Kitwana Kondo alipofichua jina la mpelelezi wa waingereza ndani ya TANU 1950s

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,839
30,168
Leo katika maziko ya Mzee Kitwana Kondo niliombwa nizungumze maneno machache kuhusu mzee wangu huyu. Ukweli ni kuwa nilikuwa nimeshtukizwa kwani sikutaarifiwa kabla kuwa niko katika orodha ya wazungumzaji. Lakini mtu ukitumwa na waliokupita makamo huna khiyari ila kutii. Ndipo nilipozungumza yale yaliyopitika baina yangu na Mzee Kondo tarehe 12 Septemba 2012 nilipokwenda kufanya mahojiano na yeye kwa ajili ya kipindi changu cha TV Imaan, ‘’Walioacha Alama Katika Historia.’’ Siku ile wakati vijana wa picha na sauti walipokuwa wanajitayarisha kurekodi ghafla Mzee Kondo akaniita akanambia nikakae pembeni yake ana jambo anataka kuniambia. Ndipo akanieleza haya ambayo ninayeleza hapo chini bila kutaja jina la mpelelezi yule, jina ambalo Mzee Kondo alinitajia na akaniambia nisieleze historia hii hadi yeye atakapokuwa ameondoka duniani.

Mohamed Said: KITWANA KONDO ALIPOMFICHUA MPELELEZI WA WAINGEREZA NDANI YA TANU 1
Mohamed Said: KITWANA KONDO ALIPOMFICHUA MPEPELEZI WA WAINGEREZA NDANI YA TANU 1950s 2
 
Kama maelezo yapo tofauti maana hiyo video huyo mtu hujamtaja na wewe wadai alikuambia umtaje au ndie Hamza? Na hilo la Uislam lazima uliweke kwani? Na uzuri leo umeweka wazi kuwa Uislam ulikuwa haukubaliki kamwe na bila nyerere pengine hadi leo tungekuwa chini ya Uingereza... safi sana Ukristo oyeee ni wakushukuriwa na kuenziwa kwa kila namna.
 
Duduwasha,
Huu ndiyo uzuri wa kuwa na historia ya kweli na kwa uwazi watu wakaisiki na
kuisoma kisha kika mtu akawa na mawazo yake huru katika tafsiri ya historia
hiyo.

Huyu kachero hakika sikumtaja na pale msibani nilieleza hili kuwa sitamtaja.
bahati mbaya hii haipo katika hiyo clip.

Lakini ikiwa utakuwa umefuatilia katika historia hii ya Abdul Sykes katika
juhudi zake za kuunda TANU, utakuwa umesoma safari ya Abdul kutoka
Dar es Salaam kwenda Nansio kuonana na Hamza Mwapachu ili apate
kauli yake kuhusu kumunuingiza Nyerere katika uongozi wa TAA 1953
na mwaka unaofuatia, 1954 waunde TANU.

Sasa ikiwa umesoma utaliona jina la huyu kachero wa Waingereza.
Umeniuliza kwa nini nimetaja Uislam.

Labda nami nijibu swali lako kwa kukuuliza swali pia kwa nini nisitaje Uislam.
Lakini kulikuwa na ''wind of change,'' yaani upepo wa uhuru ulikuwa unavuma
Afrika na hili Waingereza walilitambua na walijitayarisha kuziachia hizi nchi.

Uhuru ungepatikana hata kama Nyerere asingekuwapo.
Inawezekana hili hulijui.

Abdul Sykes yeye mtu wake katika kuletwa TAA na kuunda TANU alikuwa
Chief Kidaha Makwaia.

Hamza Mwapachu yeye aliona Nyerere angefaa zaidi kuliko Chief Kidaha.

Ikiwa utapenda naweza nikakupa darsa ya historia hii ya Chief Kidaha na
Nyerere
na Abdul Sykes na Hamza Mwapachu katika historia ya uhuru wa
Tanganyika.

Vita baina ya India na Pakistan baada ya uhuru wa India 1947 ulikuwa na mafunzo
nakubwa kwa wazee wetu.

Ile ilikuwa ni vita baina ya Wahindu na Waislam na ilitokea kwa viongozi wa harakati
za uhuru wa India Mohamed Ali Jinah na Nehru kushindwa kuidhibiti ushawishi wa
dini zao katika siasa.

Hii ndiyo sababu Hamza Mwapachu akasema yale aliyosema.
 
Kila mwenye akili ajiulize kwa nini haukutajwa uyahudi au baniani.
Uislam umetajwa kwa sababu ulishiriki ktk harakati hizo, mbona kina Mzee Rupia wametajwa kwenye harakati, ndiyo historia hiyo. Kama kuna anaekerwa na ukweli huu ajaribu angalau kuandika "historia" kama alivyofanya yule alisoma kivukoni.
Kutokubalika kwa Uislam kwa asiyekuwa Muislam ndio akili hiyo.
Mohammed Said...endelea kuandika kila lililo la kweli, tunatambua kuwa hakuna mwandishi wa historia ya Uhuru wa nchi hii aliyefanikiwa kuwafikia na kuwahoji waasisi wa taifa hili kama wewe.
Fanya kazi mwalimu.
 
Duduwasha,
Huu ndiyo uzuri wa kuwa na historia ya kweli na kwa uwazi watu wakaisiki na
kuisoma kisha kika mtu akawa na mawazo yake huru katika tafsiri ya historia
hiyo.

