Kituo cha AICC Arusha kushusha Mjengo Mwingine Hatari

Status
Not open for further replies.

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
749
1,797
Kituo cha Mikutano Cha Kimataifa ( AICC) jiji Arusha,kimedhamiria kuanza ujenzi wa jengo jipya la kisasa kwa ajili ya Mikutano litakalojulikana kwa jina la Mount Kilimanjaro International Convention Center na hivyo kuongeza uwekezaji katika sekta ya kumbi za mikutano.


Jengo hilo litajengwa eneo la Kijenge jijini hapa na litaenda sanjari na ujenzi wa jengo la Biashara litakalojengwa katika eneo la Kaloleni,ujenzi wa jengo la Hospital katika hospital ya Aicc(OPD), litakalohudumia wagonjwa wa nje na kugharimu kiasi cha sh,bilioni 1.5 ambapo mchakato wa miradi hiyo inatarajia kuanza katika kipindi cha mwaka wa fedha ,2019/20.


Akiongea na wapangaji wa Aicc katika maadhimisho ya utumishi wa Umma,kikitanguliwa na kikao cha wafanyakazi wa kituo hicho,Kaimu Mkurugenzi mtendaji wa aicc,Sovo Mung'ong'o alisema kuwa utekelezaji wa miradi hiyo katika hatua ya michoro unatarajiwa kuanza julai na agosti mwaka huu.


"Miradi mingine itakayojengwa ni pamoja na ujenzi wa kumbi za mikutano katika Mikoanya Dodoma, Zanzibar Iringa na Mwanza" Amesema Savo


Aidha Amesema pamoja na kutekelez miradi hiyo mipya Aicc,kimedhamiria kwa dhati kufanya ukarabati wa baadhi ya majengo yake ambayo yamejengwa tangu mwaka 1978 ikiwemo kuweka taa za umeme ,taa za jua na kuboresha miundo mbinu katika barabara zake .


Mkurugenzi, Miliki na Miradi, mhandisi Vickor Kamagenge aliwataka wapangaji katika majengo ya Aicc kuhakikisha wanazingatia mikataba yao ikiwemo ulipaji wa kodi ,bill za maji na umeme jambo ambalo litasaidia kituo hicho kujiendesha na kuweza kulipa kodi ya ardhi na majengo.


"Mwaka Jana tumelipa malimbikizo ya bill ya umeme zaidi ya sh,milioni 100 uliyozalishwa na wateja wetu ,sasa hatutaki hali hiyo ijirudie" alisema Kamagenge.


Wapangaji wa nyumba za kulala za Aicc wameitaka Aicc kuzifanyia ukarabati wa haraka nyumba zake wanazoishi kwani baadhi yake zimekuwa chakavu na kuvuja.


Akiongea kwa niaba ya wapangaji hao Emanuel Kesy amesema wanakabiliwa na wimbi la mbwa koko ambao huwashambulia nyakati za usiku pia kuwepo na vibaka ambao wamekuqa na destuli ya kuiba Nguo zilizoanikwa kwenye kamba na kutokomea.


Wameika Aicc kuimarisha ulinzi katika maeneo ya wapangaji ili kuepuka na majanga ya vibaka hao.


Ends.......



IMG_20190619_113843.jpeg
IMG_20190619_113900.jpeg
IMG_20190619_113906.jpeg
 
AICC hii hii ya kimataifa Mbwa koko wanasumbua na vibaka kuanua nguo kweli?hebu lindeni heshima ya jengo basi
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom