Kiuno kuuma hasa kwenye baridi

king kan

JF-Expert Member
May 6, 2011
1,629
2,043
Wanajamii wenzangu!

Kwanza niwatakie mapumziko mema ya kumalizia weekend.

Tatizo kuu linalonisibu mimi, ni kuumwa sana hasa nyakati za baridi kiunoni na kwenye makorodani. Tatizo hili mara nyingi hunipa shida kiasi kwamba nikitaka kutembea natembea kwa shida na hata kubadili position nikiwa nimekaa huwa napata tabu kiasi.

Tatizo hili limekuwa ni la muda mrefu lakini halitokei mara kwa mara kwa wastani yaweza kupita hata miezi mitatu halijatokea. Na mara nyingi linapotokea huwa ni nyakati ambazo ninakuwa na appointment za kufanya mapenzi.

Ndugu zangu naombeni ushauri maana hali sasa ni tete. Nawashukuru wote mtakaotoa muda wenu kunisaidia kwa namna moja au nyingine.
 
Mkuu.@king kan PPole sana kwa kuumwa na hayo Maradhi hujatuambia umesha kwenda hospitali na walisha wahi kukupima?Umetumia dawa gani? na inaonyesha wewe haupo nchini Tanzania upo nje ya Tanzania kwenye nchi za baridi? Ninakuomba uyajibu hayo maswali yangu?
 
Mkuu Mzizi mkavu sijawahi kwenda hospitali na kupata vipimo vya aina yeyote kwa sababu kuna kipindi nilimcontact daktari mmoja na kama unavyojua madaktari wetu akaniambia nenda kesho ukiendelea hivihivi urui, kesho yake nilikua poa hivyo sikwenda tena. Sasa kwa kuwa hili tatizo huwa linanikumba kwa muda mchache ndani ya siku na hutokea baada ya muda mrefu sikuwahi kulipa umuhimu sana. Kuhusu makazi mie naishi Tanzania, na baridi ninayoiongelea hapa ni kale kabaridi ka jioni hasa pale ninapokuwa nje ya Dar-es-Salaam ( sio siku zote panapokuwa na baridi bali hutokea mara mojamoja).
Na tumaini nimekujibu maswali yako mkuu.
 
Last edited by a moderator:

Mkuu king kan itabidi uende Hospitali kuu ya Muhimbili ninakushauri ukaonane na

Daktari akupime na kujuwa chanzo cha hayo matatizo yako ni nini ndipo atakapo kupatia Dawa za kutumia hapa hutoweza kupata

msaada wowote ule mpaka uende kuonana na Daktari, huo ndio ushauri wangu .
 
aksante mkuu naufanyia kazi ushauri wako
 
Back
Top Bottom