Baba_Enock
JF-Expert Member
- Aug 21, 2008
- 7,076
- 2,443
Alfajiri ya leo tarehe 9 March 2012 nimepita Mwenge na kulikuta Lori la kubeba Saruji linalomilikiwa na Kiwanza cha Saruji cha Wazo lenye namba za usajiri T697 ATD likiwa limepinduka "miguu juu", na inaelekea dereva wake amepoteza maisha...!
Tukio hili linatokea takribani wiki moja tuu baada ya Lori jingine la kubebea saruji kuacha njia na kuparamia "pick-up" na nguzo ya umeme eneo la Tegeta-Kibaoni, nadhani pia liliua mtu mmoja...!
Ni bahati kuwa hizi ajali zinatokea maeneo ambayo kwa kawaida uwa yanakuwa na msongamano wa watu na Daladala, lakini wakati zikitokea maeneo hayo uwa hakuna msongamano wowote...! Vinginevyo maafa yanaweza kuwa makubwa mno. Kwa mfano hii ya leo imetokea eneo la Mwenge-mataa karibu kabisa eneo ambalo Daladala hushusha na kupakia abiria kutoka Tegeta, na kuelekea Ubungo,Mbezi, Buguruni, e.t.c...!
Swali ninalojiuliza, hiki kiwanda cha "Wazo" kinao mpango wowote wa kuondosha hali hii? Kwa maana kama nilivyoandika hapo juu, tunaweza kushuhudia ajali mbaya sana na ya kutisha kama hali ikiachwa hivi hivi...!
Waliopatwa na majanga ya ajali hizo mbili nawapa pole...!