Kituo cha polisi Geita chavamiwa, Askari wauawa!

Kituo cha polisi Geita chavamiwa, Askari wauawa!

WABHEJASANA

JF-Expert Member
Joined
Jun 22, 2011
Posts
4,225
Reaction score
869
Wakuu habari za leo Jumamosi?!

Nimepokea taarifa kutoka Mkoani Geita kwamba usiku wa leo majira ya saa 9 watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wamevamia kituo cha polisi cha wilaya ya Bukombe na kuua askari sita waliokuwa zamu na kuvunja ghala la silaha na kuzichukua.

Nitaendelea kutoa taarifa kadri zitakavyokuwa zinanifikia.

Updates...

Askari waliokufa ni wawili mmoja hali yake mbaya sana...wengine watatu wamejeruhiwa.

MoreUpdates.

Askari waliouawa ni Dastan Kimathi na Hulia Mwandiga.

Waliojeruhiwa ni Mohamed Hassan Kilomo (25) ambaye amejeruhiwa kwa risasi kifuani na kuvunjwa mguu wa kulia.

Mwingine ni David Ngupama Mwalugelwa (44) ambaye amepigwa bomu kichwani na usoni na kumharibu vibaya.

Majambazi wamepora Bundiki 10 aina ya SMG pamoja na mabomu.

Inadaiwa walikuwa majambazi wapatao watano.

Muda si mrefu RPC Konyo atazungumza na waandishi wa habari.

Endelea kufuatilia hapa hapa...

============================================

Askari wawili wauawa, SMG 10, risasi na mabomu vyaporwa
IGP-Mangu.jpg

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Mangu

BUKOMBE

HOFU ya usalama wa raia na mali zao imetanda baada ya askari polisi wawili kuuawa na bunduki 10 aina ya SMG kuporwa katika Kituo Kikuu cha Polisi wilayani hapa.

Uporaji huo umefanywa na watu ambao hawajafahamika baada ya kuvamia kituo hicho saa 9:45 alfajiri na kuwashambulia askari polisi waliokuwa zamu ambapo wawili waliuawa na wengine watatu walijeruhiwa.

Mbali na kupora SMG 10, pia inadaiwa wamefanikiwa kupora risasi ambazo idadi yake haijafahamika, pamoja na mabomu ya kutupa kwa mkono ambayo walitokomea nayo kusikojulikana.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Joseph Konyo, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema uvamizi huo umetokea baada ya askari waliokuwa doria kushambuliwa kwa bomu kupitia dirisha la chumba cha mapokezi (CRO) kituoni hapo na kisha kushambuliwa kwa risasi.

Aliwataja askari waliouawa kuwa ni WP 7106 Uria Mwandiga na G. 2615 PC Dustan Kimati. Waliojeruhiwa ni E.5831 CPL David Ngupama Mwalugelwa aliyejeruhiwa kichwani na usoni huku akiumizwa mdomo na meno mawili kung'oka na Mohamed Hassan Kilomo ambaye amejeruhiwa kifuani na mguu wa kulia.

Mganga Mkuu wa Wilaya

Mganga Mkuu wa Wilaya ya Bukombe, Dk. Honorata Rutatinisibwa, amekiri kupokea maiti za askari wawili na majeruhi wawili.

Alisema hali za majeruhi zilikuwa mbaya, hivyo walihitaji matibabu zaidi na kulazimika kuwahamishia Hospitali ya Rufaa ya Bugando kwa matibabu zaidi.

IGP atua eneo la tukio

Kutokana na tukio hilo, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Ernest Mangu, alilazimika kwenda Bukombe jana akiwa ameambatana na Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Geita ikiongozwa na mwenyekiti wake, Mkuu wa Mkoa, Saidi Magalula.

IGP Mangu ameagiza askari polisi wa mikoa jirani ya Tabora, Shinyanga,Kagera, Mwanza na Kigoma kushirikiana na askari wa Geita kuwasaka wahusika na kurejesha silaha zote zilizoporwa.

Agizo la IGP kuwataka askari wa mikoa ya jirani kusaidia msako huo, linatokana na asilimia 60 ya eneo la Wilaya ya Bukombe kuwa na misitu mikubwa.

