Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 20,912
- 30,253
Katika maziko ya Mzee Kitwana Kondo niliombwa nizungumze.
Sikiliza video hii kuna historia muhimu sana kueleza kuundwa kwa TANU.
Nilizungumza kuhusu kikao cha watu watatu nyumbani kwa Hamza Mwapachu, wengine wakiwa Abdul Sykes na Ali Mwinyi Tambwe agenda ikiwa namna ya kumuingiza Julius Nyerere katika uongozi wa TAA katika uchaguzi uliokuwa mbele yao April 1953 na baada ya hapo 1954 TANU iundwe.
Nazungumza mbele ya viongozi wa CCM na serikali waliokuwepo hapo mazikoni.
Wote waliokuwapo pale walipigwa na mshangao mkubwa sana na kisa nilichoeleza.
Naamini kikubwa kilichowashangazwa wengi pale mazikoni ni ile kusema kuwa Abdul Sykes na Hamza Mwapachu wakifanya mipango ya kuunda TANU.
Waingereza walikuwa wanaijua mpango hii na walichuua hatua madhubuti kuzuia TANU isiundwe.
Waliwatumia makachero kupata taarifa zote.
Haujafanywa utafiti wa kuwajua makachero wa Special Branch ndani ya TANU wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika.
Kachero niliyekutananae wakati wa utafiti wa kitabu cha Abdul Sykes ni mmoja tu, Alexander Tobias na huyu jina lake nilitajiwa na Mzee Germano Pacha nilipokwenda Tabora kufanyanae mahojiano.
Hassan Upeka ambae yeye mwenyewe alikuwa kachero wa TANU kuanzia mwaka wa 1956 na baada ya uhuru akawa Usalama wa Taifa katika mazungumzo niliyofanyanae miaka ya 1980 alinisisitizia sana nizungumze na Mzee Germano Pacha.
Mzee Pacha alinifahamisha kuwa agenda ya kwanza ya mkutano wa TAA wa 1954 uliounda TANU ilikuwa kuthibitisha kufukuzwa kazi kwa Alexander Tobias kwa kosa la kuwapa Specal Branch mafaili ya TAA.
Alexander Tobias aliajiriwa kama Executive Secretary wa TANU mwaka wa 1951 au 1952 baada ya Abdul Sykes kurejea Dar es Salaam kutoka Nansio Ukerewe.
Abdul Sykes alikwenda Nansio kushauriana na Hamza Mwapachu kuhusu matatizo yaliyokuwa yanaikabili TAA HQ baada karibu vongozi wake wote kuondolewa Dar es Salaam na kupelekwa majimboni kufuatia mapendekezo ya katiba yaliyowasilishwa TAA kwa Gavana Twining ambayo yaliwataka Waingereza waruhusu uchaguzi kuchagua Wajumbe wa LEGCO na baada ya miaka 13 waipe Tanganyika uhuru wake.
President wa TAA Dr. Vedasto Kyaruzi akahamishiwa Kingolwira.
Waingereza walighadhibishwa sana na mapendekezo haya na wakaamua kuwaondoa viongozi wa TAA Dar es Salaam ili wapate kupumua.
Hamza Mwapachu akapelekwa kisiwani Nansio.
Hamza Mwapachu akamshauri Abdul Sykes ambae alikuwa Act. President na Secretary kuwa TAA HQ iajiri Executive Secretary.
Hivi ndivyo Alexander Tobias alivyokuja kuajiriwa na TAA.
Alexander Tobias