Kiwanda cha Megatrade kifungwe

rr4

JF-Expert Member
Mar 19, 2015
3,346
4,657
Tafadhali Mheshimiwa WAZIRI wa viwanda, please funga kiwanda cha viroba jogoo. Tafadhali sana. Vijana hawafai, wadogo zetu hawawezi kuoa tena. Hali ni mbaya sana.

MAGUFULI KAMA UTASOMA HAPA PLEASE ACT FAST. FUNGA MEGATRADE PLEASE.
 
Nafikiri ameshaanza kufuata sheria za kunywa vileo kuanzia saa kumi.
Kama bado watu wanakunywa kinyemela kwa kujificha hiyo itakua suala lingine.
Mwishoni tutaanza kuiomba serikali izuie hata uuzaji wa sumu za panya kwa kuwa kuna watu watajiua kwa utashi wao
 
kiko wapi hiko?????kila kaz sio ya rais
ndomaana kukawa na mamlaka husika za kusima100 hizo kaziiiiiiiiiiiiiiii
usijali ombi lako limefika ntajitahidi kulifikisha kwa wahusika,..
 
Nafikiri ameshaanza kufuata sheria za kunywa vileo kuanzia saa kumi.
Kama bado watu wanakunywa kinyemela kwa kujificha hiyo itakua suala lingine.
Mwishoni tutaanza kuiomba serikali izuie hata uuzaji wa sumu za panya kwa kuwa kuna watu watajiua kwa utashi wao

Kufunga kiwanda kimojawapo ambacho hakivunji sheria siyo suluhu ya tatizo maana hata Kama vingefungwa viwanda vyote vinavyotengeneza pombe za spirit kwa hapa nchini bado serikali itakuwa imeloba kwani badala ya kumaliza tatizo moja itakuwa imejiongezea matatizo ikiwepo pamoja na kujinyima kodi zinazokusanywa kutokana na
Uzalishaji huo kuwepo nchini, pia kuna watu watakaokosa ajira lakini hii haitazuia pombe kuwepo ndani ya nchi kwani wafanyabiashara wataingiza kutoka nje ya nchi muhimu Kwao ni kuangalia ikiwa tu ni kwa kiasi gani bidhaa hiyo inavyohitajika ktk soko.

Ni bora tungeshauri zipangwe na kutungwa sheria za utengenezaji, usambazaji na matumizi bora ambayo hayatatoa nafasi kwa watumiaji kutumua hovyo na bila adabu Kama ilivyo kwa sasa .

Tukianzia kwa watengeneji;
ipigwe marufuku ya kufunga kwenye vifuko vya plastiki ambavyo gharama yake ni nafuu na inatoa fursa kwa mtumiaji hasa wa kipato cha chini kumudu gharama hiyo kwa urahisi,basi ifungwe ihifadhiwe kwenye chupa za Kioo ili kuiongezea gharama hii itapunguza walaji kwa kiasi kikubwa,

Kwa wasambazaji: limekuwa ni jambo la kawaida sana kupata vibanda vidogo vidogo vilivyokuwepo kwa sura ya udanganyifu wa kuuza vocha za simu na kutoa huduma ya maji ya kunywa na vinywaji baridi Kama soda n.k kwenye maeneo ya mikusanyiko ya watu wengi hasa ndani na nje ya masoko na hasa zaidi vituo vya mabasi makubwa na hata madogo,lakini hawa ndio wauzaji wakuu wa hizi vinywaji vikali, hawa nao wangedhibitiwa

Kumekuwepo na zoezi la kutokufunguliwa baa wakati wa kazi asubuhi ni hadi jioni huu ni mpango mzuri lakini Kama baa zitakuwa zimefungwa na wakati huo sehemu hizi za vibanda nilizozitaja zenyewe zikaachiwa tu kuendesha biashara hizo bila usimamizi wa taratibu bado tutakuwa hatuna nia nzuri ya kupambana NA kusimamisha unywaji wa pombe kiholela.
Ni vizuri ikiwa tumeamua kupambana na unywaji pombe holela tukaangalia na upatikanaji wake pia
Na tena tuweke sheria ya umri wa kuingia sehemu zinazotoa huduma hizi za pombe iwe ni zaidi ya miaka 18 na kuendelea halafu yake iwekwe bayana adhabu atakayokumbana nayo mtu atakaevunja sheria hizi. Hapo discipline ya matumizi ya pombe utaiona ikijichukulia nafasi yake taratibu.
 
Hiki kifungwe ni hatari
 
HIKI MKUU KIFUNGWE. NO MAELEZO, WATU WANAHARIBIKA KASKAZINI.
 
