Kituko: CCM walalamika kuibiwa kura Moshi Mjini

TAWA

JF-Expert Member
Jun 23, 2013
3,667
1,566
Ni kituko kwa kuwa tume ya uchaguzi iliteuliwa na mwenyekiti wa CCM Taifa ambaye pia ni mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano.

Mkurugenzi wa wilaya ambaye kimsingi ndiye msimamizi wa uchaguzi ngazi ya wilaya ameteuliwa na mwenyekiti wa CCM taifa.

Watendaji wote wa kata wapo chini ya serikali ya CCM.

Sasa wapinzani wameibaje kura? Kwanini tusiamini kuwa mmelewa?
 
Ni kweli,kuna kura ziliokotwa kwenye msitu wa mwanjera zimetiwa tiki kwa upande wa ccm kwenye urais,wabunge na madiwani na zina muhuri wa nec
 
Ni kweli,kuna kura ziliokotwa kwenye msitu wa mwanjera zimetiwa tiki kwa upande wa ccm kwenye urais,wabunge na madiwani na zina muhuri wa nec

Sasa si ndiyo ccm walitaka kuiba kura kwa kuleta kura feki wakafeli wakaamua kizitelekeza msituni!?
Ukumbuki yale ya Himo kule Vunjo!!!?
 
Ni kweli,kuna kura ziliokotwa kwenye msitu wa mwanjera zimetiwa tiki kwa upande wa ccm kwenye urais,wabunge na madiwani na zina muhuri wa nec

Hizo ni sawa na zile zilizokamatwa Bukoba baada ya kushindikana kuingizwa kwenye masanduku.
 
Sasa si ndiyo ccm walitaka kuiba kura kwa kuleta kura feki wakafeli wakaamua kizitelekeza msituni!?
Ukumbuki yale ya Himo kule Vunjo!!!?

Kwa upande wa moshi mjini kwa kweli ccm walizidiwa ujanja na chadema mgombea wa ccm alikubalika kilichokuja kutokea ni ccm wenyewe kwa wenyewe kumhujumu sana hususani yule Tajiri wa mabasi aliyeshindwa kwenye kura za maoni na Devis mosha, huyo Tajiri aliamua kumkomoa mwenzake akaungana na Ndesambulo wakafanya yao kirahisi tu.
 
Kwa hiyo ndiyo wanaenda mahakamani hao ccm!?
 
Hata mimi nimesikia leo asubuhi nilipigwa na mshagao ni bora wakakaa kimya kuepuka aibu kwa umma
 
Hizo ni sawa na zile zilizokamatwa Bukoba baada ya kushindikana kuingizwa kwenye masanduku.

Kwa hapa moshi mjini ccm hawakuwa na kura feki bali kilichofannyika ni ccm wenyewe kwa wenyewe kuhujumiana sana huku ndesa pesa akiwa kapenyeza mashushu wake watatu kwenye kambi ya Devis mosha, jamaa mmoja anaitwa Gaga alikuwa akitumiwa na ndesa pesa kumpelekea Habari zote huku akishinikiza wafuasi wa ccm wawapige chadema kisha kukimbilia Radioni kusema wanapigwa na ccm, hizi mbinu za kimafia za ndesa pesa akishirikia na mwana ccm anayejulikana kwa jina la Ibra line ambaye ni Alikuwa hasimu wa Devis mosha.ndipo Ibra kwa kumtumia ndugu yake Devis anayeitwa Siza wakaenda kuleta mawakala toka Arusha ambao ndiyo walimhujumu sana Devis mosha ambaye ni mara ya kwanza kujiingiza kwenye Siasa ingawa alijitahidi sana kuifufua ccm ambayo ilikuwa imefifia sana moshi mjini kutokana na chadema kutawala miaka 15 bila kikomo.
 
Ni kituko kwa kuwa tume ya uchaguzi iliteuliwa na mwenyekiti wa ccm taifa ambaye pia ni mheshimiwa Rais wa jamhuri ya muingano.
Mkurugenzi wa wilaya ambaye kimsingi ndiye msimamizi wa uchaguzi ngazi ya wilaya ameteuliwa na mwenyekiti wa ccm taifa.
Watendaji wote wa kata wapo chini ya serikali ya ccm.
Sasa wapinzani wameibaje kura? Kwa nini tusiamini kuwa mmelewa?

Kilichomteketeza Devis mosha ni wale Watu ambao walipenyezwa kwake na ndesambulo na ibra line, hao watu ndio waliokuwa wakimteketeza na kusuka mipango yote ya Uovu juu yake ikiwemo ya insa job kupigwa jiwe mpaka kukaribia kupoteza maisha, mfano huyo Mtu mmoja ajulikanae kwa jina la Gaga alikuwa akiwaelekeza njia za kupita ambazo kawaanda watu wa kurusha mawe na kila walipopita huko walikumbana na balaa, lakini siku wakipanga kupita njia zao walirejea salama, kampeni ya moshi mjini ilikuwa ni zaidi ya vita yaani Tajiri wa Dsm alipambana na meya wa jijini la moshi huku akisaidiwa na ndesambulo na ibra line katika mazingira hayo usingekuwa kuwa rahisi mgombea wa ccm kushinda moshi mjini.
 