Huyu kachero hakika sikumtaja na pale msibani nilieleza hili kuwa sitamtaja.
bahati mbaya hii haipo katika hiyo clip.

Lakini ikiwa utakuwa umefuatilia katika historia hii ya Abdul Sykes katika
juhudi zake za kuunda TANU, utakuwa umesoma safari ya Abdul kutoka
Dar es Salaam kwenda Nansio kuonana na Hamza Mwapachu ili apate
kauli yake kuhusu kumunuingiza Nyerere katika uongozi wa TAA 1953
na mwaka unaofuatia, 1954 waunde TANU.

Sasa ikiwa umesoma utaliona jina la huyu kachero wa Waingereza.
Umeniuliza kwa nini nimetaja Uislam.

Labda nami nijibu swali lako kwa kukuuliza swali pia kwa nini nisitaje Uislam.
Lakini kulikuwa na ''wind of change,'' yaani upepo wa uhuru ulikuwa unavuma
Afrika na hili Waingereza walilitambua na walijitayarisha kuziachia hizi nchi.

Uhuru ungepatikana hata kama Nyerere asingekuwapo.
Inawezekana hili hulijui.

Abdul Sykes yeye mtu wake katika kuletwa TAA na kuunda TANU alikuwa
Chief Kidaha Makwaia.

Hamza Mwapachu yeye aliona Nyerere angefaa zaidi kuliko Chief Kidaha.

Ikiwa utapenda naweza nikakupa darsa ya historia hii ya Chief Kidaha na
Nyerere
na Abdul Sykes na Hamza Mwapachu katika historia ya uhuru wa
Tanganyika.

Vita baina ya India na Pakistan baada ya uhuru wa India 1947 ulikuwa na mafunzo
nakubwa kwa wazee wetu.

Ile ilikuwa ni vita baina ya Wahindu na Waislam na ilitokea kwa viongozi wa harakati
za uhuru wa India Mohamed Ali Jinah na Nehru kushindwa kuidhibiti ushawishi wa
dini zao katika siasa.

Hii ndiyo sababu Hamza Mwapachu akasema yale aliyosema.

Chief Kidaha Makwaia nilimfahamu miaka mingi baadae, 1980s nikiwa shule ya sekondari. Baada ya siasa kumwendea kombo alihamia katika masuala ya dini, alikuwa anafundisha somo la dini kwa wakatoliki shuleni kwetu, na mara zote alikwepa kuzungumza siasa. Jina lake kwa ukamilifu ni Paul David Kidaha Makwaia.
Mwalimu wa dini ya kiislamu alikuwa Ahmed Olotu, huyu ambaye siku hizi anacheza sinema za kibongo kwa jina la "Mzee Chillo".
 
Ralph...
Kwangu mimi Chief Kidaha ni baba ya rafiki yangu wa utotoni Edward Makwaia
ambae tulisoma darasa moja St. Joseph's Convent na ilikuwa kupitia Edward ambae tukipenda kumwita Ted ndipo nilipata bahati ya kukutana na mzee wetu huyu.

Huu ulikuwa mwaka wa 1967 au 1968.
Wakati huo akiishi Nairobi.

Ted ndiye Chief wa Siha hivi sasa baada ya kifo cha baba yake.

Katika utafiti wangu wa kuandika maisha ya Abdu Sykes nilikutana na Chief Kidaha
katika Nyaraka za Sykes kupitia barua aliyoandika Dr. Wilbard Mwanjisi mwaka wa
1950 akimsifia Chief Kidawa kuwa ni mwanasiasi makini kwa michango yake ndani ya
Legco.
 
Leo katika maziko ya Mzee Kitwana Kondo niliombwa nizungumze maneno machache kuhusu mzee wangu huyu. Ukweli ni kuwa nilikuwa nimeshtukizwa kwani sikutaarifiwa kabla kuwa niko katika orodha ya wazungumzaji. Lakini mtu ukitumwa na waliokupita makamo huna khiyari ila kutii. Ndipo nilipozungumza yale yaliyopitika baina yangu na Mzee Kondo tarehe 12 Septemba 2012 nilipokwenda kufanya mahojiano na yeye kwa ajili ya kipindi changu cha TV Imaan, ‘’Walioacha Alama Katika Historia.’’ Siku ile wakati vijana wa picha na sauti walipokuwa wanajitayarisha kurekodi ghafla Mzee Kondo akaniita akanambia nikakae pembeni yake ana jambo anataka kuniambia. Ndipo akanieleza haya ambayo ninayeleza hapo chini bila kutaja jina la mpelelezi yule, jina ambalo Mzee Kondo alinitajia na akaniambia nisieleze historia hii hadi yeye atakapokuwa ameondoka duniani.

Mohamed Said: KITWANA KONDO ALIPOMFICHUA MPELELEZI WA WAINGEREZA NDANI YA TANU 1
Mohamed Said: KITWANA KONDO ALIPOMFICHUA MPEPELEZI WA WAINGEREZA NDANI YA TANU 1950s 2

Ndo nani huyo?
 
B207

Ted ndiye Chief wa Siha hivi sasa baada ya kifo cha baba yake.
Kaka mo'hd Ted kama anarithi uchifu hawezi kuwa chifu wa siha kwani babake alikuwa chifu huko shinyanga. Asante kwa shule adhimu unayo shusha hapa jf.
 
Back
Top Bottom