Kiwanda cha kusindika muhogo Bungu kimeanza uzalishaji?

malewa

Member
Joined
Feb 23, 2015
Posts
15
Reaction score
4
Wadau tunakaribia msimu wa mavuno ya zao la muhogo kwa wingi hasa kutoka mikoa ya kusini mwa Tanzania na baadhi tayari wameanza kuvuna. Soko la zao hili limekuwa halina uhakika sana kutokana na kutokuwa na viwanda vya kusindika muhogo hapa nchini hivyo kilimo cha zao hili kutowanufaisha sana wakulima.

nilifarijika sana kusikia habari za kuzinduliwa kwa kiwanda cha kusindika muhogo katika kijiji cha Bungu Wilayani Rufiji kilichozinduliwa kwenye mwezi Julai 2014 kama sijakosea. Kwa hakika kiwanda hiki kinaweza kuwanufaisha zaidi wakulima wa zao hili na kuchangia kwa kiasi kikubwa ukuaji wa uchumi wa nchi yetu.

Kwa kuwa sasa msimu wa mavuno ya muhogo umeanza, ningependa kujua kama kiwanda hicho kimeanza kununua muhogo pamoja na utaratibu unaotumika kununua muhogo. Wadau, nami ni mmoja wa wakulima waliolima zao hili kwa mwaka huu. Mwenye taarifa tafadhali naomba msaada.
 
Mkuu ulipata kufahamu kuhusu hicho kiwanda?
 
Wakati kinajengwa nlikuwa kwenye pilikapilika za kwenda shambani kwangu hapo ikwiriri,nliskiaga muda kuna kiwanda kinajengwa kama watakuwa wameanza kazi basi hiyo ni habari njema!Kwa wakulima wa mihogo

Ova
 
Hakuna majibu sahihi... hata wakazi wa Rufiji pia hawapo??

Mihogo yangu jamani.
 
Back
Top Bottom