Kiwanda cha MWATEX vipi?

Tutor B

JF-Expert Member
Jun 11, 2011
9,025
6,598
Habari za majukumu waungwana,

Napenda kuuliza kuhusu hiki kiwanda cha Mwatex kilichopo Mwanza jijini, kiliajiri wafanyakazi baada ya muda wafanyakazi walisimamishwa.

Cha kushangaza kuna tetesi kwamba kiwanda hicho kilifanyiwa hujuma kama viwanda vingine... hujuma yenyewe ni kuuza mitambo iliyokuwemo na kupaacha wazi.

Wenye kujua kuhusu hilo naomba mjitokeze ili tuendelee kumjuza Rais wetu aweze kufanya ufuatiliaji.

Nawasilisha kwenu watanzania wenzangu.
 
Ofisi ya mbunge wa Ilemela ambaye pia naibu waziri na ofisi ya DED Ilemela wanafahamu kinachoendelea.

Inasemwa mashine nyingi zimeuzwa huku chache zilizobaki wakitumia kuni badala ya umeme!

Pia ndani ya eneo la kiwanda kuna shughuli ya kupaki mafuta ya kula inafanaywa na wahindi wanaokiendesha kwa sasa. Wanaleta mafuta ya kula toka nje mwisho wa siku yanawekwa katika vifungashio vya mafuta yanayouzwa kwa wingi mtaani.

Jitihada za uongozi wa mtaa wa nyakato mashariki pamoja na kata umeshindwa kutumbua jipu hili kwani wahusika wanakula na wakubwa.
 
Ofisi ya mbunge wa ilemela amvbaye pia naibu waziri na ofisi ya ded Ilemela wanafahamu kinachoendelea.
Inasemwa mashine nyingi zimeuzwa huku chache zilizobaki wakitimia kuni badala ya umeme!
Pia ndani ya eneo LA kiwanda kuna shughuli ya kupaki mafuta ya kula inafanaywa na wahindi wanaokiendesha kwa sasa. Wanaleta mafuta ya kula toka nje mwisho wa siku yanawekwa katika vifungashio vya mafuta yanayouzwa kwa wingi mtaani.
Jitihada za uongozi wa mtaa wa nyakato mashariki pamoja na kata umeshindwa kutumbua iipu hili kwani wahisika wanakula na wakubwa.
Hao wakubwa ndo nawataka mimi ...

Umesema jambo mkuu, niliwahi kukuta gari kubwa la mafuta ya petrol liko nje - nikawa najiuliza linaingia humo kuna shughuli zipi wakati hata wafanyakazi hakuna .... walifanikiwa kukiondoa kituo kidogo cha polisi hili waendelee na mambo yao ya ajabu.....
 
J
Kimekuwa godauni la kuhifadhia mafuta ya kula ya wahindi
JPM anajua hilo???? ...
Uozo ulioko kwenye nchi hii haupaswi kufumbiwa macho. Kwa sasa kila mtu anaongelea sukari badala ya kufuatilia mambo mengine .... jamani tutatoboa kweli????
 
Ajabu hayo yote yanafanyika lakini mm u a kituo kikubwa cha polisi umbali wa mita chino ya 100. Kiasi ukiwa kituoni unaona kila kinachoendelea Mwatex.
Ajabu Jana kama SAA tano hivi nikamshuhudia polisi mmoja katika eneo LA Pepsi kamkamata mkaka wa watu kwa kuwa na mifuko miwili ya sukari na dumu LA mafu ta ya kula! Ikionyesha huyo jamaa anamiliki kibanda au duka lakini... Yuko nikononi mwa polisi
 
Wakati serikali ikitangaza kufufua viwanda, wabunge wa mkoa wa mwanza na kanda yote ya ziwa wanafahamu hili na wamepitisha bajeti ya kufufua viwanda! Mwatex oyeee
 
Wakati serikali ikitangaza kufufua viwanda, wabunge wa mkoa wa mwanza na kanda yote ya ziwa wanafahamu hili na wamepitisha bajeti ya kufufua viwanda! Mwatex oyeee
siamini kama wabunge wetu Ilemela na Nyamagana wana uchungu na Mwanza ... wote nawaona kama ni bora liende ...
 
Wabunge hawa hawapaswi na hawawezi kuwa na machungu na mwanza, walichokuwa wanatafuta walipata na sio hayo machungu, hayakuwa ajenda yao.

Suala LA muhimu ni kwa wana Mza kuamka na kujitambua mnataka iko wapi Mza ya 1980 iliyokuwa na viwanda lukuki?

Cha ajabu Leo naona Karibu kila eneo kuna chuo au chuo kikuu lakini mazao yake..
 
Bora wahitimu wa Form IV ya miaka ya 90 kuliko wahitimu wa vyuo wa miaka ya 2000.
 
Huwa najuliuliza mkapa kubinafisha viwanda alikuwa anatumia vigezo gani? Mwatex licha ya ajira na kuzalisha nguo bora zaidi ya zinazotoka China na India ilikuwa tegemeo kwa wakulima wa pamba. Hahaha pamba!!
 
JIBU LAKE KULIPATA NI NGUMU ...
NA JE! KUUZA NYUMBA WATUMISHI WA SERIKALI WAKAPANGA MAHOTELINI?

NCHI HII INA MAMBO YA AJABU .. EBU TUONE TRACK NO. 5 INACHEZEKA VIPI ..... ..
 
Back
Top Bottom