101 East
JF-Expert Member
- Feb 25, 2015
- 1,040
- 2,121
Moja kati ya taarifa kubwa kuanzia Wiki iliyopita hadi Wiki hii ni taarifa ya uzazi na visababishi vyake kutoka kwenye Ripoti ya Afya ya Uzazi na Mtoto na Viashiria vya Malaria ya 2022 iliyozinduliwa hivi karibuni na Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Ripoti hiyo inaonesha kuwa utafiri kwa kulinganisha Mikoa umeonesha Wanawake wa Dar es salaam kiwango chao cha uzazi kipo chini kwa wastani wa Watoto 2.8 kwa kila Mwanamke huku Wanawake wa Mkoa wa Simiyu kiwango chao cha kuzaa kikiwa juu kwa wastani wa Watoto 6.6 kwa kila Mwanamke.
Wanawake wa Arusha kiwango chao ni wastani wa Watoto 4.7 kwa Mwanamke, Mwanza ni wastani wa Watoto 4.9, Tanga Watoto 5.2 kwa kila Mwanamke, Mbeya Watoto 4.3, Iringa Watoto 3.9 na Njombe wastani wa Watoto 4.0.
Ripoti hiyo inaonesha Wanawake wanaoishi katika maeneo ya Vijijini wana uwezo wa kuwa na Watoto wengi kuliko Wanawake wa maeneo ya mijini (wastani wa Watoto 5.5 dhidi ya 3.6 mtawalia).