Alisema msako huo utasimamiwa na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) Isaya Mungulu ambaye aliwasili Bukombe kwa helkopta ya polisi saa 11:39 jioni tayari kwa kuanza msako huo.

Pamoja na hayo, IGP Mangu pia alitangaza dau la Sh. milioni 10 kwa mtu atakayesaidia kukamatwa kwa wavamizi hao, ikiwa ni pamoja na kupatikana kwa silaha zilizoibwa.

Katika kile ambacho kilionyesha kwamba viongozi wa juu wa jeshi hilo wamekasirishwa na tukio hilo, jijini Dar es Salaam Kamishna wa Polisi Operesheni na Mafunzo, Paul Chagonja, naye aliitisha mkutano na waandishi wa habari kuelezea tukio hilo, huku akiwataka wananchi kuwa na utulivu.

Hili ni tukio la pili katika kipindi cha miezi mitatu kwa majambazi kuvamia kituo cha polisi. Juni 11, mwaka huu askari polisi mmoja aliuawa baada ya watu wasiojulikana kuvamia Kituo Kidogo cha Polisi cha Kimanzichana mkoani Pwani kisha kupora bunduki tatu aina ya SMG na risasi zake.

Chanzo: Mtanzania
 
Ukicheka na kima........yani imefikia hatua mpk askari nao wanachezewa...inabidi jeshi hili liamke...hii inachangiwa na wao pia kuwalealea...majambazi yakikamatwa soon wayaona kitaani..R.I.P askari
 
Aiseee,sasa wezi wameandelea,kumbe hata askari nao kwao ni target!
 
RIP our soldiers, hili ni tishio sasa kuna kila dalili kuwa nchi inakwenda kusiko, hivi haya matukio ya ujambazi hayana mkono wa watu zaidi ya hao majambazi wenyewe au maadui zetu nje ya mipaka yetu? Inatupasa sote kuamka na kujiuliza ni wapi tunakosea maana tukiendelea kucheka na nyani tutavuna mabuwa
 
serikali ya ccm imefanya maisha ya watanzania kua magumu mpaka raia wanafanya unyama kama huu daah poleni wahanga wa hili tukio..

CCM ni chama cha maruhani.
 
Nchi imewekwa rehani. Serikali dhaifu, Jeshi la polisi limelala fofofo, wanachojua ni kudhibiti upinzani tu na kuhakikisha ccm 'inatawala milele'. Matokeo yake ndio hayo... Poleni wote mlioguswa na hili, lakini watu wa kuleta mabadiliiko ni sisi wenyewe. Mungu Ibariki Tanganyika!
 
Ukicheka na kima........yani imefikia hatua mpk askari nao wanachezewa...inabidi jeshi hili liamke...hii inachangiwa na wao pia kuwalealea...majambazi yakikamatwa soon wayaona kitaani..R.I.P askari

si ajabu mchange na lumumba buku 7 wakasema walio fanya hili tukio ni cdm.
 
Rip askari , majeruhi ugua pole...
 
Shida ni uhamiaji, hawako makini au ni rushwa, hao walovamia kituo siamini kama ni watanzania, hao huenda ni wanyarwanda,burundi, kenya, au wasomali, maana wao hawaogopagi polisi, wito wangu kwa polis msikae kizembe, mnashindwaje kuwa na silaha muda wote? Silaha mnazifungia mnakaa mnakunywa kahawa mnataimiwa,halafu msiwe mnakaa eneo moja, mkae mbali mbali na kila mmoja awe na silaha.mnapoona kundi linakuja kituon amrisheni kuwasachi, atakaewasachi awe ni mmoja tu,wengine muwaelekezee silaha ili wakileta fyoko toa roho zao,lakini kwa tabia hii ya polisi kukaa kwenye bench mmerundikana tena bila silaha na huku mmevua buti mmevaa kandambili mnakunywa kahawa mtaendelea kuuliwa kizembe namna hii,askari sita ni weng sana kama kila mmoja angekuwa na silaha yake na amekaa kijeshi, dhamani askari hata akiwa mmoja alikamata watuhumiwa hata sita na akawafunga mashati na kuwapeleka kituoni,lakini dhama za sasa askari wawili mtuhumiwa mmoja, hvy polis ondoeni dhana ya zamani,
 
