Kiwango cha chini cha ujenzi daraja la Singida.

Kiwango cha chini cha ujenzi daraja la Singida.

Dingswayo

JF-Expert Member
Joined
May 26, 2009
Posts
4,019
Reaction score
2,932
Nimeangalia leo taarifa ya habari ya ITV nimeona jinsi daraja la Singida lilivyosombwa na maji. Mimi si mhandisi wa barabara, lakini nimeweza kuona kuwa kiwango cha ujenzi wa daraja lililosombwa kilikuwa cha chini mno. Sehemu ya njia ya maji ni pana mno, ikimaanisha kuwa kama kukiwa na mvua kubwa, maji yatakuwa mengi sana. hata hivyo ukiangalia 'daraja' lililojengwa ni culvert ambazo juu yake kumewekewa zege kidogo na kisha kujaziwa juu na kifusi cha mchanga.

Ujenzi wa namna hii ina maana kwamba kama kutakuwa na mafuriko (kama ilivyotokea) maji yatajaa na kupita culvert mpaka barabarani na kusababisha kusombwa barabara.

Kitu ambacho wahandisi wangefanya ni kujenga daraja imara la zege hadi kiwango cha bararabara na daraja hilo lizingatie pia upana wa njia ya maji.

Wakati umefika sasa tujifunze kujenga vitu vya kudumu na kuacha kufanya mambo kwa mzaha, tabia amabayo inatugharimu sana.
 
Mkuu,

Suala zima la viwango katika Tanzania yetu halimo.

Jana tu tumesikia watu wakilalama kuhusu mpango wa kurusha matangazo ya TV kwa digitali. Wengine wanasema hawaoni kabisa, wengine wanaona TBC peke yake n.k.

Ndiko tulikofikia mkuu, ikiwa vihiyo wanakuwa mawaziri, wanasaini mikataba bila kuelewa wanasaini kitu gani, wanajua hata kama hilo daraja haliko kwenye viwango vinavyokubalika? Kwao mradi walikuja kulifungua kwa mbwembwe nyingi, na hotuba kibao majukwaani na watu kushona sare na kuvaa kapelo, hilo daraja mbona linafaa tu? Vilaza watupu waliopo kwenye uongozi wa ngazi za juu serikalini, meradi tu walimpigia kampeni kigogo fulani basi. Kwa mtindo huu majanga kama haya tuyategemee mengi tu, sio hapo peke yake!

Mungu Ibariki Tanzania na watu wake!
 
Si ajabu hilo eneo lilipangwa lijengwe daraja lakini wajanja wakapiga juu kwa juu na kuzilamba billioni za daraja na kuweka hizo culverts. Mvua ndizo hizo zinaanza, tusubiri pale maeneo ya Same, maporomoko ya milima ya Iyovu, sehemu korofi za tambarare kati ya Shelui na Igunga, mteremko wa Sekenke, tambarare za Bahi, maeneo baada ya daraja la Mkapa etc. Kweli Tanzania ni muungano wa Zimbabwe, Zanzibar and Tanganyika in 11964!!!!
 
Asante kwa taarifa hiyo. Ina maana hata wakaguzi wa ujenzi hawakuona kuwa kutakuwa na tatizo. Kweli ufisadi utatumaliza kama tusipoamka na kusema basi imetosha!
 
Asante kwa taarifa hiyo. Ina maana hata wakaguzi wa ujenzi hawakuona kuwa kutakuwa na tatizo. Kweli ufisadi utatumaliza kama tusipoamka na kusema basi imetosha!

Hiyo siyo taarifa, ni hisia zangu tu!!! Haingii akilini ujenge mtaro wa kuelekeza majina wenye upana wa mita kumi halafu uweke culvert lenye mdomo wa kipenyo cha mita moja. Hapo utakuwa umejenga kinga maji (DAM) na siyo daraja!!!
 
kampuni iliyojenga ni CHICO-china henan international company : barabara ya bilion 65 unajengea culvert lenye kuzungukwa na bati?
 
Back
Top Bottom