Kituko JNIA mgahawani: Immigration hii si sawa!

Kuna watu wanajitoa akili mleta mada upo sahihi muhudumu lazima ajue kiswahili kama lugha ya taifa na kiingereza kama lugha ya biashara, ndo mana ukienda ujeruman, china, algeria, korea, n.k kwa ajili ya kuishi au kufanya kazi lazima ujifunze lugha yao full stop 😎
 
Nasafiri kwenda Mwanza flight FN 141 kuelekea Mwanza.
Kabla ya kupanda ndege naamua kupata kipasha moto, kahawa na keki, kwa kiswahili safi kabisa.

Namuuliza mhudumu kaunta aliyevaa shati bkuu, tai na kapendeza, muasia.

Cha kushangaza ananiuliza "what sir?"
Nashangaa, narudia tena kwa kiswahili.
Ajabu jamaa anasena"I dont understand sir"
Namuuliza "how did you get here, and where are you from"
Ananijibu "India sir"
Immigration, mtu asiyejua hata lugha ya kiswahili anafanya nini hapo?
Na ana kibali cha kazi au?
Mkuu kazi zile hata Mwajuma ndala ndefu anaweza kuzifanya na English yake ya "come here go there", usishangae kuwa kuna mkono wa mkubwa kwenye system nzima hiyo.
 
Kwani mgeni haruhusiwi kufanya kazi nchini?
wa hapa kwetu walikuja kubebwa na immigration,kulazwa mahabusu,,,, na kamapuni ikalipa mpunga wa kutisha waliobaki wote ni wale wahindi wa kariakoo ambao vitovu vimetupwa hapo ocean road ambao pale mwanzo walikuwa wanajifanya hawajui kiswahili!!! lakini sasa tunapiga porojo kama kawa kwa kiswahili cha kizaramo kile cha ndani kabisaa
 
Sasa kosa ni lugha, ok.

Ila waakiweka wazawa nao washindwa na kuharibu biashara.

Wewe kwenda kusema sijui achekiwe ni ubaguzi tu. kwani mtu kutokujua lugha ndio hana kibali cha kuwepo nchini? Siku nyingine jibadili uwe detective uulize maswali hapo hapo
Jitathimini kwanza kile unachojadili kama unauelewa kuhusu lengo hasa la mtoa post. Katika kuajiri wageni hapa nchini inabidi kuangalia hasa kama kuna wazawa wenye vigozo na kama utakosa basi utaajiri kutoka nje ya nchi. ila sitegemei kama hapa nchini tunakosa wahudumu wa migahawa kwa kuwa kikubwa zaidi ni kuwa na ulewa wa lugha mbili kiswahili na kiingereza na hapa nchini kuna vyuo vingi vinavyozalisha wahudumu katika maeneo sawa na hili. hivyo tunatakiwa kuwapa kipaumbele wazawa kabla ya kuangalia wageni.
 
Wapi kwingine uliona migahawa ya airport wana bei mbili za raia na wageni ? Iwe kwa dola yen pound euro au shillingi?
Sehemu nyingine unapotumia au kunujua chochote, unatakiwa upate risiti, ukifika airport muda wa kuondoka unawapa risiti wanakupigia hesabu ya kodi uliyolipa halafu wanakurudishia hiyo!
 
Jitathimini kwanza kile unachojadili kama unauelewa kuhusu lengo hasa la mtoa post. Katika kuajiri wageni hapa nchini inabidi kuangalia hasa kama kuna wazawa wenye vigozo na kama utakosa basi utaajiri kutoka nje ya nchi. ila sitegemei kama hapa nchini tunakosa wahudumu wa migahawa kwa kuwa kikubwa zaidi ni kuwa na ulewa wa lugha mbili kiswahili na kiingereza na hapa nchini kuna vyuo vingi vinavyozalisha wahudumu katika maeneo sawa na hili. hivyo tunatakiwa kuwapa kipaumbele wazawa kabla ya kuangalia wageni.

Ukiweka lugha pembeni

Tanzanians customer service, pia communication skills kwa wengi ni majanga, wengine hata mabosi waongee vipi ule uvivu na tabia sijui ya wapi hawabadiliki.

Sasa kwa nini mtu uache kuajiri wa nje, ambao watafanya wateja warudi tena?
 
