Kituo cha polisi Geita chavamiwa, Askari wauawa!

Kwa nini post zisilindwe kama kambi za jeshi? Ushauri kwako igp mangu,kila post ilindwe na askari wawili kama bank,hata raia wakija pata huduma wasachiwe hata kwa macho tu,kwani kwenye kambi za jeshi hamuoni?
 
Muda si mlefu utawasikia polisi wanatuuzia mbuzi kwenye gunia ili kuficha udhaifu wao,watatoa siraha kwenye ghara na kuwabambikizia watu,utamsikia mkuu wa policcm tumeyakamata majambazi yaliyoua asikari pamoja na siraha zote tumezipata,subili mtaona cinema ndo inaanza.
 
KATI YA ASKARI NA MAJAMBAZI YUPI SHUJAA?Wakuu habari za leo Jumamosi?!

Nimepokea taarifa kutoka Mkoani Geita kwamba usiku wa leo majira ya saa 9 watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wamevamia kituo cha polisi cha wilaya ya Bukombe na kuua askari sita waliokuwa zamu na kuvunja ghala la silaha na kuzichukua.

Nitaendelea kutoa taarifa kadri zitakavyokuwa zinanifikia.

Updates...

Askari waliokufa ni wawili mmoja hali yake mbaya sana...wengine watatu wamejeruhiwa.

MoreUpdates.

Askari waliouawa ni Dastan Kimathi na Hulia Mwandiga.

Waliojeruhiwa ni Mohamed Hassan Kilomo (25) ambaye amejeruhiwa kwa risasi kifuani na kuvunjwa mguu wa kulia.

Mwingine ni David Ngupama Mwalugelwa (44) ambaye amepigwa bomu kichwani na usoni na kumharibu vibaya.

Majambazi wamepora Bundiki 10 aina ya SMG pamoja na mabomu.

Inadaiwa walikuwa majambazi wapatao watano.

Muda si mrefu RPC Konyo atazungumza na waandishi wa habari.
 
Wamepora silaha my God bless us wakamatwe na Silaha zote zipatikane majambazi yatateka raia haya
 
Mimi siipendi CCM ila sidhani kama ulichokiandika ni sahihi. Hao waliovamia kituo hawawezi kuhalalisha unyama huo eti kwamba wana maisha magumu. Hao ni majambazi yaliyokubuhu na inawezekana miongoni mwao sio waTZ. Ujambazi upo hata nchi zilizoendelea na usiuhusishe moja kwa moja na umaskini!
Ni wajibu wetu wananchi kuwafichua hawa majambazi na kuhakikisha haki inatendeka!

safi sana mkuu umeongea kizalendo mno
 
Mbona matukio kanda ya ziwa kwa ujambazi yanataka zidi? hasa kwa ushirombo, lunzewe na kahama?
Jeshi lifanye kaz kuchunguza maeneo hayo.
Kama mtu anaiba gari la Rais na anakamatwa kwa nini jambazi anaye ua askari wetu asikamatwe?
 
Nimeshaona Movie nyingi za kijeshi na kijasusi. Unakuta kuna jamaa wanapewa mafunzo maalum magumu sana. Sasa huwa wanapewa mission ngumu sana na za hatari/Do or Die ili kujiridhisha kama wameiva na pia huwa ni sehemu ya mazoezi yao. Wanapewa mission hizo hata nje ya nchi. Mfano kufanya uvamizi/Raid kwenye Logistic instalation yenye zana muhimu zinazoweza kutumiwa kuleta madhara kwao nk. Na mara ingine sio lazima wachukue zana hizo, inaweza kuwa hata ni kufanya uharibifu tu ili mradi kumdhoofidha adui yake. Na haya mazoezi yanaweza kufanyika kwa wingi hasa kama nchi fulani haziaminiani au zina mahusiano ya kimashaka. Nimezikumbuka hizi move baada ya kusikia hili tukio la kuvamia kituo nakuchukua smg zaidi ya 5, japo tumekuwa tunahitimisha kila uvamizi kuwa ni Ujambazi na kwamba silaha zimeibiwa kwenda kufanyia uhalifu. Si ajabu jamaa wakawa wameshavuka na kila mmoja ana kabidhi yake. Huo ni mtazamo wangu tu kwasababu ni mpenzi wa Movie. Hata hivyo intellijensia zetu zinatakiwa kwenda mbali zaidi
 
