Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,209
- 25,546
Nawiwa kukiri kufahamu kuwa jana limetolewa tangazo Bungeni kuwa Ubunge wa Tundu Antipas Lissu wa Singida Mashariki umekoma na jimbo lake liko wazi. Nimefahamu haya hapahapa JF kupitia bandiko la kaka na mtani wangu Pascal Mayalla.
Nimesoma na kusikia tangazo la Spika ambalo hasa limejikita kwenye mambo mawili: utoro wa Lissu Bungeni ( kutojulikana alipo na anachofanya) pamoja na kutojaza Fomu za Maadili ya Viongozi. Hayo ni mambo ya kisheria na kiutaratibu.
Niweke wazi kabisa hapa kuwa mimi ni muumini wa utii wa sheria na taratibu zilizowekwa. Kila Taasisi na jumuiya ya watu huwa na sheria na taratibu za kufuata, Bunge halikadhalika. Kufuata sheria na taratibu huponya,huepusha na kulinda. Kutofuata hutisha,huathiri na kuadhibu. Aliyoyasema Spika ni masuala ya kisheria na kiutaratibu.
Mkuu BAK amepandisha uzi wenye majibu ya Lissu kwa jambo lililojitokeza jana. Alikuwa akizungumza na BBC. Nimevutiwa na kupata mambo mawili. Mosi, Lissu analenga kufungua shauri Mahakama Kuu ya Tanzania kupinga uamuzi wa kukoma kwa Ubunge wake na jimbo lake kuwa wazi kwa sababu zilizotajwa. Pili, Lissu amesema kuwa kuna mawasiliano ya barua kati ya Ofisi ya Katibu wa Bunge na familia yake kuhusu maendeleo yake kiafya.
Barua husika aliandikiwa kaka wa Lissu, kwa niaba ya familia na Lissu mwenyewe. Ni Wakili Msomi Mwandamizi Alute Mughwai ndiye kaka wa Lissu. Kuandikiana barua humaanisha kufahamika mahali wahusika wa barua hizo walipo. Na kujua na kinachozungumziwa. Hakika,ni barua muhimu.
Kwangu binafsi, sababu ya utoro na kutojulikana alipo Lissu ni kuu kuliko iliyobaki. Ni kwakuwa inayofuata huweza kumalizwa nguvu na uamuzi juu ya hiyo. Yaani, ikithibitika kuwa Bunge lilijua lipokuwepo Lissu na alichokuwa akikifanya, ujazaji wa fomu za maadili unazungumzika. Kama alikuwa mgonjwa,angejazaje?(kwa mfano).
Ndiyo maana nasema kuwa kama kweli kulikuwa na barua kutoka Ofisi ya Katibu wa Bunge maana ya haraka ni kuwa Bunge lilifahamu alipokuwa Lissu na alichokuwa akikifanya. Kama barua hiyo ipo, Spika alipaswa kujua kabla ya tangazo lake.
Naamini, 'barua' ya Katibu wa Bunge kwa familia ya Lissu inaweza kupindua matokeo mapema sana baada tu ya mechi kuanzia kuchezwa Mahakama Kuu ya Tanzania. Tusubiri tuone!