Nasafiri kwenda Mwanza flight FN 141 kuelekea Mwanza.
Kabla ya kupanda ndege naamua kupata kipasha moto, kahawa na keki, kwa kiswahili safi kabisa.

Namuuliza mhudumu kaunta aliyevaa shati bkuu, tai na kapendeza, muasia.

Cha kushangaza ananiuliza "what sir?"
Nashangaa, narudia tena kwa kiswahili.
Ajabu jamaa anasena"I dont understand sir"
Namuuliza "how did you get here, and where are you from"
Ananijibu "India sir"
Immigration, mtu asiyejua hata lugha ya kiswahili anafanya nini hapo?
Na ana kibali cha kazi au?
Kwenye hii thead ndio nimepima IQ za waTZ, mtoa mada anashangazwa na raia anayefanyakazi TZ lakini hajui kiswahili ndio mshangao wake, hazungumzii mgeni kutokufanyakazi,ila anazungumzia iweje anakuja raia wa kigeni kwetu kufanyakazi lakini hajui kiswahili ......Nikirudi kwenye mada, hili kweli ni tatizo la nchi yetu kutokusimamia sheria zetu za kazi. Haiwezekani mgeni anafanyakazi TZ halafu hajui kiswahili wakati nchi zingine huwezi kufanya hivo.
 
Pamoja na kujifanya wewe ndio mjuaji zaidi na mwenye IQ ya juu lakini ndio wale wale tu,

Chukulia mfano wa Dubai international airport,kuna wahudumu/waiters kibao tu kwenye migahawa ya airport na hawajui kiarabu na wala sio waarabu! Qatar,Saudi arabia na hata Ujerumani ni hivyo hivyo pia,

Unaonekana hujawahi kutoka nje ya mipaka ya Tz,unaandika kwa hisia tu,mimi naandika/nacomment kwa experience.

Mleta mada bila shaka itakua hiyo ni mara yako ya kwanza kutumia Airport kwa ajili ya safari ndio maana umeshangaa kuona vitu ambavyo ni vya kawaida tu kwenye nchi nyingi tu.
 
Vipi unajisikia kufanya mdahalo na mimi,au unani quote kwa kujisikia tu .........???
 
Wapi kwingine uliona migahawa ya airport wana bei mbili za raia na wageni ? Iwe kwa dola yen pound euro au shillingi?
Hata mimi nimeshangaa. Yaani kuna bei mbili? Ya raia na wageni? Wabongo sisi kiboko na mtu kama huyu naye utamkuta ana donge balaa na mamlaka husika kisa tu hauziwi vitu kwa bei rahisi wakati ye ni raia [emoji23][emoji23][emoji23]. Na watajuaje kuwa huyu ni raia na huyu siye? Au itabidi kutoa passport ukitaka kununua andazi?
 
Heheeeee,shangaa na wewe mkuu,siku hizi kila mtu ni mjuaji hata kama hajui kitu,atajitia anajua kwa kulazimisha tu ili mradi asiachwe nyuma na yeye aonekane yupo kwenye hii dunia,Kazi kweli kweli.
 
Business lounge kwenye viwanja vyetu vya ndege mara nyingi zinaendeshwa na hawa ndugu zetu Wahindi ikiwa ni pamoja na hiyo migahawa mingine ,hivyo usishangae kukutana na Muhindi asiyejua Kiswahili swala liwe tu ana vibali husika vya kufanya kazi
 
Nasafiri kwenda Mwanza flight FN 141 kuelekea Mwanza.
Kabla ya kupanda ndege naamua kupata kipasha moto, kahawa na keki, kwa kiswahili safi kabisa.

Namuuliza mhudumu kaunta aliyevaa shati bkuu, tai na kapendeza, muasia.

Cha kushangaza ananiuliza "what sir?"
Nashangaa, narudia tena kwa kiswahili.
Ajabu jamaa anasena"I dont understand sir"
Namuuliza "how did you get here, and where are you from"
Ananijibu "India sir"
Immigration, mtu asiyejua hata lugha ya kiswahili anafanya nini hapo?
Na ana kibali cha kazi au?
Hauna hoja ndugu yangu. Suala la mgahawa liko chini ya mamlaka ya uwanja wa ndege JNIA sasa uhamiaji wanahusika vp hapo. Ulishawahi kupewa chakula na uhamiaji?
 
Back
Top Bottom