Wakati mwingine wageni tunawasingia tu, watz tumekuwa wanyama sana na hata hao hao polisi ambao ni watz kuna ambao wanaratibu mtandao wa majambazi, zamani pale Benako mpakani na Rwanda palikuwa hatari sana kama utalala usiku lazima uvamiwe lakini ukivuka daraja la mto Lusumo kuingia Rwanda na kuupiga usingizi kwa wenzetu papo shwari (hapa tatizo ni nani sasa ni wageni au sisi wenyewe? na mgeni mpaka afanye uhalifu lazima atakuwa ameshirikiana na mwenyeji). Alafu polisi wetu wanajiamini sana wanapokuwa kituoni na ndio maana hata kama gari lako litakamatwa ukaambiwa ulipaki kituoni yaani hakikisha lisilale maana ukiangalia tu ni rahisi kuibiwa hakuna system nzuri ya cross check usalama zaidi ya kuambiwa acha funguo

Sasa hivi ni ulimwengu wa digitali maeneo muhimu ya polisi yanatakiwa yawe CCTV especially sehemu kama counter na nje hii itajenga dhana ya uwabikaji kwa polisi na raia pia maana hata upokeaji watuhumiwa utabadilka kwani si kamera zinachukua kila kitu.

Sema wewe ukivuka lusumo hata kabanga uko safe kutembea usiku na hata mchana..........
lkn tz ukitembea usiku ni hatari lazima ukutane na wachana tulubai
 
Kwa staili hii hawa majambazi kwenye makazi ya watu wakiamua kufanya mambo haiwapi tabu , Inatisha sana maana uwoga umewatoka kabisa hawa majambazi hadi kufikia hatua ya kuvamia vituo vya polisi!!
 
Nimeshaona Movie nyingi za kijeshi na kijasusi. Unakuta kuna jamaa wanapewa mafunzo maalum magumu sana. Sasa huwa wanapewa mission ngumu sana na za hatari/Do or Die ili kujiridhisha kama wameiva na pia huwa ni sehemu ya mazoezi yao. Wanapewa mission hizo hata nje ya nchi. Mfano kufanya uvamizi/Raid kwenye Logistic instalation yenye zana muhimu zinazoweza kutumiwa kuleta madhara kwao nk. Na mara ingine sio lazima wachukue zana hizo, inaweza kuwa hata ni kufanya uharibifu tu ili mradi kumdhoofidha adui yake. Na haya mazoezi yanaweza kufanyika kwa wingi hasa kama nchi fulani haziaminiani au zina mahusiano ya kimashaka. Nimezikumbuka hizi move baada ya kusikia hili tukio la kuvamia kituo nakuchukua smg zaidi ya 5, japo tumekuwa tunahitimisha kila uvamizi kuwa ni Ujambazi na kwamba silaha zimeibiwa kwenda kufanyia uhalifu. Si ajabu jamaa wakawa wameshavuka na kila mmoja ana kabidhi yake. Huo ni mtazamo wangu tu kwasababu ni mpenzi wa Movie. Hata hivyo intellijensia zetu zinatakiwa kwenda mbali zaidi

