Jamani, kuna namna huwa nakaa nafikiria juu ya masuala kadhaa bila kupata majibu yake, sasa leo hili limenisumbua na ninaomba great thinkers wa JF mnisaidie majibu yake. Jamani ni kiumbe gani ambacho kinapokufa na kuoza kinatoa harufu nzuri na ya kuvutia kwa watu/binadamu?
Viumbe ni vitu ambavyo mwenyezi Mungu aliumba hapo mwanzo mwa ulimwengu huu na dunia.
Hivyo kuna aina mbili ya viumbe
1. Viumbe hai 2. Viumbe visivyo hai
1. Viumbe hai vina sifa zifuatazo hukua, huzaa, hula chakula, sifa ya mjongeo, hutoa taka mwili, sifa ya kuhisi n.k mfano wa viumbe hai ni aina zote za wanyama pia akiwemo binadamu, miti na mimea aina zote
2. Viumbe visivyo hai vina sifa kinyume na viumbe hai kama kuto kukua, havili chakula, havitoi taka mwili, havina sifa ya mjongeo, havihisi kitu mfano wa viumbe visivyo hai ni pamoja na aina zote za miamba, maji n.k
Pia kuna viumbe wengine ambao wanasayansi wameshindwa kuwatafutia makundi yao kisayansi, hao ni viumbe ambao wameumbwa na mwenyezi Mungu lakini hawaonekani mfano wa hao viumbe ni majini, mapepo, kuna viumbe wengine ambao wamepewa majina kama Unidentified Flying Objects - UFO's na Alliens.
Hivyo nikienda kwenye swali lako kwamba ni kiumbe gani kikifa hakitoi harufu ni kwamba ili kiumbe kife na kutoa harufu inategemea kimeumbwa na aina gani za seli, tissues, molecules, pia ni aina gani ya mnyama kama ni carnivoles, reptiles n.k
Hivyo ninaweza kusema kwamba miti na mimea mbalimbali vinakuwa katika kundi la viumbe ambao wanakufa na kutoa harufu nzuri.
Note:
Haya ni maoni na uelewa wangu ila wajuzi wataongezea zaidi.