Kiwanda cha karatasi Mgololo chatozwa faini ya Millioni 20 kwa kuvunja sheria

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,557
21,507
Serikali imekitoza faini ya shilingi milioni 20 kiwanda cha karatasi cha Mufindi kilichopo Mgololo mkoani Iringa kwa kutiririsha maji machafu yanayotoka kiwandani hapo bila kuyasafisha hali inayotishia maisha ya watu na viumbe hai wanaotumia maji ya mto Kigogo.

Mratibu wa Baraza la Taifa la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC Kanda ya Nyanda za juu Kusini Godlove Mwansojo amesema baraza hilo limelazimika kutoza faini hiyo kutokana na kiwanda hicho kukiuka sheria za uhifadhi wa mazingira kwa mujibu wa vifungu vya sheria namba 186 na 198 ya mwaka 2014 kwa kutiririsha maji machafu yanayotoka kiwandani hapo bila kuyatibu.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Luhaga Mpina ameuagiza uongozi wa NEMC Kanda ya Nyanda za juu Kusini kusimamia vema suala hilo na kuhakikisha kiwanda hicho kinatimiza vigezo vya uzingatiaji wa sheria za mazingira ndani ya kipindi cha wiki mbili.

Kwa upande wake Meneja Mkuu wa kiwanda hicho ambacho ndicho pekee kinachozalisha karatasi humu nchini Bw.Yerra Choudary amesema wapo tayari kulipa faini hiyo licha ya kutoridhishwa na matakwa hayo ya kisheria kutokana na kutofautiana na viwango vya dunia.
 
Back
Top Bottom