kisiasa, bali asasi isiyo ya kiserikali (NGO), lakini baada ya kuwashirikisha wasomi kadhaa kuandaa rasimu ya katiba ya NGO hiyo, wanasheria walioipitia wakawaambia kuwa katiba hiyo ni zaidi ya NGO na kuwashauri waanzishe chama cha kisiasa.

“Hapo tukaanza kuzungumza na watu tunaofahamiana nao ndani na nje ya nchi, tukashauriana, tukachangishana na kuipeleka katiba yetu kwa Msajili wa Vyama vya Siasa, John Tendwa, na alipoisoma mwenyewe akakiri kuwa ile ndiyo katiba mbadala na bora kuliko nyingine karibu zote.

“Bahati mbaya au nzuri, kuna mwandishi wa habari aliipata katiba hiyo, akaitangaza siku mbili kabla ya uzinduzi wa chama chetu. Siku ya uzinduzi ikawa balaa! Chama kikajulikana kweli kweli. Tukatangaza kuwa katika kukitangaza chama mikoani, tungeanzia mkoa wa Mara nyumbani kwa Mwalimu Nyerere.

“Wafadhili wakajitokeza, tukapewa tiketi za ndege, tukaenda Butiama na kuzindua kazi zetu pale pale. Hakika ilikuwa tishio na kama tungeshiriki uchaguzi wa 2010, tungepata wabunge wengi sana na hata 2015 ninakwambia tutapata viti vingi.

“Sababu kubwa ni moja, CCK ndicho chama cha kukimbilia watu wasiopenda mizengwe, minyukano na walio tayari kuikomboa nchi yetu,” anasema.

Anamalizia kwa kuzungumzia ukombozi wa pili wa Tanzania, amesema rasilimali tulizo nazo ni lazima zitumike viwandani kwani bila viwanda hakuna maendeleo ya kiuchumi, muda umefika wa kujikomboa kutoka kwenye laana tuliyonayo.

Israel ndiyo nchi yenye teknolojia au watu waliobobea kwenye teknolojia duniani na ili tuendelee, tunapaswa kuwatumia watu hao (Waisrael) kwa kushirikiana nao tofauti na sasa ambapo hatuna uhusiano wa kibalozi
All the best. Roma was not built in a day
 
Sifa ya kuwa kiongozi bora kumbe ni lazima uwe kama Nyerere! I see
 
taarifa rasmi ya Chama Cha Kijamii kuhusiana na uchaguzi mkuu itatoka siku chace zijazo,tujuavyo ni kuwa Richard Kyabo ni mwanachama wa chama cha mapinduzi na hahusiki na ukada wa Chama Cha Kijamii.

Hakuna uchaguzi wowote unaoendelea kwa sasa ndani ya chama japo kuna kundi la watu likiongozwa na Akitanda na wenzake wa mitaani wameokotana hapo mbagala na temeke kumuhadaa msajili ya kuwa leo kunafanyika uchaguzi kitu ambacho si kweli.

ili uchaguzi mkuu ufanyike kunahitajika kuwe na matawi ya chama kutoka ngazi za vijiji,mitaa,kata,wilaya na taifa,na mpaka sasa hatuna uongozi uliokamilika katika mkoa hata mmoja wa Tanzania.

J.S.ALAWY
KATIBU MWENEZI WA MUDA - CCK TAIFA.
 
Duh naona AKATANDA anasifiwa msomi, Mandela wa Tanzania ama anaupeo wa Nyerere.

SWALI: AMEFANYA KITU GANI TUMFANANISHE NA NYERERE AMA MANDELA?

Msomi ana elimu gani? amelifanyia nini Taifa?
 
Kwa njia ya kimiujizaujiza sawa, cck yaweza. Lakini kisayansi mh!!!!
 
taarifa rasmi ya Chama Cha Kijamii kuhusiana na uchaguzi mkuu itatoka siku chace zijazo,tujuavyo ni kuwa Richard Kyabo ni mwanachama wa chama cha mapinduzi na hahusiki na ukada wa Chama Cha Kijamii.

Hakuna uchaguzi wowote unaoendelea kwa sasa ndani ya chama japo kuna kundi la watu likiongozwa na Akitanda na wenzake wa mitaani wameokotana hapo mbagala na temeke kumuhadaa msajili ya kuwa leo kunafanyika uchaguzi kitu ambacho si kweli.

ili uchaguzi mkuu ufanyike kunahitajika kuwe na matawi ya chama kutoka ngazi za vijiji,mitaa,kata,wilaya na taifa,na mpaka sasa hatuna uongozi uliokamilika katika mkoa hata mmoja wa Tanzania.

J.S.ALAWY
KATIBU MWENEZI WA MUDA - CCK TAIFA.

Hahahaha... Kuna harufu ya gogoro kufurukuta. Ina maana Mwenezi (J.S. Alawy) hamuelewani na mwnykiti (Akatanda). Siasa za bongo full comedy. Chama kimeanzishwa juzi, leo migogoro imeanza kumea. Hahahahaha..
 
taratibu basi jamani; uwanja mpana huu kila mtu anaweza kucheza.. vyama vingine vya upinzani havina sababu ya kuihofia CCK, chama kidogo na hakina watu wenye majina, hakina diwani wala Mbunge... waachwe wajijenge..

kweli Mzee Wetu... Ahsante kwa Busara zako.
 
Back
Top Bottom