getrusa
JF-Expert Member
- Aug 16, 2013
- 2,150
- 1,824
Wakuu habari za jioni nimekuwa nikipita hapa Kibaha Mail moja, kinachonivutia ni hii stand mpya (kituo kipya cha mabasi) kinachojengwa hapa Mail moja.
Kwanza napenda niipongeze serikali kwa kuchukua hatua stahiki za ujenzi huu na kupendezesha Mji wa kibaha hakika panapendeza, pamoja na yote nimekuwa najiuliza je kituo hiki kiko mahali sahihi...?
Nikiangalia umbali kilipojengwa toka barabarani ninapata mashaka kujua kama hituo hiki hakiko ndani ya hifadhi ya barabara! Ukichukua mfano wa ubomoaji wa nyumba zilizojengwa maeneo ya kimara mpaka Mbezi ninapata mashaka kama kituo hiki kitasalimika wakati wa awamu nyingine ya utanuzi.
Kama kitabomolewa je waliohusika na upitishwaji wa mradi huu wataachwa tu kula raha kama wale wa miradi mingine ya hovyo iliyopitishwa?
Nawasilisha..