Kituo cha usalama kinachomlinda Rais Mstaafu wa Nigeria chashambuliwa na askari mmoja ameuawa

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,501
9,280
Kituo cha usalama kilichoko karibu na nyumba ya rais wa zamani wa Nigeria Bw. Goodluck Jonathan katika jimbo la Bayelsa, nchini Nigeria kimeshambuliwa na watu wenye silaha wasiojulikana na askari mmoja ameuawa.

Msaidizi wa Bw. Jonathan anayeshughulikia mambo ya habari amesema watu hao wenye silaha walifanya shambulizi kwa kutumia boti tano za injini dhidi ya kituo cha usalama kinacholinda usalama wa nyumba ya rais huyo wa zamani.

Habari pia zinasema katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres ameeleza wasiwasi mkubwa kuhusu ripoti za kuuawa kwa raia na kutekwa nyara na makundi ya kisilaha kaskazini mwa jimbo la Borno, Nigeria.

Bw. Guterres ametoa salamu za rambirambi kwa familia za watu waliouawa, huku akisisitiza kuwa Umoja huo uko pamoja na watu na serikali ya Nigeria.
 
Back
Top Bottom