ni hatari kweli mlikua mnauacha hadi asubuhi?Mie bibi yangu miaka hiyo akiwa hai aliwahi kuja Arusha si unajua tena baridi yake, yaani usiku akitaka kulala mbali na blanket na shuka mpaka umewekee na vimkaa kwenye jiko uvunguni ili apate lile joto ndio analala. Na bila kumuwekea halali aisee na hata akilala atasononeka huyooo.
Uzuri kitanda kilikuwa kirefu hivyo ikawa ni lazima kufanyiwa hivyo japokuwa kulikua na hatari ila hakukuwa na jinsi si unajua tena mtu akiwa mzee anakuwa kama mtoto vile.
Hapana my dear ilikuwa kwa muda tu akishapata kile kijoto tunautoa.ni hatari kweli mlikua mnauacha hadi asubuhi?
aisee si unifundishe na mimiMi nakumbuka tu bibi yangu alivyonifundisha kupanda fisi
[emoji57] [emoji57] [emoji57] bad guyNiliweka pilipili kichaa kwenye kiko akavuta wacha aimbe siku 3 mfululizo nyimbo zenyewe hazieleweki
Looh maskinBabu yangu akiwa amelewa gwagwa/pombe ya ndizi alipenda kujigamba kijiji kizima ati yeye ndo kasomesha wanae.wananzengo /wanakijiji wakakasirika mmoja akamwotea mvua imenyesha akamkata panga.japo alimjeruhi tu hakufa.japo sasa amelala.alikuwa mwenyewe mpaka la 12 enzi hizo.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Babu yangu ni mfugaji ana ng'ombe nyingi sana,sasa ni kama amekua affected psychologically kwamba kila mtu huwa anam_treat kama ng'ombe
Sasa kuna mtoto wake mmoja(dingi yangu mdogo) alikua mtoro sana wa shule,siku moja Babu akaona huyu dogo asintanie,akavizia asubuhi kabisa jamaa bado kalala akamkamata akamfunga kamba za kufungia ng'ombe na akaanza kumswaga kama anaswaga ng'ombe hadi skuli huku akimtandika fimbo dingi mdogo
kufika skuli wanafunzi ndo wako paredi afu jamaa ndo analetwa huku amefungwa kamba na babu
Ilikua noma sana siku hiyo wanafunzi na walimu walicheka sana siku hiyo
Sikupatii picha hasira yake[emoji23][emoji23][emoji23]Baada ya kuvunja ungo tu nikiwa kidato cha pili, bibi yangu nilipokuwa nikitoka shule (nilisoma day) alinikagua bikira au popote pale mradi nimeenda kitaa nikirudi nilikaguliwa vua pichu lala kitandani panua miguu isipokuwa siku za damu tu zinginezo hilo zoezi lilifanyika, hasira nilokuwa naipata basi tu,
Alale mahali pema bibi
[emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2]bibi alikula dawa ya mswaki kila mara alikuwa anasema nimletee ajilambe