... Jambazi na bunduki sita zapatikana
NA MWANDISHI WETU
Jeshi la polisi mkoani Geita,
limefanikiwa kulitia mbaroni jambazi
moja na kufanikisha kuzinasa
bunduki sita ambazo ziliporwa na
kundi la majambazi usiku wa kumkia
juzi katika kituo cha polisi wilayani
Bukombe.
Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi
(IGP), Ernest Mangu, alisema jambazi
hilo lilinaswa porini likiwa na silaha
hizo ambazo ziliporwa baada ya
kuvamia kituo hicho na kuua polisi
wawili papo hapo na kujeruhi
wengine wawili.
“Hawa majambazi wameonekana
kujichanganya na wafugaji waliopo
mipakani, hivyo uhalifu wao
wakifanya wanakimbilia kwa
wafugaji…natangaza kuanzia sasa
wale wafugaji waliopo pembezoni
mwa mipaka kuondoka mara moja ili
kutowapa nafasi majambazi kujificha,”
alisema Mangu.
Hata hivyo, Mangu alisema baadhi ya
mapori ya akiba katika mikoa ya
Kagera, Geita, Kigoma na Shinyanga
yamegeuzwa maficho ya wahalifu na
mikakati inafanyika kutafuta
ufumbuzi wa kudumu badala ya
ukanda wa mapori hayo kutangazwa
kanda maalum ya mikoa ya kipolisi.
Akikwepa kulihusisha tukio la juzi la
kuvamiwa kwa kituo cha polisi na
kuuawa kwa polisi wawili na kujeruhi
wengine na kuondoka silaha
mbalimbali zikiwamo bunduki aina ya
SMG, risasi na mabomu ya kutupa
kwa mkono, alisema matokeo ya
uchunguzi ndiyo yatabainisha ukweli
halisi.
Alisema baadhi ya wahalifu hutoka
nchi jirani na kushirikiana na baadhi
ya wenyeji kwa kutumia mapori ya
akiba na baadhi ya hifadhi kujificha
kabla na baada ya kutekeleza uhalifu
wao.
Alisema operesheni rasmi ya
kuwasaka watuhumiwa waliohusika
na tukio la uvamizi wa kituo cha
polisi cha Bushirombo umeanza
baada ya kikao cha kamati ya ulinzi
na usalama cha mkoa wa Geita
kufanyika juzi.
Juzi watu wanaoaminika ni
majambazi walivamia kituo cha polisi
cha Bushirombo ambacho makao
makuu ya polisi wilaya ya Bukombe
kushambulia na kuwaua polisi WP
7106 Uria Mwandiga na G.2615 Pc
Dustani Kimati.
Waliojeruhiwa ni E.5831 CPL David
Ngupama Mwalugelwa aliyeumizwa
kichwa na usoni pamoja na
kung’olewa meno mawili, huku H.627
Mohamed Hassani akijeruhiwa
kifuani.
CHANZO: NIPASHE
 
