mjasiliaupeo
JF-Expert Member
- Apr 21, 2013
- 2,170
- 3,106
Hahahaaaaaa!! Khaah dogo katisha, ila nasubiri kituko chako[emoji12] maana mie chautundu najaza ndoo.Hahaha mtoto ni mtoto tu. My lil sis yeye alikuwa anaonja kitu chochote mbele yake. Yani kila anachokiona anabugia tu fasta. Tushapata kesi kibao na yeye kwa mzee maana mara leo anywe mafuta ya taa, kesho kabugia mseto dawa, mara atake kuonja mafuta ya betri yani ni heka heka tu. Si unawajua wazee mlivyo, nyie mnaona tu kama sisi hatupo makini na mtoto, wazembe
Siku ya siku, bi mkubwa alihisi kuna panya kaingia ndani. So akamtegea dawa, kosa ni kwamba alichukua kipande cha samaki kizuri tu kwa matumizi ya binadamu, akapaka dawa akategesha kwenye kisosi. Ameingia bafuni kuoga, anatoka kipande cha samaki hakipo. Mmh machale kumcheza haiwezekani dk chache panya awe ashabeba samaki wote yule, kamuita dogo, kumuuliza uliingia chumbani dogo kagoma. Maza kampa kofi takatifu ikabidi kaseme kenyewe ndo kamechukua samaki Hahaha. Mama presha Tafuta maziwa fasta, kumpigia simu mzee fasta (ilikuwa weekend uzuri) wakamuwahisha hospital. Kufika hospital ikaonekana dawa haina nguvu kihivyo so wakampa tu nini sijui
Tatizo sasa mzee wangu ni anapenda utani, me sioni ndani. Ile hospital aloenda ndo huwa tunatibiwa hapo mara nyingi so doctors tumezoeana nao. Dr mmoja akaanza kumzingua mzee " eti daah ila mshkaji hiki si kiashiria kizuri, haiwezekani mtoto achukue hadi samaki wa panya, home lazima kuna uhaba wa nyama nyama. uwe unawanunulia nyama watoto bana", mzee akaishia tu kucheka.
Usiku tumekaa mzee akaanza kuniambia "daah ila watoto wanatiaga aibu jamani, huyu dogo kanifedhehesha leo, utadhani nyama halagi, kumbe anakula hadi basi", nilichekaje
Duuuh ex shemeji hivi kumbe haya mambo umeyaanza kitambo[emoji134]Nikiwa mdogo niliwahi kuiba hirizi iliyokuwa inapumua ya mzee mmoja mchawi aliyekuwa anaogopeka sana pale kijijini. .kwenda kuipasua nilikuta kinyonga aliyekatwa mkia alitweta kwa kukosa pumzi vizuri
Lile tukio lilikuwa kubwa na baya pale kijijini mpaka ikibidi nihamishwe
Hahaha rudi page za nyuma kidogo utaona kituko changu (page ya 8)Hahahaaaaaa!! Khaah dogo katisha, ila nasubiri kituko chako[emoji12] maana mie chautundu najaza ndoo.
Hahaha nahisi kimoyomoyo mzee alimmind dogo.Yaaa watoto sometimes wanaaibisha sana Heaven Sent , i can imagine mzee alivyojisikia japokuwa ilikuwa utani
Hii ilinitokea Mimi form four ninajisahau Kama niliiweka dvd na hata tv sikuzima umeme ulirudi Mida ya saa 2 usiku afu ndio tumekaa mezani tunakula...nilikana kabisa sihusiki na sijagusa tvNskumbuka ndugu yangu miaka ya hivi karibuni alivizia mama yake na baba yake awapo akatupia kitu hicho,da umeme zii,jamaa kachanganyikiwa,sasa anajua kwamba mama yake jion humuagizia kwenye mambo ya vikoba,sasa jamaa kafikilia hapa wazee wakirud wakiniagiza harafu umeme ukarud itakuwaje,jamaa katulia tutweeeeeee,walivyorud jamaaa akaongopea km anaharisha kweli wazaz wake walivyorudi wakawa na lengo lilelile la kumuagiza,sasa baada ya kuona kwamba jamaa anaendesha basi wakasema atampelekea asubuhi,jmaaa huku akipiga misele ya ndani chooni,ndani chooon,sasa wakati ile nakwenda chooni anafungua mlango "anasikia uwoooooooooo",jamaaa badala ya kuingia choooni mbio ndan mpka wakamshangaaa,alivyofanikiwa akasema mwanzo na mwisho
Hahaaaaa akyanani, utoto raha sana kwa kweli, unajifanyia mambo kadri akili inavokutumaHahaha rudi page za nyuma kidogo utaona kituko changu (page ya 8)
Hahaha nahisi kimoyomoyo mzee alimmind dogo.
