Fall Army Worm
JF-Expert Member
- Jan 8, 2015
- 19,322
- 14,244
Wakuu natumai mnaendelea vizuri na kusukuma gurudumu la maendeleo ya Taifa.
Kama kichwa kinavyoeleza,Kituo cha Polisi cha Mlangali,Kata ya Mlangali,Katika Wilaya ya Ludewa iliyoko mkoa wa Njombe,pana nuka rushwa.Iko hivi hawa jamaa wakimkamata raia na kosa lolote lile hata km ni dogo namna gani watamuweka ndani halafu kutoka ni hadi utoe pesa ambayo haina risiti.Najua mtaniuliza kwanini hujapeleka kunako husika ??,Je,JF itaweza kukusaidia kutatua changamoto hiyo?
Kama kuna hoja ya namna hiyo ni kwamba hadi wilayani wanafahamu tatizo hilo,OCD anajua lkn hamna utatuzi,Naleta hapa JF ili kuuhabarisha umma wa Watanzania ujue kuwa kuna Askari wanaotumia vibaya nafasi zao kunyanyasa raia na kujipatia pesa kwa njia ya rushwa.Hebu niende kwenye visa na mikasa ya hao Polisi.
Kuna matukio kadhaa yanawapata ndugu zangu na watu wengine ambapo kwa kweli yanatia simanzi.
TUKIO LA KWANZA.
Kuna jamaa mmoja,ambaye si ndugu yangu,ila nilimfahamu kwa vile alikuwa ni Fundi simu,hivyo tulifahamiana kupitia kunitengezea simu,huyu alipelekewa simu na mteja ili aifrash,kumbe simu ile ilikuwa imeokotwa,yule aliyeipoteza alipoanza kufuatilia trend ya wahusika wakamkata na yule fundi simu,kutoka wakamdai 50,000/=,yule akawauliza Polisi kosa lake ni lipi?,maana ile ni ofisi na inajulikana na Serikali kuwa yeye ni Fundi simu na hata Polisi wenyewe huwa wanaenda kufrash hapo.Ile ishu aliingilia kati Afisa tarafa akaamuru yule jamaa arudishiwe pesa yake.
TUKIO LA PILI
Juzi kuna jamaa wamweka ndani kwa kesi isiyo na kichwa wala miguu,kiasi kwamba Polisi wenyewe wanatofautiana,wapo waliosema hapa hamna kesi na wengine kuna kesi, kikubwa walikuwa wakidai pesa ,sasa jamaa yule alikuwa na pesa kidogo yaani Polisi wale hawana hata mshipa wa aibu,walisikika wakisema pesa ni kidogo mno tutagawanaje?,tupo wengi.Jamaa akampigia simu OCD,wakapelekwa Wilayani huko wakakutanishwa na OC-CID na yeye hali ikawa hivyo hivyo,anasema jamaa wameniletea dili kwa hiyo lazima utoe pesa ya kutosha kuwagawia na wenzangu,na kwamba asipofanya hivyo basi atamfunga miaka saba jela au kumtengenezea kosa kubwa zaidi,Ili bidi jamaa zimtoke.Kwa hiyo Askari wale wote ni kitu kimoja,kuanzia wale wakubwa hadi wadogo.Lakini kitu kinachostaabisha zaidi ni jinsi hawa Polisi wanavyoweza kuomba rushwa waziwazi na kisha kugawana fedha hizo waziwazi bila woga,hadi mtoto mdogo anajua kabisa jamaa wanakula rushwa na wanagawana.
Hayo ni matukio mawili niliyoyasimulia kimuhtasari tu.Yapo mengi,ambayo nikisema niyaeleze hapa yote nitajaza Seva.
NINI NAFIKIRIA KUKIFANYA??
Kwa kuwa wananchi wengi wa Mlangali ni waoga,wanawaogopa wale Polisi,Mimi nataka kujitoa mhanga,Siogopi chochote wala yeyote Ila Mungu tu mwenye uwezo na mamlaka juu ya pumzi yangu,yeye awezaye kuua mwili na Roho;Nataka kuwa mkombozi kwao,Maana hakuna kitu ninakichukia sana ktk maisha km dhuluma,nasema hivi najitoa mhanga sina cha kupoteza,Ninasubiri waingie kwenye 18 zangu halafu wanidai rushwa, mimi nitakubali halafu nitawapigia TAKUKURU makao makuu,maana sina Imani na TAKUKURU ya Ludewa.Halafu nione je na Makao Makuu nao watapuuzia?,wakipuuza nitatafuta kila namna niende kwa Rais.Kwasababu Ikulu sio mbinguni,ni duniani na ipo kwaajili yetu.Huo ndio mpango wangu,nina hasira za kufa mtu,siwezi kuvumilia uonevu huu.Najua ktk kufanya hivyo kuna watu watapata madhara matharani wategemezi wa wahusika lkn sina namna.
WITO WANGU KWA JESHI LA POLISI
Askari Polisi msitumie vibaya madaraka yenu,hiyo kazi ni dhamana tu.Vitendo vyenu vya unyanyasaji ndivyo vinavyofanya raia tuwachukie ninyi.Mfano mmoja kule Ngara Mwanajeshi alipata ajari ya gari ambapo raia waliokuwa karibu wangemnusuru mapema angeweza kuokoa maisha, lkn jamaa walipochungulia kwenye gari na kuona ni mjeda,walisema acha afe,hatumsaidii Kwasababu ya uoenezi waliokuwa wanawafanyia.Ninyi sio miungu watu.Kutokana na dhuluma mnazozifanya na manung'uniko ya hao wanaodhulumiwa wengi wenu mkistaafu huwa mnakuwa na hali mbaya,nina Ushuhuda huo,wa Askari mmoja aliyekuwa OCD baada ya kustaafu maisha yalimwendea kombo sana hadi sasa ukimwona huwezi amini maana hadi funza wameota miguuni.Binafsi siwaombei mabaya lkn acheni kunyanyasa watu wanyonge,hizo fedha za dhuluma hazitawafikisha popote.Ombi langu kwa IGP Sirro,ni kwamba juhudi ulizozionyesha ktk kudhibiti wahalifu nchini,zionyeshe pia ktk kudhibiti nidhamu ya Askari wako nchini,Namsifu sana Mwema aliyeanzisha Polisi jamii ili kuondoa uhasama kati ya Polisi na mwananchi.
Maisha sasa hivi magumu sana,fikiri ikiwa wewe mwenye mshahara unaona hali ni ngumu,vipi kwa yule mkulima hokhe!hakhe!,hali ikoje?,halafu bado unambambikizia kesi ili akupe rushwa.Kweli wananchi wapo sahihi kutomsaidia Askari hata km anakata roho.Mjue pia mnafanya Wananchi waichukie Serikali Kwasababu ya huo mchezo wenu mchafu.
Ni matumaini yangu,kuwa nimeeleweka.Nasisitiza siogopi chochote,nimetoka mavumbini,nitarudi Mavumbini,na Kila nafsi itaonja mauti.
ALAMSIKI