Acheni Upuuzi, kwann usiseme TDL, kila bidhaa inayozalishwa pale imethibitishwa na TBS, na kwa taarifa tu ni kwamba Kampuni za Vileo ndo zinaongoza kwa kulipa Kodi Tanzania, kwahiyo acha kuota ndoto za Mchana.
 
Kufunga kiwanda kimojawapo ambacho hakivunji sheria siyo suluhu ya tatizo maana hata Kama vingefungwa viwanda vyote vinavyotengeneza pombe za spirit kwa hapa nchini bado serikali itakuwa imeloba kwani badala ya kumaliza tatizo moja itakuwa imejiongezea matatizo ikiwepo pamoja na kujinyima kodi zinazokusanywa kutokana na
Uzalishaji huo kuwepo nchini, pia kuna watu watakaokosa ajira lakini hii haitazuia pombe kuwepo ndani ya nchi kwani wafanyabiashara wataingiza kutoka nje ya nchi muhimu Kwao ni kuangalia ikiwa tu ni kwa kiasi gani bidhaa hiyo inavyohitajika ktk soko.

Ni bora tungeshauri zipangwe na kutungwa sheria za utengenezaji, usambazaji na matumizi bora ambayo hayatatoa nafasi kwa watumiaji kutumua hovyo na bila adabu Kama ilivyo kwa sasa .

Tukianzia kwa watengeneji;
ipigwe marufuku ya kufunga kwenye vifuko vya plastiki ambavyo gharama yake ni nafuu na inatoa fursa kwa mtumiaji hasa wa kipato cha chini kumudu gharama hiyo kwa urahisi,basi ifungwe ihifadhiwe kwenye chupa za Kioo ili kuiongezea gharama hii itapunguza walaji kwa kiasi kikubwa,

Kwa wasambazaji: limekuwa ni jambo la kawaida sana kupata vibanda vidogo vidogo vilivyokuwepo kwa sura ya udanganyifu wa kuuza vocha za simu na kutoa huduma ya maji ya kunywa na vinywaji baridi Kama soda n.k kwenye maeneo ya mikusanyiko ya watu wengi hasa ndani na nje ya masoko na hasa zaidi vituo vya mabasi makubwa na hata madogo,lakini hawa ndio wauzaji wakuu wa hizi vinywaji vikali, hawa nao wangedhibitiwa

Kumekuwepo na zoezi la kutokufunguliwa baa wakati wa kazi asubuhi ni hadi jioni huu ni mpango mzuri lakini Kama baa zitakuwa zimefungwa na wakati huo sehemu hizi za vibanda nilizozitaja zenyewe zikaachiwa tu kuendesha biashara hizo bila usimamizi wa taratibu bado tutakuwa hatuna nia nzuri ya kupambana NA kusimamisha unywaji wa pombe kiholela.
Ni vizuri ikiwa tumeamua kupambana na unywaji pombe holela tukaangalia na upatikanaji wake pia
Na tena tuweke sheria ya umri wa kuingia sehemu zinazotoa huduma hizi za pombe iwe ni zaidi ya miaka 18 na kuendelea halafu yake iwekwe bayana adhabu atakayokumbana nayo mtu atakaevunja sheria hizi. Hapo discipline ya matumizi ya pombe utaiona ikijichukulia nafasi yake taratibu.
You said it all, only great thinkers ndo watakuelewa.
 
NASHUKURU ARUSHA NASIKIA VIROBA MARUFUKU. SASA NA MOSHI TUFUATIE. SHENZY.
 
Sio kufunga wapaki kwenye chupa 2 mills 300 huko bei ipande kdogo..biashara kama kawa
 
WAZO ZURI PIA. HIZI SACHET NI TOO CHEAP, ANY TOM AND DICK CAN BUY. AU PAKETI IWE 3,000/=.
Hyo itasaidia lkn huwezi kuwaambia et waache kuuza au wafunge kiwanda kama pombe kali ziko nyingi zinauzwa kali hata zaid ya viroba.
 
Inaonekana hawana nidhamu kwa matumizi ya pombe kwa nini huko kaskazini kama unavyosema!!?

SIO NIDHAMU MKUU. KITU KINAUZWA BUKU, UKIGONGA VIWILI TU NA JUA LIKIWA LINAWAKA UNAONA MBILIMBILI. NI HATARI SANA. MOSHI KONA YA MAWENZI PALE USISEME HALAFU NI KARIBU NA POLISI, BODABODA WANATOA LOCK TU.
 
Back
Top Bottom