Siku moja tena kapo kindergarten bado. Karudi shule kafika tu "mama mimi kesho ntaachwa na school bus, sijalipa ada". Mama akamwambia mbona ada tulishalipa, hudaiwi. Yeye kakazania tu, ataachwa na gari, yani kakomaa huyo mmh
Basi jioni yake nilikuwa nimetumwa dukani, nikarudi na chenchi nikaziweka mezani kwa mama chumbani kwake. Kesho yake mchana maza ananiambia heaven nipe zile hela ulizorudi nazo dukani, nikamwambia niliweka mezani kwako mbona. Kaanza kuniambia wewe usinitanie. roho tu ikaniambia ukute dogo kaichukua kaenda kulipa shule as alikuwa anaogopa kuachwa na gari. Hela yenyewe sijui elfu 8, sasa sijui ni ada ya shule ipi mwee
Basi ile Karudi tu nikampokea na kimtego " vipi umempa ada sista, kasemaje". Mwenyewe kwa bashasha zote kajibu "eeh nimempa, kasema Ahsante sana", cheko lilinibana nikamfikishia ujumbe mama ake, kumbe hela yenyewe kuna mtoto mkubwa alimpokonya huko shule. Siku hiyo bi mkubwa kamsamehe. Kesho yake Karudi shule kuonja onja kaingia store kakuta mafuta ya battery akataka kunywa, jamani alipigwa mabanzi na mama hadi aliiva na hivi ni keupeee sasa hahahhaa. Ila tunamshukuru kameshakua kenyewe tumepumzika na stress mmh
Mungu wangu nimecheka hadi machozii. Kama hujabadilika utakuwa na rohoo mbayaa mbayaaa mchoyo mchoyoo hahaaaaaa hizo hasira zako komeshaaaNilipokuwa mtoto nilikuwa napenda sana wali maharage na hata iweje ni lazima mimi nipikiwe Chakula hicho.Siku moja hali ikawa ndivyo sivyo nyumbani na bi Mkubwa akaniambia bwana mzee leo hakuna wali utakula ugali tuu jioni. Nikajifanya mimi bingwa wa hasira si nikanyea unga uliokuwa umehifadhiwa kwenye kindoo.Kilichonipata ni Mungu tu anajua.
Duh ... hii ilikuwa balaasitasahau nilivyoingia chooni wakati shangazi anajisaidia kisa tu nilikua najiuliza hivi huwa wanajisaidia kama mimi au wana style yao na je ina ukubwa gani yaani i was curious to know,
nilichapwa mnooo na ni kati ya tukio ambalo huwa silisahau.
dah, naujua huu, na hii kitu ilikua inatokea sana kule uchagani, kwa kilugha hivi huu mmea ulikua unaitwaje tena?
