Sioni cha ajabu hapo, mnaoona kama hizi kazi angepewa mtanzania, mjiulize kwa nini nyie hamzifanyi? Ni sawa na wamarekani wanalalamika mexicans wanakuja kuchukua kazi zao ndogo ndogo, huku ukiwaambia wafanye hawawezi.
Huyu jamaa anaongea kihindi, ni wazi kabisa, Tanzania ina visitors wengi sana wanaolonga kihindi, huyu anajua kihindi, anajua kiingereza, wabongo wangapi kihindi kinapanda? na je walienda kuomba hapo kazi au ndio wale wanajidahi hawawezi hudumu kwenye migahawa? Na tuwe wa kweli, hata kama ni business decision, ukweli watanzania wengi wanaopanda ndege ni watu ambao kiingereza kinapanda angalau kiasi flani, ambao hawajui kiingereza hata kidogo wengi wao masikini wanapanda mabasi.
Raia wa kigeni wana ruhusa kufanya kazi Tanzania, na isitoshe Kiingereza ni lugha ya taifa, ndio maana tunaitumia kufundishia kuanzia secondary hadi chuoni, tuliihalalisha wenyewe. Watanzania tusilaumu wageni kwa uvivu wetu wenyewe, kama mtu uko competitive ungekua na kazi hadi sasa hivi, kuondoa wageni alafu wabongo wamelala hakuna replacement ni kutafuta visingizio tu.