Wacha wauwawe tu pengine watapata akili,wanaacha kulinda raia na mali zao badala yake wananyanyasa raia na kula rushwa tu.
Polisi wameshindwa kujua tupo wakati gani huu,nakumbuka huko nyuma hata mtoto mdogo akikataa kunywa uji akitishiwa polisi anakuja basi atakunywa huo uji hata kama haupendi.
Siku hizi polisi wanakaa uraiani nidhamu kushney,vituo vya polisi havina hata fensi unaweza kuingia mpaka kaunta ukafanya ambush na kuteka kituo bila shida.
Tumefika wakati askari wetu mbali na mafunzo ya awali wapelekwe katika nchi zenye uhalifu km SA wakajifunze namna ya kukabiliana na matukio ya kihalifu. Nikiwa SA wakati fulani nilishuhudia gari la kubeba fedha likikatwa kwa gesi na grinder katikati ya barabara na huku majambazi yakiwa yamezingira eneo hilo!!
 
samahani mkuu,umeandika kwa hisia kidogo ila nilitaka nikukumbushe tu nchi hii bila karushwa kidogo mambo hayaendi.utakufa hukuunajiona
 
Shida ni uhamiaji, hawako makini au ni rushwa, hao walovamia kituo siamini kama ni watanzania, hao huenda ni wanyarwanda,burundi, kenya, au wasomali, maana wao hawaogopagi polisi, wito wangu kwa polis msikae kizembe, mnashindwaje kuwa na silaha muda wote? Silaha mnazifungia mnakaa mnakunywa kahawa mnataimiwa,halafu msiwe mnakaa eneo moja, mkae mbali mbali na kila mmoja awe na silaha.mnapoona kundi linakuja kituon amrisheni kuwasachi, atakaewasachi awe ni mmoja tu,wengine muwaelekezee silaha ili wakileta fyoko toa roho zao,lakini kwa tabia hii ya polisi kukaa kwenye bench mmerundikana tena bila silaha na huku mmevua buti mmevaa kandambili mnakunywa kahawa mtaendelea kuuliwa kizembe namna hii,askari sita ni weng sana kama kila mmoja angekuwa na silaha yake na amekaa kijeshi, dhamani askari hata akiwa mmoja alikamata watuhumiwa hata sita na akawafunga mashati na kuwapeleka kituoni,lakini dhama za sasa askari wawili mtuhumiwa mmoja, hvy polis ondoeni dhana ya zamani,

askari wa siku hizi ni mdebwedo kweli kweli hawana ukakamavu kama enzi za kina chrisslukosi
 
Last edited by a moderator:
Yatatokea mengi,hali imesababishwa na maccm
 
Aibu kubwa sana kwa chombo husika!!!!!
Ile ya (Mkuranga???!!!) haikutoa fundisho lolote kweli???!!!

Hivi kama imefikia hatua ya kituo kuvamiwa, kinavunjwa askari wanauwawa, amari inapokwa bado tu haiingii akilini kuwa hali sio nzuri???!!!!

Kuna mdau kasema hapo ukicheka na kima utavuna mabua lakini ukweli ni kuwa kima hawa hawaachi hata hayo mahindi yabebe!!!!!
 
Hii Ni hatari Sana, Kuna miaka kila mwananchi alikuwa mlinzi mwaminifu WA mali zake, kijiji chake na taifa kwa ujumla, hali ile ilianza kuyeyuka taratibu.......sasa taarifa za ujambazi hazipatikani, bad enough wakipungukiwa na vitendea kazi hata hawajiulizi Mara mbili wapi pa kuzipata na namna gani. Miezi michache imepita tangu kuuwawa kwa askari kule Pwani, Leo tunasikia huku Bariadi. Hapa naona tatizo Ni kubwa kuliko wengi tunavyodhani. Polisi peke Yao na intelijensia Yao, bila ule moyo WA kizalendo WA watanzania kurudi....hali itaendelea kuwa mbaya zaidi. Moyo huo unarudi vipi? Haki itendeke kwa kiasi chake, na ionekane ikitendeka! Gape la wenye nacho (hasa la watawala) na wasio nacho lisiendelee kupanuka kiasi hiki! Kukua Kwa uchumi kusiangaliwe katika makaratasi Tu, twendeni field tukalinganishe data za makaratasi na uhalisia! RIP askari, pateni nafuu majeruhi.
 
Back
Top Bottom