ManiTek TV
JF-Expert Member
- Jun 3, 2011
- 410
- 159
Baada ya kutembelea kiwanda cha BMW Mini Cooper kilichopo Oxford, kiwanda pekee kinachotengeneza gari hizo Duniani, tutaeleza kwa ufupi kabisa mambo machache kuhusu kiwanda hicho na gari hii. Mini Cooper ambayo miaka michache iliyopita ilipozalishwa toleo ya kwanza ilipata soko zuri katika baadhi ya nchi, huku tangazo kubwa la gari hiyo likiwa ni ushirikishwaji wa gari hii katika sinema ya Italian Job.

Kiwanda hicho kinakamilisha uzalishaji wa gari moja mpya kila baada ya sekunde 6, usiku na mchana, hii maana yake katika kila hatua moja ya utengenezaji wa gari hii hakuna inayozidi muda ambao kila gari moja humalizika. Kwa mfano hatua ya muoano kati ya injini na gari, yaani hatua ya kuiingiza injini kwenye gari yenyewe inachukua muda wa sekunde tano na inafanywa na roboti wawili tu.
Hatua ya kupachika kioo cha nyuma kwenye gari nayo hutekelezwa na roboti wawili, wa kwanza hufanya kazi ya kupima iwapo mpira unaozunguka sehemu ya kuweka kioo imewekwa kwa vipimo vilivyo sahihi, iwapo vipimo haviko sawa inapeleka taarifa kwenye utaratibu mzima (system) na gari ile hupita bila ya kuingizwa kioo, na badala yake huja kuingizwa na mafundi kwa kutumia mikono, mafundi hupata maelekezo ya karatasi inayochapishwa na taarifa ya roboti yule juu ya hitilafu iliyosababisha roboti asiweke kioo. Hatua hii hutekelezwa mwishoni kabisa baada ya gari kutolewa kwenye mkanda wa utengenezaji. Iwapo vipimo vitakuwa sawa roboti yule anatoa taarifa na robiti mwengine ambaye anafanya kazi ya kupachika kioo. Muda ambao roboti wawili hawa huuchukua kukamilisha hatua hii ni sekunde nne.

Waya ambazo zinaingizwa kwenye gari za BMW Mini Cooper iwapo zitaunganishwa zote na kufanya waya mmoja zitakuwa na urefu wa kilomita mbili. Utengenezaji wa gari hii umegawanywa katika jumla ya hatua 220, na hushirikisha wafanyakazi 2000, ikiwa ni pamoja na wanafanyakazi wa ofisi na utawala, na kuna shift mbili katika kiwanda hicho, hivyo kiwanda kina jumla ya wafanyakazi 4000. Mashine za kiwanda hicho huwa hazizimwi isipokuwa tu kwa dhararu na kila inapozimwa mashine utawala unahesabu kuwa umepata hasara ya £17,000 katika kila sekunde sita, muda ambao unachukua kukamilisha gari moja, ha hasara hii ni wastani wa bei ya gari hiyo.
Kiwanda hichi kilianzishwa mwaka 1913, na gari ya kwanza ilijulikana kama Morris Oxford iliuzwa kwa £195 mwaka 1914, gari hiyo (iliyo pichani) ilikuwa na gia tatu kwenda mbele na ya kurudi nyuma (reverse), pia Morris hiyo ilikuwa na siti mbili tu. Gari hii kwa wakati huo ilipata umaarufu jina la Bull Nose kutokana na Umbile lake la mbele. Gari aina ya Mini ya kwanza ilitengenezwa mwaka 1959. Mini ya kwanza ilitamba mno katika miaka ya sitini.
Mini Cooper hutumia utaratibu wa mauzo tofauti na utaratibu wa kawaida, yaani wao hufanya mauzo kwa oda tu. Iwapo mteja atatoa oda wastani wamuda wa kusubiri gani ni kuanzia wiki sita hadi miezi mitatu kutegemeana na oda zilizomtangulia mteja huyo na mambo ambayo ameyachagua kuwekwa kwenye gari yake, hapa utaweza kujua kiasi gani utawala huchanganyikiwa inapotokea tatizo ambalo linabidi mkanda wa uzalishaji usimamishwe. Kiwanda hichi huchukua oda kutoka kwa wafanya biashara ya kuuza magari na hata watu binafsi moja kwa moja kupitia mtandao wao.
Chanzo: www.gajetek.com