Idimi
JF-Expert Member
- Mar 18, 2007
- 15,326
- 11,175
Kituo cha mabasi cha Mpemba, kilichopo nje kidogo ya mji wa Tunduma mkoani Songwe kina vyoo vibovu na vinatia kinyaa na aibu.
Kati ya vyoo vya haja ndogo 10, vitatu tu ndivyo vizima, vingine vyote 7 aidha vimepasuka ama vibovu na vimezibwa kwa maboksi.
Kituo hiki, mbali na kutumika na sisi abiria wazawa, kinatumika pia na abiria wa mataifa jirani kama Zambia, Malawi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wanaopita hapo wakielekea kwenye nchi zao.
Ubovu wa vyoo hivi unasabisha msongamano mkubwa wa raia hasa inapotokea mabasi kadhaa yameshusha abiria kwa mara moja.
Abiria tunalipia kutumia vyoo hivyo, ni jukumu la halmashauri ya mji wa Tunduma kuhakikisha vinakuwa vizima na visafi muda wote.
Naomba wahusika (kama ni mkandarasi anayekusanya ushuru ana halmashauri ya mji) warekebishe kasoro hizo!
Naambatanisha na picha za vyooo husika!
Pia soma ~ Songwe: Vyoo vya Kituo cha Mabasi Mpemba Tunduma vyarekebishwa