Kivipi jamii yako imenufaika na elimu yako???

Konseli Mkuu Andrew

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2013
Posts
748
Reaction score
887
Nipende kuchukua nafasi hii kuzipongeza jamii za miaka ya nyuma kwa kusomesha vijana kwa ajili ya kuja kusaidia changamoto zilizoikabili jamii za wakati huo,miaka ya nyuma watu walikuwa wanalipiwa ada na vijiji ili waje kuwa wataalamu wa kilimo na mifugo au sheria na kweli vijana hao wakaja kuwa watatuzi wa changamoto hizo.

Mambo yamebadilika kwa miaka ya hivi sasa,watu hawalipiwi tena ada na vijiji wanalipiwa ada na familia zao na ata jamii watokazo hawafaidiki kwa lolote na elimu za vijana hao.Kwa mfano unakuta mtu kasoma masuala ya kilimo au mifugo na jamii anayotokea pana changamoto za kilimo,kijana huyo mtaalamu wa kilimo hafanyi jambo lolote la ufumbuzi wa changamoto hiyo na badala yake muda wote unamkuta kwenye Play stations kucheza magame.Swali la kujiuliza ni kuwa huko mavyuoni huwa kuna somo linaitwa Play Station?

Mwingine unakuta kasoma masuala masoko na jamii anayoishi kuna wamama wanajishughulisha na biashara ndogo ndogo na wana changamoto ya masoko,lakini unakuta huyo aliyesoma masuala ya masoko hafanyi lolote lile kuwasaidia hao wakina mama na badala yake muda wote yupo na baasha kusaka ajira.

Hali hii inapelekea ata wale wasio soma kuona elimu ya Tanzania ni bure maana hawaoni manufaa yatakanayo na elimu..
 
Kwa haraka haraka upo sahihi kuwaza hivyo,lakini ukitulia zaidi umeandika bila kuitafiti jamii yetu vizuri. Kwa asili sisi ni wagumu mno kubadilika,tunaishi kwa mazowea sana. Ni vigumu mno kuwabadilisha mtazamo watu wetu,hata kijana akijaribu ataambulia kejeli na msuto tu. Like tunafanyaga hivi hivi siku zote,wewe inakuhusu nini,nani kakutuma,kamsaidie mama yako,mpaka anakata tamaa. Kiufupi tunachukia elimu hasa ya bure.
 
Uzi mzuri, kwanza lazima ufahamu jamii yetu kwa kiwango kikubwa hawaheshimu wataalamu wamezoea kufanya vitu kwa mazoea hivyo ushauri wa vijana wataalamu umekuwa ukipuuzwa

Binafsi jamii inayonizunguka kuanzia familia yetu wamefaidika sana na kaelimu kangu japo kadogo, I'm medical practitioner kwa hiyo naulizwa maswali kuhusu afya kwa ujumla ana kwa ana or kwenye cm. Yaani cm zinakuwa nyingi hadi inakuwa usumbufu
 
Mkuu unakosea sio jamii zote zipo hivyo pia ukianza safari inatakiwa ujue kutakuwa na vikwazo
 
Uzi mzuri, kwanza lazima ufahamu jamii yetu kwa kiwango kikubwa hawaheshimu wataalamu wamezoea kufanya vitu kwa mazoea hivyo ushauri wa vijana wataalamu umekuwa ukipuuzwa

Binafsi jamii inayonizunguka kuanzia familia yetu wamefaidika sana na kaelimu kangu japo kadogo, I'm medical practitioner kwa hiyo naulizwa maswali kuhusu afya kwa ujumla ana kwa ana or kwenye cm. Yaani cm zinakuwa nyingi hadi inakuwa usumbufu
Kwanza hongera kwako mkuu kwa elimu yako kuwa na faida na jamii inayokuzunguka.

Pili ni kweli kuwa jamii nyingi hasa za Afrika zina desturi ya kupuuza wataalamu lakini sababu ni wasomi wenyewe wanavyojiweka katika jamii..
 
Ni sahihi mkuu unakuta msomi/ mtaalamu wa mambo fulani kila siku yeye ni kulewa tu au ni uzinzi tu au matusi , ugomvi n.k sasa kwa tabia hizi na nyinginezo ndizo hupelekea jamii zetu kuwapuuza wasomi wetu na kutokuwa na imani nao kutokana na matendo wanayoyafanya mbele ya jamii tena bila aibu yoyote.
 
Ni tofauti kabisa na miaka ya nyuma
 
Kwa haraka haraka upo sahihi kuwaza hivyo,lakini ukitulia zaidi umeandika bila kuitafiti jamii yetu vizuri. Kwa asili sisi ni wagumu mno kubadilika,tunaishi kwa mazowea sana. Ni vigumu mno kuwabadilisha mtazamo watu wetu,hata kijana akijaribu ataambulia kejeli na msuto tu. Like tunafanyaga hivi hivi siku zote,wewe inakuhusu nini,nani kakutuma,kamsaidie mama yako,mpaka anakata tamaa. Kiufupi tunachukia elimu hasa ya bure.
Kwahiyo sekta ya elimu ifutwe au? Kuibadilisha jamii ni elimu pia na hutolewa ktk gani zote za elimu, kuna vitu vinaitwa managerial skills, saikolojia, falsafa, uongozi nk ni sehemu tu ya taaluma zinalosaidia hilo. Kushindwa kuibadili jamii kwa mbinu zote zote ni kushindwa kwa elimu yako.

Nadharia ikishindwa vitendo vitafundisha, nenda kalime kwao, watajifunza kutokana na ulichokipata. Jamii haibadilishwi kwa ghafla ni process.
 
Ni kweli mkuu kuibadirisha jamii sio jambo la muda mfupi ni mchakato wa muda mrefu.
 
Mkuu japo nina kaelimu kadogo sana ila nimejitolea kuwafundisha masikini wenzangu wasio na uwezo wa kumudu tutions bure
Pia, wafundishe juu ya umuhimu wa elimu ktk maisha, changamoto zake na jinsi ya kuzitatua, mfano ajira nk, waelimishe kwamba mantiki kuu ya elimu ni kumwezesha mpokeaji kuweza kuyamudu mazingira yake.
 
Back
Top Bottom