... Jambazi na bunduki sita zapatikana
NA MWANDISHI WETU
Jeshi la polisi mkoani Geita,
limefanikiwa kulitia mbaroni jambazi
moja na kufanikisha kuzinasa
bunduki sita ambazo ziliporwa na
kundi la majambazi usiku wa kumkia
juzi katika kituo cha polisi wilayani
Bukombe.
Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi
(IGP), Ernest Mangu, alisema jambazi
hilo lilinaswa porini likiwa na silaha
hizo ambazo ziliporwa baada ya
kuvamia kituo hicho na kuua polisi
wawili papo hapo na kujeruhi
wengine wawili.
"Hawa majambazi wameonekana
kujichanganya na wafugaji waliopo
mipakani, hivyo uhalifu wao
wakifanya wanakimbilia kwa
wafugaji…natangaza kuanzia sasa
wale wafugaji waliopo pembezoni
mwa mipaka kuondoka mara moja ili
kutowapa nafasi majambazi kujificha,"
alisema Mangu.
Hata hivyo, Mangu alisema baadhi ya
mapori ya akiba katika mikoa ya
Kagera, Geita, Kigoma na Shinyanga
yamegeuzwa maficho ya wahalifu na
mikakati inafanyika kutafuta
ufumbuzi wa kudumu badala ya
ukanda wa mapori hayo kutangazwa
kanda maalum ya mikoa ya kipolisi.
Akikwepa kulihusisha tukio la juzi la
kuvamiwa kwa kituo cha polisi na
kuuawa kwa polisi wawili na kujeruhi
wengine na kuondoka silaha
mbalimbali zikiwamo bunduki aina ya
SMG, risasi na mabomu ya kutupa
kwa mkono, alisema matokeo ya
uchunguzi ndiyo yatabainisha ukweli
halisi.
Alisema baadhi ya wahalifu hutoka
nchi jirani na kushirikiana na baadhi
ya wenyeji kwa kutumia mapori ya
akiba na baadhi ya hifadhi kujificha
kabla na baada ya kutekeleza uhalifu
wao.
Alisema operesheni rasmi ya
kuwasaka watuhumiwa waliohusika
na tukio la uvamizi wa kituo cha
polisi cha Bushirombo umeanza
baada ya kikao cha kamati ya ulinzi
na usalama cha mkoa wa Geita
kufanyika juzi.
Juzi watu wanaoaminika ni
majambazi walivamia kituo cha polisi
cha Bushirombo ambacho makao
makuu ya polisi wilaya ya Bukombe
kushambulia na kuwaua polisi WP
7106 Uria Mwandiga na G.2615 Pc
Dustani Kimati.
Waliojeruhiwa ni E.5831 CPL David
Ngupama Mwalugelwa aliyeumizwa
kichwa na usoni pamoja na
kung'olewa meno mawili, huku H.627
Mohamed Hassani akijeruhiwa
kifuani.
CHANZO: NIPASHE
Kuna matukio mengine yasipotolewa feedback nzuri basi inakuwa ni fedheha kwa POLICE to the PUBLIC. kama ni kweli wamekamatwa WELL n GOOD. Lakini inawezekana pia kuwa hawajakamatwa ni changa la macho tu ili kuondokana na Fedheha na AIBU hii
 
Mtu akisema wewe pia ni jambazi atakuwa amekosea? Acha roho ya kinyama ndugu, siku yakiikuta familia yako ndo utaelewa ubaya wa jambo hili. Kifupi amani inatoweka kama jua linavyosogea taratibu mpaka linazama. Hakuna aliye salama. Na ujue sababu mojawapo ya amani ya nchi pamoja na uzalendo ila pia ni udhibiti wa raia kumiliki silaha za moto, sasa ikiwa wanazifuata kwa nguvu silaha hizo, tena mahali penye watu wenye silaha ujue hakuna aliye salama tena. Zikishakuwa nyingi mikononi mwa wahalifu ndio uasi wa nchi unaanza, unakuwa backed na mataifa makubwa basi tena story inakuwa political instability na wanachukua almasi na dhahabu bila shida wakati wenye nchi wanauana tu. Tafakari.

majambazi wameua majambazi wenzao teh teh teh teh
Polisi wa Tz=majambazi
 
pole yetu
[FONT=times new
roman]Wakuu habari za leo Jumamosi?!

Nimepokea taarifa kutoka Mkoani Geita kwamba usiku wa leo majira ya saa 9
watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wamevamia kituo cha polisi cha
wilaya ya Bukombe na kuua askari sita waliokuwa zamu na kuvunja ghala la
silaha na kuzichukua.

Nitaendelea kutoa taarifa kadri zitakavyokuwa zinanifikia.

Updates...

Askari waliokufa ni wawili mmoja hali yake mbaya sana...wengine watatu
wamejeruhiwa.

MoreUpdates.

Askari waliouawa ni Dastan Kimathi na Hulia Mwandiga.

Waliojeruhiwa ni Mohamed Hassan Kilomo (25) ambaye amejeruhiwa kwa
risasi kifuani na kuvunjwa mguu wa kulia.

Mwingine ni David Ngupama Mwalugelwa (44) ambaye amepigwa bomu kichwani
na usoni na kumharibu vibaya.

Majambazi wamepora Bundiki 10 aina ya SMG pamoja na mabomu.

Inadaiwa walikuwa majambazi wapatao watano.

Muda si mrefu RPC Konyo atazungumza na waandishi wa habari.

Endelea kufuatilia hapa hapa...
[/FONT]
============================================




Chanzo: Mtanzania
 
Back
Top Bottom