Stroke
JF-Expert Member
- Feb 17, 2012
- 34,675
- 40,927
Kipindi cha JK gap la walionacho na wasiokuwa nacho lilikuwa kubwa sana na walionacho walikua wanafuja tu mali za uma.Kosa la Kikwete ni kwamba hakuandaa mtu thabiti wa kugombea urais. Na mtu anaeandaliwa ni vyema asijijue kama Kamati juu Ina ajenda nae. Mfano mzuri ni Mkapa alikuwa ameandaliwa kwa mrefu(i.e alikuwa anamuandalia mwalimu hotuba na alikuwa anaiwakilisha nchi yetu kama waziri wa mambo ya nje vizuri Sana. Mpaka mwalimu alimuita Mr Clean. Japo kwa kiasi chake alibadilika alipopata Urais) lakini alikuwa hajui kama atakuwa chaguo la Kamati kuu. JPM alibahatika kutokana na kukosekana mtu thabiti wa kugombea. Lowassa alikuwa anakubalika na wengi lakini sio kamati kuu na Membe hakuandaliwa vizuri (i.e uwekezaji haukufayika wa kutosha kwake).
Chama kilipoteza ushawishi kutokana na vitendo vya wazi kabisa Vya kifisadi vilivyokuwa vinafanyika na hakuna aliyekemea.
Maisha yalikua magumu na maskini ambao walikua wengi walizidi kuwa mafukara huku matajiri wachache wakiendelea kuwa matajiri wa kutupwa.
Magu alijitahidi kulevel mambo ila hakumaliza kazi.
Kama kusingekuja aina ya leadership ya Magu, sasa hivi tungekuwa katika civil war.
Maana mateso ya watu wa chini kama yangeendelea kwa miaka mitano zaidi toka JK tungeshuhudia the first civil unrest in Tanzania.
Na vita ingekua baina ya Maskini na matajiri.
Ungeona tu masikini wakivamia nyumba za matajiri kuzichoma, kuwadhuru na kujitwalia mali.
Ila sasa hao wanaojiita wenye chama hawajui tu kuwa wanaturudisha into the same same situation tuliyokuwa 6 years ago.
And i am telling you kama hawataacha huu ujinga wao we are heading into a disaster.