Kituo cha polisi UDSM na wizi wa magari

DASA

JF-Expert Member
Jan 6, 2011
1,031
301
Kwa asilimia kubwa wizi wa magari maeneo ya UDSM na maeneo jirani ya hapo unafanywa na polisi wa kituo hiki kama sio wenyewe binafsi ni kwa kushirikiana na watu wanaowajua wao.

Dada mmoja kwa jina la Jackline komba aliibiwa gari aina ya suzuki swift maeneo ya Engineering january 16 ikiwa imepita takriban kama wiki moja tangu dada mwingine aibiwe gari aina ya Escudo maeneo hayo hayo. Huyu dada alipotoa taarifa kituo cha polisi baada ya muda polisi hao hao walikuwa wanampigia simu kwamba gari lake wanalo na ili alipate awapelekee kiasi cha shilingi milioni 3, lakini alipowaomba kwamba ana 2.5 walimkubalia azipeleke. Huyu Dada alishtuka akaenda kutoa taarifa Kituo cha urafiki na ndipo walipotengeneza mtego na kuwakamata askari hao kwenye baa maeneo ya makaburini. Afande aliyekamatwa anaitwa afande Lufefe na mwingine kwa jina la Davis kutoka makao makuu.

Hichi kituo cha polisi watu wamekosa imani nacho sababu wanashirikiana na hao majambazi kama sio kuiba wenyewe.

Source: Nipashe la jana.
 
Huu ni upuuzi zaidi ya ufilauni haiwezekan kabisa watu wa usalama tunao wategemea ndiyo wanaleta usee.

Inabidi kova alete majibu ya kienterejinsia juu ya hili
 
da hi noma juzi tumesikia polisi wa2 wameshiliki kuiba msasani, sasa usalama wa watu na mali zao unalindwa na wezi kweli!?
 
Tukigoma na hilo wanatufukuza, unakumbuka yule mmalawi aliyekuwa anapola laptop,simu na pesa hapa hall 6, 7 na pale chepo? Nani alikuwa anamsupport kama si auxilliary? Usikute hata mkandala anahusika hapo.
 
Kwa asilimia kubwa wizi wa magari maeneo ya UDSM na maeneo jirani ya hapo unafanywa na polisi wa kituo hiki kama sio wenyewe binafsi ni kwa kushirikiana na watu wanaowajua wao.

Dada mmoja kwa jina la Jackline komba aliibiwa gari aina ya suzuki swift maeneo ya Engineering january 16 ikiwa imepita takriban kama wiki moja tangu dada mwingine aibiwe gari aina ya Escudo maeneo hayo hayo. Huyu dada alipotoa taarifa kituo cha polisi baada ya muda polisi hao hao walikuwa wanampigia simu kwamba gari lake wanalo na ili alipate awapelekee kiasi cha shilingi milioni 3, lakini alipowaomba kwamba ana 2.5 walimkubalia azipeleke. Huyu Dada alishtuka akaenda kutoa taarifa Kituo cha urafiki na ndipo walipotengeneza mtego na kuwakamata askari hao kwenye baa maeneo ya makaburini. Afande aliyekamatwa anaitwa afande Lufefe na mwingine kwa jina la Davis kutoka makao makuu.

Hichi kituo cha polisi watu wamekosa imani nacho sababu wanashirikiana na hao majambazi kama sio kuiba wenyewe.

Source: Nipashe la jana.

Hawa si ni mabingwa wa kukanusha sasa na hili nalo sijui watasemaje?
 
Si wanaona wao wametoswa kimaslahi, wanaamua kutafuta wenyewe maslahi?
Si mnawaona maaskari wanavyo simamisha magari na kuanza kupotezea watu muda wao kwa kuhoji ujinga? eti fire extinguisher iko wapi,/ Kama gari ikiungua si kuna insurance? we askari inakuuma vipi kuuliza fire extinguisher? Tumewaendekeza ma askari, mpaka umekuwa mzigo kwetu.
 
Hongera sana mleta mada!!!
Sio tu kwamba kituo cha polisi udsm kimelipaka jeshi la polisi matope, ukweli ni kwamba kimechafua jina la udsm ile mbaya. Maana juzi kati nilikuwa sehemu ya kilaji nikasikia meza ya pili wakilalamikia tatizo hilo kwa mapana sana. Ukweli ni kwamba hawa jamaa wa kituo cha udsm wameshakubuhu kwa wizi na rushwa!

Tunaomba wanafunzi mtuunge mkono kuwang'oa hawa vibaka ndani ya chuo chetu heshima irudi!!!!!
 
Hebu wekeni wazi, ni askari gani hao wanaotuhumiwa, waajiriwa wa UDSM (Auxilliary Police) au askari wa wizara ya mambo ya ndani wa Shamsi Vuai Nahodha? Pale pana polisi mbili
 
Waliokamatwa ni Askari wa serikali wanaokula kodi zetu. lakini vile vile wanashirikiana na hao hao auxiliary. hakuna mwema.
 
Duh! usishangae jinsi tulivyokuwa na watu mambumbumbu kwenye serikali yetu hao askari hawatachukuliwa hatua zaidi, na usikute wapo mtaani siku nyingi. Ingekuwa china wameshanyongwa hao siku nyingi.
 
Auxiliary police nao wanahusika,kama kuna lile bonge lenye pua bapa lina kiherehere kweli!
 
Polisi ndio majambazi wenyewe
Kwa asilimia kubwa wizi wa magari maeneo ya UDSM na maeneo jirani ya hapo unafanywa na polisi wa kituo hiki kama sio wenyewe binafsi ni kwa kushirikiana na watu wanaowajua wao.

Dada mmoja kwa jina la Jackline komba aliibiwa gari aina ya suzuki swift maeneo ya Engineering january 16 ikiwa imepita takriban kama wiki moja tangu dada mwingine aibiwe gari aina ya Escudo maeneo hayo hayo. Huyu dada alipotoa taarifa kituo cha polisi baada ya muda polisi hao hao walikuwa wanampigia simu kwamba gari lake wanalo na ili alipate awapelekee kiasi cha shilingi milioni 3, lakini alipowaomba kwamba ana 2.5 walimkubalia azipeleke. Huyu Dada alishtuka akaenda kutoa taarifa Kituo cha urafiki na ndipo walipotengeneza mtego na kuwakamata askari hao kwenye baa maeneo ya makaburini. Afande aliyekamatwa anaitwa afande Lufefe na mwingine kwa jina la Davis kutoka makao makuu.

Hichi kituo cha polisi watu wamekosa imani nacho sababu wanashirikiana na hao majambazi kama sio kuiba wenyewe.

Source: Nipashe la jana.
 
nasikia dodoma kuna wizi mkali wa mita za maji, labda polisi pia wanahusika kama hali ndo hii. Jamaa yangu yuko duwasa anasema zimeishaibiwa mita zaidi ya laki tatu.
 
Tatizo kubwa ambalo limejitokeza,serikali haitoi pesa za upelelezi ya kutosha za kumuwezesha askari mpelelezi kuendesha upelelezi wa kesi kubwakubwa kama hizo za wizi wa magari,kitu kilichotokea ni kuwa wale soldier waliendesha upelelezi na kumpata yule mwizi kwa kutumia simu ya mkononi kupitia kwa mtu mwingine.wale wapelelezi ilibidi waingie kwa mlango wa kulinunua lile gari kwa milion 2,huku wakiwasiliana kwa simu bila ya kuonana.wale wapelelezi walikuwa hawana pesa,ndio hapo tatizo lilipoanzia.
 
Back
Top Bottom