Kituo cha afya hiki kitatusababishia magonjwa ya kudumu kwa kukosa umakini

Chidu Mangalili

Senior Member
Mar 24, 2017
144
96
Kituo kimojawapo ya vituo vya afya kata ya Kaloleni jijini Arusha kimekuwa hatarishi kwa afya za watu wanaoishi maeneo ya Kaloleni na Ulezi pamoja na wanaofanya shughuli zao maeneo ya stand kuu ya mabasi kwa kutokuzingatia taratibu za uteketezaji wa taka zinazo zalishwa hapo kituoni.

Huwa wanachoma tanuru lao la taka majira ya jioni na mapema alfajiri.
Moshi na hewa chafu ya taka za kitabibu husambaa hewani na hudumu kwa muda wote wa usiku.
Hewa huwa chafu kwa usiku huo wa uchomaji hadi asubuhi.

Nimeona nilisemee hili kwani kuna wagonjwa wanaotaabika na hali hii.

Wengine hawajajua hasa chanzo cha uchafuzi huo.

Pia kuna hatari ya kutengeneza wagonjwa wapya hapo baadae watokanao na hali hii.

Watumishi wa kituo hicho wanaohusika na uzembe huu huenda hawajui athari inayowakuta wakazi wa maeneo haya kwani huenda wao hawaishi jirani na kituo.

Nawasihi mrekebishe mifumo ya uteketezaji taka wenu huo tafadhali.

Arusha inafikiwa pia na wageni wa kimataifa ambao wangependa kubarizi mida ya jioni na huenda kuna wanaolala maeneo ambayo uchafuzi wa hewa unawafikia.

NI BORA KUKINGA KULIKO KUTIBU.

USAFI NA USTAARABU WA MTU HUTAFSIRIWA PIA NA USAFI WA HEWA ALIYOJITENGENEZEA KUISHI KWAYO.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom