Kituo cha Sheria chataka adhabu ya kifo ifutwe

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
pic+haki.jpg

Ikiwa dunia leo inaadhimisha siku ya kupinga adhabu ya kifo, Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimeitaka Serikali kuifuta adhabu hiyo.

Pia, Serikali na mamlaka husika zimetakiwa kufuta vipengele na sheria zinazoelekeza adhabu hiyo.

Kituo hicho kimeshauri mamlaka husika kuweka adhabu mbadala wa kifungo cha maisha ili kuthamini uhai ambao ni haki ya kila binadamu.

Akizungumza leo Jumanne, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Ana Henga amesema adhabu ya kifo inaondoa uwezekano wa mkosaji kujirekebisha na badala yake ni kuendeleza ukatili na kuondoa ubinadamu.

Henga amesema adhabu ya kifo inavunja misingi ya tamko la kimataifa la haki za binadamu la mwaka 1948 ambalo linasema kila mtu ana haki ya kuishi.

Amesema Tanzania inapaswa kujifunza kutoka kwa mataifa mengine duniani ambayo hayatekelezi adhabu ya kifo na badala yake kutoa adhabu mbadala kama vile kifungo cha maisha na kazi ngumu kwa watuhumiwa wa mauaji ili kulinda haki ya msingi ya kuishi.

Henga amesema harakati za kupinga adhabu ya kifo hazimaanishi kuwa ni kutetea uhalifu, hasa mauaji ila ukweli ni kwamba, hakuna ushahidi kuwa uwepo wa adhabu hiyo unaweza kupunguza uhalifu badala yake umekuwa ukiongezeka.

Tanzania ni miongoni mwa nchi chache duniani kama vile China, Korea Kaskazini na Marekani ambazo zinaruhusu na kutekeleza adhabu ya kifo katika sheria zake.

Sheria ya Kanuni za Adhabu, Sura ya 16 ya Sheria za Tanzania, kifungu cha 197 kinaeleza mtu yeyote anayepatikana na hatia ya kuua atahukumiwa adhabu ya kifo.

Henga ameitaka Serikali itekeleze pendekezo la mpango wa kujitathmini wa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa wa mwaka 2016 kwa kuridhia mkataba wa nyongeza wa haki za kiraia na kisiasa na kutangaza kuwa haitekelezi adhabu hiyo.

Amesema kwa mujibu wa ripoti ya haki za binadamu ya mwaka 2016 takwimu zinaonyesha hadi mwaka 2015 kulikuwa na watu 472 waliohukumiwa kunyongwa kati yao wanaume wakiwa 452 na wanawake 20.

Pia, kati ya hao wanaosubiri kunyongwa ni 228, huku 244 wakisubiri uamuzi wa rufaa zao.

"Hii ni adhabu ya kibaguzi maana mara nyingi wanaopatikana na hatia na kupewa adhabu ni masikini wasioweza kuwa na uwakilishi na ushauri wa kisheria," amesema Henga.

- Mwananchi
 
Honestly kunawatu wanastahili adhabu ya kifo, mfano kama yule kijana aliye baka mtoto wa dadayake na kisha kumuua hivi wanadhani ni adhabu gani itamfaa ...
 
Kila kitu kina mtu wake so Adhabu ya kifo ina watu wake, kuna watu wana mabaya sana mpaka shetani anaogopa hao wapewe adhabu gani?

Binafsi naona sheria hiyo ibaki hivyo hivyo iendeshwe kwa maono ya Rais aliepo madarakani.
 
Honestly kunawatu wanastahili adhabu ya kifo, mfano kama yule kijana aliye baka mtoto wa dadayake na kisha kumuua hivi wanadhani ni adhabu gani itamfaa ...
Kuua sio adhabu ni kulipiza kisasi .
 
Mimi nadhani wangeanza kupigania sheria nyingine nyingi kandamizi kama vile kuweka watu ndani halafu ndio unafanya uchunguzi! Watu wanaanza kuadhibiwa kabda hata ya kukutwa na hatia na mahakama. Kuna watu wamekaa ndani miaka mitano huku ikiambiwa uchunguzi bado unaendelea! Mwisho wa siku wanashinda kesi kwa kukosekana kwa ushahidi.

Hii ni dhulma kubwa sana ya kisheria na ni kama vile waendesha mashtaka wana enjoy sana kipengele cha kupinga dhamana kwa washtakiwa. Sina hakika kama nguvu ya kupinga dhamana haipingiki au nayo ni discretion ya hakimu lakini yoyote alie na powers hizo kwenye mfumo wetu wa sheria amekua aka abuse.
Kuna nchi kama South Africa hata kosa la mauaji lina dhamana. Maoni yangu kwa hapa kwetu makosa yote ambayo ni non violent yangekua na dhamana hata kama ni kwa masharti magumu ili kuepuka kutoka adhabu ya vifungo kwa watu kabda hawajapatikana na kosa mahakamani na taasisi za kutetea haki za binadamu wangeanza na hili ambalo linaathiri watu wengi
 
Ikiwa dunia leo inaadhimisha siku ya kupinga adhabu ya kifo, Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimeitaka Serikali kuifuta adhabu hiyo.

Pia, Serikali na mamlaka husika zimetakiwa kufuta vipengele na sheria zinazoelekeza adhabu hiyo.

Kituo hicho kimeshauri mamlaka husika kuweka adhabu mbadala wa kifungo cha maisha ili kuthamini uhai ambao ni haki ya kila binadamu.

Akizungumza leo Jumanne, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Ana Henga amesema adhabu ya kifo inaondoa uwezekano wa mkosaji kujirekebisha na badala yake ni kuendeleza ukatili na kuondoa ubinadamu.

Henga amesema adhabu ya kifo inavunja misingi ya tamko la kimataifa la haki za binadamu la mwaka 1948 ambalo linasema kila mtu ana haki ya kuishi.

Amesema Tanzania inapaswa kujifunza kutoka kwa mataifa mengine duniani ambayo hayatekelezi adhabu ya kifo na badala yake kutoa adhabu mbadala kama vile kifungo cha maisha na kazi ngumu kwa watuhumiwa wa mauaji ili kulinda haki ya msingi ya kuishi.

Henga amesema harakati za kupinga adhabu ya kifo hazimaanishi kuwa ni kutetea uhalifu, hasa mauaji ila ukweli ni kwamba, hakuna ushahidi kuwa uwepo wa adhabu hiyo unaweza kupunguza uhalifu badala yake umekuwa ukiongezeka.

Tanzania ni miongoni mwa nchi chache duniani kama vile China, Korea Kaskazini na Marekani ambazo zinaruhusu na kutekeleza adhabu ya kifo katika sheria zake.

Sheria ya Kanuni za Adhabu, Sura ya 16 ya Sheria za Tanzania, kifungu cha 197 kinaeleza mtu yeyote anayepatikana na hatia ya kuua atahukumiwa adhabu ya kifo.

Henga ameitaka Serikali itekeleze pendekezo la mpango wa kujitathmini wa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa wa mwaka 2016 kwa kuridhia mkataba wa nyongeza wa haki za kiraia na kisiasa na kutangaza kuwa haitekelezi adhabu hiyo.

Amesema kwa mujibu wa ripoti ya haki za binadamu ya mwaka 2016 takwimu zinaonyesha hadi mwaka 2015 kulikuwa na watu 472 waliohukumiwa kunyongwa kati yao wanaume wakiwa 452 na wanawake 20.

Pia, kati ya hao wanaosubiri kunyongwa ni 228, huku 244 wakisubiri uamuzi wa rufaa zao.

"Hii ni adhabu ya kibaguzi maana mara nyingi wanaopatikana na hatia na kupewa adhabu ni masikini wasioweza kuwa na uwakilishi na ushauri wa kisheria," amesema Henga.

- Mwananchi
Kabla ya kufuta adhabu ya kifo kwanza wananchi tuache kuwaua vibaka, maanake tusijifanye sie tuna huruma sana kwa sababu hayajatukuta hivi kweli mtu aliyemnyang'anya mama mtoto Albino mgongoni ameenda kumcharanga na unakuta baadhi ya viungo vyake vimetupwa sehemu leo hii uishi nae nyumba moja utajihisi uko salama kabisa!
 
Huyo kaimu mkurugenzi naomba mzazi wake na watoto wake walawitiwe kisha wauliwe

Halafu wahalifu wakamatwe halafu abaki na msimamo huo hapo sawa
90bdce94762579ab0a5d545c7b229043.jpg

5c52342e00f4f1b99fc6b0c0b425936b.jpg
 
Hata wanyama wa porini wakiuwa huwa wanatafutwa ili wauawe, wauaji hawahitaji kupewa muda wa kujutia ili tubaki salama waondoke tu! Kuna wahalifu wengi wenye kustahili nafasi ya kujutia lakini si wauaji hii ni ngazi juu sana la muhimu adhabu itekelezwe
 
Back
Top Bottom