KITUKO: Nimekojolewa na mtoto kwenye basi

KITUKO: Nimekojolewa na mtoto kwenye basi

Daah nimesoma komenti za baadhi ya wakulungwa zinatia ukakasi flan kidogo....kiukwel ukiwa a family man swala la kusaidia watoto ni Jambo la kawaida Sana....huwezi ukaona mtoto anapata shida ukaacha kumsaidia au kuona mtu anapata changamoto flan ukashindwa kumsaidia kama unauwezo wa kufanya hivyo...

Mtoa post alisaidia Kwa mapenz makubwa kwakuwa ana asili ya ubaba,na always wababa WA ukweli huwa ngao na furaha Kwa jamii Yao......yaliyotokea ni bahati mbaya Tu,lkn yasitufanye next time kuacha kufanya wema Kwa binadamu wenzetu.

Much respect kwako article
 
Huo ndio ukubwa mkuu, angekuwa wako ungevumilia wala usingetwambia,ndo mpende jirani yako kama nafsi yako ndio hii🙄🙄🙄
 
Mosi ukamsalimia hakujib vizuri

Pili ,huruma kiuno chamtoto

3--- ilikua kukazwa huyu mama enzi tunasafiri na basi tumetafuna sana akina mama kwa dizaini hiyo ,unaweza shika mtoto kilomita 500....mama wamtoto anakuona wamana

Mwishowake anachezea mguu haijalishi itakua lini kikubwa kakupa namba sahihi
 
Mi nimewahi tapikiwa 2011 sema nilimsamehe maana alikua mama kijacho, ila harufu haikuisha
poleeeeeh, mie niliyemtapikia pale pale akaomba kwa dereva ashukie pale, then akanipa no yake nimtafute, couz nilikua naenda shule sikua na cm.

Tulimuacha pale sisi tukaendelea na safari, ila nilikua najiona mkosefu sanaaa. Nilikua had naogopa mnooo, nilipofika shule siku ya weekend nkamcheki, kilichofuata ni neema naa baraka tyuuh.
 
Ujanja wote huo unatapika kwenye mabasi? Au ulikuwa unaumwa?
Bina, mie natapika mnooo hata nikisikia harufu ya dizeli ile ilotumika natapika.

Nna tabu mnooo, huwa nabeba vifungashio hata 4 km safari ya mbali.
 
Bina, mie natapika mnooo hata nikisikia harufu ya dizeli ile ilotumika natapika.

Nna tabu mnooo, huwa nabeba vifungashio hata 4 km safari ya mbali.
🤣🤣🤣🤣🤣hapa nshanusa harufu ya tapishii
Jikaze bwana uwe unakunywa promethazine kabla ya safari yako kuanza. Hutatapika hata ila utaupiga usingizi mwingi kama teja
 
Una moyo, Mimi ilikuta mtoto analia sana yupo na mama yake,analia nimpakate ...aisee nilimkata yule malaika jicho Kali hakurudia tena,alikua akijisahau ananililia namkata jicho moja anatulia
 
punguza shobo bro.....wanawake wa siku hizi akili zao zimehamia kwenye papuchi na makalio......ilitakiwa hata huo msaada usimpe kwa sababu hakukuonyesha ushirikiano toka mapema.............
 
Mkuu unatabia ngumu kumbe
Unapakata mtoto mara mama yake anakubadilikia ulikuwa unataka umlawiti hivyo anaanzisha vurugu anataka umlipe pesa


Au anakuachia mtoto anaenda chimba dawa basi likisimama wote wanarudi ye harudi unamwambia konda amwambie dereva asiondoke watu wanalalamika wanachelewa konda anashuka kucheki kumuulizia watu huko nje wanasema wamemuona mmama kakimbia


Hayo ni machache
 
Habari za Usiku Wadau,

Nipo kwenye bus mida hii natokea Dar naelekea Dom pembeni yangu yupo mdada mwenye mtoto mwenye kama miaka mitatu hivi.

Safari inaanza huyu mama nikampa hai hakuitikia kivile mi nikapotezea.

Tumefika maeneo ya kibaigwa huyu mwanae akawa kamlaza kidizaini fulani mtoto nikaona amelala vibaya na anaumia kiuno so nikaamua kutake trouble ya kumuinua na kumlaza kwangu huku akiegemea kwa mama yake na miguu kwangu.

Safari imeenda mara dogo akawa akijipindua pindua ghafla nikaanza kuhisi ubaridi kama maji vile nimemwagiwa kumtoa yalabi nimeloa mkojo mapajani kwenye suruali yaani ghazabu fasta ikanipanda ila nikachili nikamwambia huyu Dada mwanao kanikojolea!

Huyu Dada mwenye mtoto kuona hivyo akaanza kujibalaguza samahani kaka , only that!Akamchua mtoto wake na kumpakata hata hajambadilisha nguo.

Nimeboreka hapa wwe acha tu sema sina cha kufanya na huyo dogo anaonekana mkubwa so sijui kwa nini amenikojolea!

Ugentlemen leo umenitokea puani,Du hatari hapa nanuka kojo tu.Sometimes ndio maana naonaga baadhi ya abiria wanawekaga sula ya mbuzi kwa wamama wenye watoto kumbe huwa wanakimbia issue kama hizi.

Nashauri wamama wanaosafiri na watoto ambao hawana siti wachukue taadhari za usafi ikiwemo kuwavisha Diapers watoto wao ambao bado hawajajitambua na kuwa na zana za usafi kuepuka kero kwa abiria wenzao.

Nashukuru Mungu tunaingia Dom usiku kama ingekuwa mchana kidume sijui aibu ningeficha wapi.

Usiku mwema.

ARTICLE.
Nakushauri nenda haraka kapime u...to japo sikuombei, hawa watoto wa siku hizi si wakuwaamini kwani yale mambo yetu huyaanza mapema.
 
Back
Top Bottom