Mwanzo kabla sijasoma post yote nilishangaa kidogo, nilijiuliza mbona magari haya yanafanana na magari ya kichina! na kweli ni(CKDs) za Kichina - siwasemi vibaya wa Nigeria nawapongeza. Tuwe wakweli hapa Wafrica mpaka tufikie hatua ya kumimina Engine blocks na ku-manufacture subassemblies zote za Engine mpaka ifikie kufanya kazi sioni kama hilo linaweza kufikiwa in our lifetime, tutaishia kuhunga hunga magari ya wenzetu na kuyapachika a local name lakini sio ku-manufacture magari per se. Nani atakubali kukuhuzia/kukujengea a modern forge an foundry Shops,pattern shops, heat treatment shops, modern labs za material/hardness testing, modern electroplating shops, sophisticated machine tools,R&D nk hivyo ndivyo vitu vya muhimu katika uhundaji wa magari, lakini cha umuhimu zaidi ni skilled labour i.e wenye elimu na uwezo wa kutumia vifaa hivyo effectively.