Ha haa hii tunafanana... Nilikua wa 63 nikafuta 3 nikabakiza 6 na nilijua sio rahisi kustukiwa mana ile ya kwanza hawakustuka. Hii ya pili maza alikua makini nilisemwa na kupewa fimbo za haja siku hiyo. Na nikafikishwa kwa mwl mkuu nikala fimbo na tokea hapo matokeo akawa anaenda kuchukua mzazi.Mi nilivyokuwa darasa la nne ripoti iitoka nimefeli kinyama,mwalimu akanipa kwwnye bahasha niipeleke home,mwanaume nikasema ngoja niifungue niicheki,kufungua tu daaaah,kitu nimekuwa wa 67 kati ya wanafunzi 77,nikaona huu ni msala nyumbani,basi nikaifuta ile sita kiustadi sana nikaonekana nimekuwa wa saba,home wakastukia mchezo kwani maksi zilikuwa mbovu halafu eti nimefaulu,weee,nilikula mbata,siwezi kuzisahau kamwe
Ha ha haaaaha haha mimi nilikuwa wa 13 nikafuta tatu na kuitoboa kabisa kufika home baba anauliza mbona imefutwa futwa nikasema kalamu ya mwalimu ilikuwa imeisha akawa anaitengenezea pale pakatoboka na amesema samahani sana ,,, ha hahaha ndugu yangu niliambulia kibao cha kwenye lips kutoka kwa mother aiseee nilipigwa mpaka nikaumwa
ulianza zamani sana huenda sasa hivi ni gwiji
Kila kitu kina asiliDuuh...[emoji176] [emoji176] [emoji125]
Ha haa hii tunafanana... Nilikua wa 63 nikafuta 3 nikabakiza 6 na nilijua sio rahisi kustukiwa mana ile ya kwanza hawakustuka. Hii ya pili maza alikua makini nilisemwa na kupewa fimbo za haja siku hiyo. Na nikafikishwa kwa mwl mkuu nikala fimbo na tokea hapo matokeo akawa anaenda kuchukua mzazi.
Aise hii tuliifanya utotoni ila tulimbahatisha mwendesha baiskeli alupoukanyaga tu mwiba upepo wote ukaisha tukacheka sana, alitutandika akatupeleka pia kwa baba naye alituchapa hasa utoto bwanaNilichukua miba ya mtende huwa ni mikubwa hivi nikaichimbia nikiacha ncha kali kwa juu katika kinjia wanapita watu halafu nikajificha,akapita kaka mmoja akakanyaga nikacheka akaniona nilikimbizwa mpaka leo sikurudia japo hakunipata.
Wanasema vimbwanga vyetu ni analojia, vyao digitali!Yaani hata usemeje pole sikupi, nao wanavimbwanga vyao acha kabisa.
Daaaah kwa mjerumani(as we used to call our mom) hilo hatukuthubutu kufanya, maana unaweza ukasahau hata jina lako.Ha haa hii tunafanana... Nilikua wa 63 nikafuta 3 nikabakiza 6 na nilijua sio rahisi kustukiwa mana ile ya kwanza hawakustuka. Hii ya pili maza alikua makini nilisemwa na kupewa fimbo za haja siku hiyo. Na nikafikishwa kwa mwl mkuu nikala fimbo na tokea hapo matokeo akawa anaenda kuchukua mzazi.
Duuuuuuh!!Kijana kumbe we ni bro wangu kwenye hizo vitu..Nakumbuka mi first time kuangalia nilikuwa form one..Basi baada ya kutoka kuangalia kila msichana ninayekutana naye namuona kama yupo uchi vile
Teh teh teeeeh! Ukataka kumbikiri sister! Ila sijui kuna nguvu gani kwenye maneno mabaya, watoto huwa rahisi sana kuyadaka.Mi nakumbuka kuna demu alimzingua jamaa mmoja kitaa..Basi yule jamaa kwa asira akamwambia "ujue ntakubikiri"..Basi mi nikalipenda hilo neno bila hata kujua maana yake..Nikihisi kuwa litakuwa linamaanisha ntakupiga....Siku tumekaa sitting room na wazee pamoja na wagen tunacheki Tv tukaanza kugombania rimoti na sista..yeye akiwa anataka kubadili chanel..Ndo kumwambia "ujue ntakubikiri,we endelea tu"...
Nilipelekwa chemba nikapewa stiki za kutoha..Zen baadae darsa ndo likafwata..Ndo ikawa chanzo cha kupunguza kuokotaokota maneno kitaa