Sera ya CCM ni kukopi na kupaste.Kumbuka ''mabadiliko'', M4C nk. Kwa hiyo CDM wakisema wameibiwa kura [which is true] CCM nao wanacopy na kupaste. Natamani CDM wabuni jambo moja au mawili ya kuwapeleka chaka....wao si wamezoea kukopy,hawana jipya,hawana innovation?.... Sijui naeleweka wenzangu...au
 
Ni kweli,kuna kura ziliokotwa kwenye msitu wa mwanjera zimetiwa tiki kwa upande wa ccm kwenye urais,wabunge na madiwani na zina muhuri wa nec

Ziliibiwa baada ya kuhesabu au kabla? Je kama ni za bandia nani anajua? Ni ngapi
 
Kilichomteketeza Devis mosha ni wale Watu ambao walipenyezwa kwake na ndesambulo na ibra line, hao watu ndio waliokuwa wakimteketeza na kusuka mipango yote ya Uovu juu yake ikiwemo ya insa job kupigwa jiwe mpaka kukaribia kupoteza maisha, mfano huyo Mtu mmoja ajulikanae kwa jina la Gaga alikuwa akiwaelekeza njia za kupita ambazo kawaanda watu wa kurusha mawe na kila walipopita huko walikumbana na balaa, lakini siku wakipanga kupita njia zao walirejea salama, kampeni ya moshi mjini ilikuwa ni zaidi ya vita yaani Tajiri wa Dsm alipambana na meya wa jijini la moshi huku akisaidiwa na ndesambulo na ibra line katika mazingira hayo usingekuwa kuwa rahisi mgombea wa ccm kushinda moshi mjini.

mkuu acha kulidanganya taifa na uma kama wewe sio mkazi wa mosh tulia.devis mosha alianza vizuri sana hapa mosh.ila tatizo lake kubwa lililomponza ni pupa na paniki kama sio mwanasiasa.alianza kupiga wananch waliokua wakitembea na tshrt za ukawa na bendera maeneo ya mjini kati stend ya mboya na kiborlon.na hii ilikuja baada ya chadema kuanza kupiga wimbo.wa yahya wa ladyjayd wimbo ulimfanya aende polis kushtaki kua anaimbwa polisi walimtimua kwakua wimbo hautaji jina lake japo maneno.yanamgusa.pili aliposhindwa hilo akaanza tabia akipita akiwanyoshea vijana dole gumba vijana wanamuonyesha ile ishara ya chadema alafu akifanyiwa hivyo anatuma mabausa wake kupiga vijana.mbaya zaid siku aliyokuja lowasa mosh jion yake aliongoza mabausa wake juwapiga na kuwavua nguo watu wote waliovaa nguo za chadema au kubeba bendera kwenye pikipiki nyumba na nk.wanawake walivuliwa tsht usiku huo wengi sana.polis walifika mida ya saa tatu na vijana hao walikimbilia kusikojulikana tulishirikiana na polis wanaume tulikesha usiku kucha tukiwatafta na tulifanikiwa kuwakamata vijana watano na kesi zao bado zinaendelea.devis aliwatukana wamama wa soko la kiborlon soko alilojenga ndesa na akawaahidi.kua akipita atawahamisha.pia aliwaambia wananch kua watake wastake yeye ndiye mbunge wa mosh mjini.siku moja kabla ya kura zilikamatwa box 30 za kura njia panda mbatia akiwemo wakaandika maelezo na kuzikabidh polis tulipata taarifa na tuliweka ulinz wawananch wenyewe kila kituo katika mkoa huu watu tulisambaa ikumbukwe kura zile zilishapigwa tiki kwa devis mosh mjin na wa mosh vijijin na makufuli.tuliweka ulinz mkubwa sana na vituo.vinafunguliwa saanane usiku tulikagua viti vyote walivyovileta kwenye vituo vyote.siku ya kura tulikamata kura mosh vijijin usiku wake tulikamata mosh mjin.na magar yaliyobeba kura hizo la mosh mjin lilichomwamoto na la vijijin wananch waliliharbu halifai hata kunyoosha.kwamazingira hayo kura hizo hizo unazosema nizile walizotaka kuiba ikashindikana kuziingiza.hata matokeo aliyopata bado upo wizi ndani yake ameiba.hakuna mtu aliyekua anamtaka mosh hapa.hatua za mwisho kila alikokua anapita watu walikua wanamzomea.na mikutano yake yote ya kampen zaid kafanya pasuatu na pasua ndio ya kwanza kutoa matokeo na alipigwa mbaya.sasa kaibiwa wapi?
 
Back
Top Bottom