Kituo cha polisi Manzese Tip Top kimechomwa moto

Feedback

JF-Expert Member
Mar 14, 2011
7,988
4,507
Kuna habari vurugu zimetokea Manzese Tip Top kati ya vijana na polisi wakigombea maiti na inasemekana kituo cha polisi kimechomwa moto.
Tunaomba mlio Manzese mtupe undani wa tukio lenyewe.

Habari nilizozipata sasa hivi ni kuwa polisi wanatumia mabomu ya machozi na risasi za moto kutawanya vijana wenye hasira tuendelee kufahamishana.
 
Da! Hii nchi sasa sijui tunaelekea wapi. Asubuhi tumesikia Mwanza wamachinga wameuawa na polisi baada ya kufyatuliwa risasi za moto, sa hizi tena Manzese. Na huu ni mfululizo tu wa mauaji. Tunakoelekea...!?
 
Hatuna polisi tuna vibaka waliopewa uniform na silaha, ukibisha nita-prove, mmoja juzi kagonga raia pale Riverside kwenye Zebra tena gari yenyewe ya polisi ilikuwa kwenye wrong-side, yaani alivyoona kuna foleni kubwa akaamua (kwakua yeye ni askari) apite the other side, mshkaji anakatisha zebra hana hili wala lile anashtukiza gari hili hapa...........wauwaji wakubwa hawa..shen............zao
 
Wale walinzi wa mkulu wasioonekana hawajapata mlo wao siku nyingi baada ya gwiji wao kufa sasa wanajitafutia wenyewe chakula ndiyo maana kila leo ajali mara polisi wametwanga watu risasi nk.
 
WaTanganyika mtamalizana wenyewe kwa wenyewe. tafadhali eleweni kuwa nchi ni yenu wote.
 
Oyaaa!ina maana huko manzese hakuna member wa JF,aliweke sawa(athibitishe)hili...maana tayari tunajadili ishu as if imethibitika!
 
Wale walinzi wa mkulu wasioonekana hawajapata mlo wao siku nyingi baada ya gwiji wao kufa sasa wanajitafutia wenyewe chakula ndiyo maana kila leo ajali mara polisi wametwanga watu risasi nk.
Haa kumbe, nilikuwa sijui kama mkulu anao walinzi wasioonekana.
 
Wananchi wavamia kituo cha polisi mwizi wa pikipiki
Tuesday, 05 July 2011 20:52
Lilian Lugakingira, Bukoba
POLISI mkoani Kagera, imefanikiwa kuokoa maisha ya John Kaitaba (35), anayetuhumiwa kumhifadhi mwizi wa pikipiki ambaye alivamiwa na waendesha pikipiki na kuanza kumpa kipigo.

Hata hivyo, baada ya polisi kumwokoa mtu huyo na kumpakia kwenye gari kumpeleka kituoni, mamia ya waendesha pikipiki na wananchi, walivamia kituo wakitaka wamwachie ili wamwadhibu.

“Tumechoka kuuawa, wanapokuja kutuibia pikipiki kama sio kuuawa wanaachiwa ulemavu wa kudumu, mlete huyo mtu tumshughulikie,” walisikika wakipaza sauti waendesha pikipiki hao wakiwa Kituo Kikuu cha Polisi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Henry Salewi, alilazimika kutumia njia za kidiplomasia kwa kuzungumza na hatimaye walikubali kuondoka bila kusababisha madhara.

Baada ya kutoka kituo cha polisi walielekea nyumbani kwa mtuhumiwa na kuchoma moto nyumba na maduka yake mawili.Hasira za waendesha pikipiki hao, zinatokana na matukio ya kuwateka na kuwaua kisha kuwanyang’anya vyombo vyao.

Tukio la hivi karibuni takriban mwezi mmoja uliopita, ni la mwendesha pikipiki aliyekodiwa na baadaye kupatikana ameuawa kwa kuchinjwa maeneo ya Bugabo, Bukoba vijijini na kuondoka na pikipiki.

Kutokana na tukio hilo, waendesha pikipiki walivamia nyumbani kwa mtu aliyemkodi wakitaka kumuua, lakini hawakumkuta na kuamua kufyeka migomba, kuchoma moto nyumba na kuharibu mali nyingine.
Kamanda Salewi alisema Julai Mosi, mwaka huu, Twaha Suleiman, aliibiwa pikipiki nyumbani kwake na kutoa taarifa polisi, mtu mmoja alikamatwa na kufikishwa mahakamani.

Salewi alisema wakati uchunguzi ukiendelea, juzi polisi walipata taarifa kuwa mtu anayedaiwa kumpangisha mtu anayehofiwa kuiba pikipiki, amekamatwa na waendesha pikipiki anapigwa, polisi walikwenda kumwokoa na baadaye zikatolewa taarifa za nyumba yake kuchomwa moto.
watu wamechoka
 
WaTanganyika mtamalizana wenyewe kwa wenyewe. tafadhali eleweni kuwa nchi ni yenu wote.
Hatumalizani, hizo ni tafrani zitazozaa maendeleo. Fikiria zanzibar ilikotokea kuanzia mapinduzi - kumwaga damu za wafuasi wa cuf hadi sasa muafaka.
Hata Tanganyika lazima ipite njia hiyohiyo; tafrani hizo zinasabaisha watu kuheshimiana.
Sijui kama anafuatilia bunge: wakati wa kujadili misamaha ya kodi wapinzani walikataa sheria hiyo lakini ccm wakawabeza sana; ilipokuja kujadiriwa bajeti ya waziri mkuu wabunge wa ccm wakasema kama kuna kitu kitaua nchi hii ni misamaha ya kodi. Sasa mtu kam huyo kwa nini usimzabe kibao!
 
Moja kwa moja hii mibonge ya CCM ni mi 'ngumbalu' sasa kwa stahili hiyo mbona na yenyewe imeona kuwa ni balaa, na pindi ilikuwa inazomeaa .............................. hovyooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooo!!!!!!!!!!
 
Ni kweli Tanganyika tulikuwa tumepungukiwa na heshima na hasa masultani wa magogoni,ngoja sahvi tutiane bakora kwanza ili adabu irudi...she...zi taipu
 
Back
Top Bottom